Ndege zetu ziko wapi, Kwenye kusafirisha mazao kwenda Ulaya?

Ndege zetu ziko wapi, Kwenye kusafirisha mazao kwenda Ulaya?

Hivi majuzi Kenya walionekana wakisafirisha mbogamboga na matunda kuelekea kwenye masoko ya Ulaya kwa kubadili matumizi ya ndege za aboria kuweza kubeba mizigo kufuatia upungufu wa abiria.

Hatua ya kupata masoko hayo imekuja baada ya mataifa mengi kusimamisha shughuli kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Corona COVID-19.

Hapa nyumbani napo hatukubaki nyuma baada ya Naibu waziri Hussein Bashe kupost picha ya Waziri Wa Kilimo Japhet Hasunga akiwa kwenye ndege akipakia mizigo. Na tani 37 za mazao zikisafirishwa kwenga Ubeligiji.

Jana shirika la ndege la Ethiopia limeweka taarifa ya kupata tenda ya kusafirisha mazao kutoka Tanzania kuelekea nchi za Ulaya.

Swali la msingi ni je ndege zetu tulizogharamikia mabillioni ya shilingi ziko wapi?
Ni mbovu? Hazina vibali? Au ni kukosa maarifa kwa viongozi?

Je, huu sio wakati muafaka wa ndege zetu kufanya kazi ya kuitambulisha nchi katika safari za anga?

Waliokuwa wanapinga mradi wa ndege je serikali inachochote cha kujitetea baada ya aibu hii?


Sent from my iPhone using JamiiForums
Usafiri wa ndege siyo sawa na wa barabara ambapo Musukuma Bus Service toka Geita na abiria mmoja na kufika Chato limejaa abiria, mbuzi, kuku, samaki n.k. na kurudi likisanya shehena mbalimbali hivyohivyo. Watu walihoji busara ya kupeleka mbuzi tani 3 Dubai na kurudi na hostages tu bila hata ngamia mmoja. Utapeleka ndege Ubelgiji na tani 20 za mbogamboga na kurudi na Coronavirus pekee italeta faida kwa Shirika na nchi? Watu hawakupinga kununuliwa ndege, wengi tulihoji busara ya Rais kununua hizo ndege kwa niaba ya ATCL wenyewe wanaozihitaji. Wengi wanamkumbuka Mwingira Waziri aliyeleta zile ndege mbili za kukodi toka Lebanon ambazo hazikuruka tena baada ya kuwasili. Mwingira alitumbuliwa kwa kutia hasara Serkali, kwa hili nani atumbuliwe ndege na mbawa zao haziruki?
 
Biashara ya ndege sio kama matoroli leo unawapa wabeba matofali ujenzi ukiisha unawapa wauza maji.
Ndege zetu ni za abiria wala sio za mizigo. Kuifanya ndege iwe ya mizigo ni process ndefu mno na inataka upate kibali tena baada ya kuibadili. Pia sio kila ndege unaweza ifanya iwe ya mizigo.
Vilevile ni lazima kampuni iliyotengeneza iridhie au ndo ibadilishe matumizi ya ndege hiyo.

Tukija kwenye biashara. Huwezi toa bidhaa zako hapa nchini kupeleka Ulaya bila kujua unampelekea nani. Hili sio soko la Mabibo kuwa utapeleka viazi mbatata umwage chini waje watu usiowajua wanunue. Ukipeleka mzigo nje ya nchi lazima ujue unampelekea nani. Na lazima kuna mikataba isainiwe ndo maana huwezi ona apple zinatolewa SA kupelekwa Europe wakati wanachama wa EU wanazalisha pia. Hutokaa uone maziwa yanatoka Kenya yanaenda Ulaya wakati Netherlands na nchi kibao kule wanazalisha ya kutosha.

Na kwanza sijui kama hata ndege za ATCL zina kibali kuruka Ulaya, kama kipo ni upuuzi mtupu maana kibali unakilipia wakati hakuna ndege inaenda.
Utalipiaje king'amuzi wakati huna Tv.
 
Akili zako bado zimegungwa na mawazo ya kijima kwamba kwenda ulaya ndo Kuna pesa..si nyie mliponda ndege kupeleka nyama ya mbuzi..Sasa mmeibuka mnataka zisafirishe kisbu nachicha!!!
 
Biashara ya mbogamboga ni mikataba nafikiri
Kenya ni lazima walete Ulaya kwa sababu ni biashara ya muda mrefu na inahitajika
Hatuwezi kujua wanalipanaje kwa sasa kama ni kati ya serikali ya [emoji636] na wafanyabiashara hatujui ila ni lazima tupate nyanya jamani
Tukipakia holela yataishia kwenye skip

Sent from my iPhone using Tapatalk

Ishu sio biashara maana mazao yetu mbona yanapelekwa na ethiopia airways


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kiukweli kwangu mm Mtz mwenye uelewa mdogo, ninashindwa kuelewa naposikia leo ndege haina vibali, ilhali ndege hiyo tulionyeshwa ilibeba shehena ya mbuzi?? Na mapichapicha ya ushahidi...
Au ilikuwa ujanjaujanja??...
Danganya toto??

Everyday is Saturday....................... 😎
 
Back
Top Bottom