Ndegevita za Urusi zalipua maghala ya silaha za Ukraine

Ndegevita za Urusi zalipua maghala ya silaha za Ukraine

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Vikosi vya anga vya Urusi vimeharibu vituo vya muda vya kuweka silaha na maghala ya risasi karibu na mji wa Artemovsk huko Donetsk, Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema hapo jana ( Alhamisi).

Hadi wafanyikazi 350 wa Ukraine na magari 20 ya kivita yaligongwa kwenye eneo hilo, kulingana na wizara.

Wizara hiyo iliongeza kuwa jeshi la Ukraine limepata hasara kubwa baada ya mashambulizi ya Urusi kwenye maeneo ya mapigano, huku jumla ya majeruhi wa kikosi cha 24 cha mechanized takriban 2,500, na kikosi cha 79 cha mashambulizi ya anga kikipoteza zaidi ya asilimia 80 ya wafanyakazi wake.

Hakuna taarifa inayopatikana kwa upande wa Kiukreni kwa sasa ili kuthibitisha majeruhi na uharibifu.
 
Kwenye vita mbona hiyo kawaida tu ila yeye mrusi akishikwa kalio kidogo tu sio kulalamika huko.
kweli kabsa tena analialia Sana akiguswa kidogo tu lakini cha kushangaza hawamgusi , wanapiga kelele za mbali Kama hivi ngoja nikuoneshe.

"Huyooo huyooo huyooo apigweee apigweee huyooo huyooo aliapigwee" ila cha ajabu hawasogei zaidi ya kurudi nyuma tu na kusukuma tusilaha twao kwa mbaliii.
 
[emoji16][emoji16] NATO watagoma kupeleka silaha zao sasa , Kila wakipeleka Zina bomolewa tu
Unadhani kisa cha Boris Johnson kufukunyuliwa u-PM atoke No 10 ni nini?

Ukiwauliza kwa nini sasa hivi hawapokei silaha kutoka Marekani na NATO, kama ilivyokuwa awali, wanakwambia, ^It's a tactical move.^ Eti hawataki kumwambia adui wamepokea silaha au silaha gani. 🙂

Wakati ambapo mwanzoni, vita vikianza, kwa kutangaza hadharani kwamba silaha nzitonzito zinatoka Magharibi na NATO, walidai Russia angenywea na kuweka silaha zake chini na kusalimu amri. Hivi sasa wameamua kubadili gia angani.
 
Hv kati ya Russia na Ukraine nani analialia sana
Wanakwambia Ukraine analia kwa maana ya ^tactical expression,^ ili dunia isitambue mapema kinachowapata Russia kwa kupigika ile mbaya, ikaja kuwasaidia. Yaani, kwa maelezo ya comedian mwenyewe, anasema eti ni sawa na kumshushia mtu kichapo huku sub-woofer umeifungulia sauti full throttle.

So, wanasema wanataka wambamize hadi Putin aombe urai wa Ukraine. Labda ni kweli. Ngoja tungoje tusubiri tuone.
 
Ngoja Annunaki MK254 waje watakwambia anategwa mtu aingie kingi
MK254 jibu lake la kila siku atasema mbona mmeshindwa Kyiv kuiteka kwa siku tatu,,,kumbe kadri siku tunavyozichelewesha ndo unaona kina Borison wanapiga mweleka,,rubble inapepea[emoji1787]
 
Back
Top Bottom