EllySkyWilly
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 2,204
- 2,085
Habari ndugu zangu, marafiki na watanzania kwa ujumla. Natumai muwazima wa afya tele.
Leo nitakwenda kuelezea umuhimu wa ndege katika taifa letu ambalo sasa linatambulika kimataifa na kupewa heshima kubwa sana baada ya kupata Rais mwenye maono na mpenda maendeleo.
Kabla sijaanza kuchimba kwa kina nitaanza kuelezea jinsi ambavyo ndege zetu zimefanya mambo muhimu mawili katika kipindi cha corona. Ikumbukwe katika kipindi cha corona ndugu zetu na watanzania wenzetu walikwama India na China kwasababu ya ukosefu wa Usafiri wa ndege kwasababu ya kuzuiliwa kwa ndege kuruka.
Ikumbukwe ni ndege zetu hizi hizi zilizokwenda kuwachukua ndugu zetu huko na kuwarudisha hapa kwetu Tanzania. Barozi zetu ziliwasiliana na barozi za China na India zikakubaliana ndipo watanzania wenzetu wakaenda kuchukuliwa.
Ili watanzania wenzetu waweze kuchukuliwa ilihitajika ndege moja kubwa non stop yenye uwezo wakubeba idadi kubwa ya watu. Ilitakiwa hivyo ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya corona. Hivyo kwa idadi ile kubwa wa watanzania, ndege yetu kubwa ndio ilikuwa dawa tosha kabisa. Watanzania wenzetu walisafiri salama salimi bila kusimama njiani wala bila kusumbuliwa mambo ya visa na passport kwenye vituo tuo vya humo dubai mara doha mara Hongkong. Usumbufu wote huo ungesababisha kuenea kwa korona na kuchelewesha safari.
Mpaka hivi navyo kwambia kuna watu wa baadhi ya mataifa bado wamekwama nchini India na China kwasababu nchi zao hazina ndege. Nchi hizo mfano mzuri ni Liberia n.k.
Kwa hilo kubwa napenda kuchukua wasaa huu kuipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya kiongozi mahiri Mhe. Dkt. John Magufuli. Kwa heshima zote Mungu awabariki sana kwasababu tusingekuwa a ndege ndugu zetu, watanzania wenzetu, wafanya biashara, madaktari wetu, watoto wetu wangekwama China na India kama walivyo kwama raia wa mataifa mengine.
Ni raha sana kupanda ndege ya moja kwa moja mpaka nyumbani Tanzania.
Sasa naomba niendelee wandugu nilikua kunywa chai
Nimeongelea ndege zetu kwenda kuchukua watanzania waliokwama huko nje kipindi cha corona, Mtanzania asiye na ndugu nje anaweza asinielewe kabisa ni ni ni namaanisha. Sasa naomba ufuatane na mimi point kwa point.
1. Wamarekani waliokuwa wamekwama nje ya Marekani kipindi cha corona, walifuatwa na ndege za Marekani na kurudishwa nyumbani. Sio kwamba Marekani hawakuwa na ndege za mashirika binafsi rahasha zilikuwepo. Lakini kumbuka mashirika yale yalisimamisha uendeshaji wa safari kipindi hicho. Hivyo hata sisi tusingekuwa na ndege zetu hayo mashirika binafsi yasingekubali. Ni nani anapenda wafanyakazi wake waugue corona? ni nani angekubali kuwaweka rubani wake kwenye danger zone?Jibu ni hayupo.
2. Mwili wa Baba wa Taifa ulifuatwa Uingereza na ndege za shirika letu mwaka 1999, haikupewa precision air kuufuata mwili wa mwasisi wa Taifa hili. Unajua kwanini?Ni ili kulinda heshima ya mzee wetu.
3. Ndege ni utambulisho na fahari ya Taifa Ndio maana kachorwa twiga ubavuni. Ndege zetu ndio zitafanya kazi ya kuitangaza Tanzania mahali pote duniani kwasasa.
4. Ndege hutumika sana katika nchi za viwanda kwa ajili ya kusafirisha bidhaa ghali lakini zenye kuweza kuharibika mapema (perishable goods).
5. Ndege hizi zinazonunuliwa miaka ya sasa zitakuja kuwa na faida nyingi tu miaka kadhaa ijayo.
Hivyo wandugu stay tuned good things are coming.
Nitaendelea............. stay tuned.
Ngoja nile ngoma ya Rais wa Afrika kwanza then nitarudi.
Tuseme tu ukweli nchi ambazo hazina ndege, viongozi wao ni washamba wa utandawazi. Wanatakiwa wafundishwe jinsi ya kushiriki katika utandawazi kama taifa.