Ndege za UFO/UAP's zimethibitishwa zinaweza kutembea kwa spidi ya ajabu, km 64,000 kwa lisaa, DAR Hadi MWANZA kinatumia dakika 1 na sekunde Moja.

Ndege za UFO/UAP's zimethibitishwa zinaweza kutembea kwa spidi ya ajabu, km 64,000 kwa lisaa, DAR Hadi MWANZA kinatumia dakika 1 na sekunde Moja.

Kwa hiyo wanamaanishq Marekani ndio kitovu cha dunia kwamba Aliens na UFOs vionekane kwao tu na si kwingineko?

Kwanini huku kwetu hatuvioni hivyo vitu? Kwa jinsi Watanzania wanavyopenda umbea hizo taarifa zingekuwa zimejaa mitaani.
 
Ni kweli, ambazo sio za kusadikika ni zile mnazozipenda za wanaojitikisa matako kule TikTok na Instagram
zisizo za kusadikika ni kuwa nyonya damu chinjachinja mkuu aliuwa watz kwenye mo29 na kukimbia na maiti zao. Na machawa wake wanashangilia na kumshangilia ili wapate chochote. Hata aliens na ufo zao hawana unyama wa hivyo
 
Nimekua nafuatilia sakata hili la UFO ama Aliens majina ambayo yamezoeleka na wengi kua ni viumbe ambavyo inasemekana vipo vinaishi na sisi SEHEMU ambayo pengine binadamu wa kawaida hatuwezi kufika pengine bila msaada wao.

Sakata hili naona limechukua sura mpya Sasa huko marekani Kuna watu wanakuja front kuelezea ukweli wa mambo baada ya nguvu kubwa kutumika ama inayoendelea kutumika kuzuia taarifa za UFO zisifike duniani watu wajue.

Wadau hao ambao asilimia kubwa walikua ni watu wa jeshi maafisa wa ngazi za juu, wako kwenye vita ya kutaka mswaada upitishwe kwenye seneti ya marekani kua taarifa zote zinazohusu viumbe hao ziwekwe hadharani Dunia ifahamu, ili siku ikitokea la kutokea kila mtu ama kila nchi ijue itajilindaje na hao viumbe.

Baadhi ya maofisa hao walikua kwnye program za Siri, ila Sasa wameamua Kuja front, wengi wao wameshakutana nao hao viumbe wakiwa hai ama wamekufa, kukuta ndege zao zimedondoka, vyote hivyo viko mahala vinalindwa

Hawa maafisa wa jeshi wanasema Kuna vitengo kabisa vya Siri vipo ikiwemo CIA, na wengineo, kazi yao ni popote pale ambapo Kuna ishu ya UFO imetokea hata iwe temeke ama mbagala rangi tatu, hao jamaa CIA jeshi wa hiko kitengo watakuja na kuchukua kila kinachohusiana na UFO wataondoka wakiwaacha mnang'aa macho. Popote duniani wanafika. Upande wa mtu kuchukua labda video ya kitu kama UFO hio Haina shida kinaweza tu kikapatikana hata kwenye socio media mana wanajua watu wata share kwaio kuipata ni chap, ila ya ndege za UFO kudondoka ama viumbe wapo kwenye hio ndege, ni chapu tu jamaa watakuja huko huko mliko.

Anyway Sasa tuachane na hio, Mimi nilistaajabishwa na jambo kwenye program hizo za Siri ambazo walikua wameshakutana ama kuona hizo UFO, mojawapo ya ndege zao hao viumbe walikua wanaitrack kwenye rada zao, wanadai hio ndege inakimbia spidi ya maili elfu 40 kwa lisaa, ambayo ni kilometa 64,000 hivi, kwamba Hawa jamaa wanaweza kuizunguka Dunia nzima kwa dakika 37 na sekunde 21....maafisa hao wanasema hawajawahi kuona spid ya namna hio hata ndege zao hypersonic hazina spidi hio, wanadai Hawa viumbe Wana teknolojia pengine za hatari kuliko kitu chochote, ndio mana walikua wanahimiza uwazi mambo watu waambiwe ili wajue.

Kwenye hiko kitengo Kuna ambao waliweza kwa kias flan kukaribiana na viumbe hao, wamepata kitu kama ugonjwa wa ngozi na mifumo yao kimwili haiko sawa kama ilivyokua mwanzoni, wengine wakiwa kwenye military base ndege zile hua zinakuja ghafla zinaelea angani ama Hilo eneo kwa muda halafu zinapotea.

Eeeh hatari.
Ulimwengu wa sasa unagubikwa sana na uongo na propaganda, lakini tuamini tu kuwa teknolojia ambayo sisi tunaijua hivi sasa ni teknolojia iliyopitwa na wakati kwa watafiti ambao wametengwa kwa ajili ya tafiti tu za kisayansi na teknolojia, kuna wenzetu wapo mbali sana katika mambo haya, hizo tunazoambiwa ni Unidentified Flying Object (UFO) sidhani kama ni product za Alliens, bali ni sisi wanadamau ndiyo tumetengeneza hayo mambo kutokana na usiri mkubwa wa hizi teknolojia ndiyo tunaaminishwa hizo story za holywood.
Dunia inaongozwa na maarifa yaliyogawanywa kwa makusudi. Tunachojua sisi ni kile tunachoruhusiwa kujua.
Na hadithi nyingi za UFO zinaeleweka zaidi kama matokeo ya usiri wa binadamu, si wageni wa anga.
 
zisizo za kusadikika ni kuwa nyonya damu chinjachinja mkuu aliuwa watz kwenye mo29 na kukimbia na maiti zao. Na machawa wake wanashangilia na kumshangilia ili wapate chochote. Hata aliens na ufo zao hawana unyama wa hivyo
Nenda basi kamuue kama una hasira sana. Si unajua alipo...?! Zanzibar tu hapo.
 
Alien technology
Kwakweli teknolojia ya ajabu Sana. Inawaogopesha hata marekani kwamba nchi yoyote kati ya zile super powers ikiipata itakua tishio hata kwao
Mbona technology ipo tayari, makombora ya ICBM yanaenda Hadi speed ya Mach 20 ingawa hayajafika bado hapo kwenye 64000kph
 
Back
Top Bottom