Ndejembi: Tusiogope kutumia “talent” tulizonazo nje ya ofisi za Serikali

Ndejembi: Tusiogope kutumia “talent” tulizonazo nje ya ofisi za Serikali

informer 06

Senior Member
Joined
May 11, 2024
Posts
184
Reaction score
170
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ametoa wito kwa wizara na baadhi ya taasisi za Serikali kuwatumia watu wenye vipaji na ujuzi mbalimbali waliopo nje ya Serikali, hususan vijana wanaofanya vizuri katika maeneo yao ya kazi (field), kwa kuwapa nafasi ya kutoa uzoefu wao na kuchangia katika shughuli za Serikali.
IMG_4022.jpeg

Akizungumza leo Oktoba 28, 2026 katika hafla ya utiaji saini wa leseni za utafutaji wa mafuta na gesi katika vitalu vya Mnazi Bay Kaskazini, Songo Songo Magharibi na Lindi–Mtwara, Ndejembi amezitaka wizara na taasisi na mashirika ya Serikali, hususan Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juuwa Petroli (PURA) kuhakikisha vijana na watu mbalimbali wenye ujuzi na uzoefu wanapewa nafasi ya kuchangia katika sekta hiyo.

“Tusiogope kutumia “talent” ambazo tunazo tukajifungia sisi wenyewe ofisini tukakaa tukajua sisi tuna utalaamu sana kuliko wale ambao wako kwenye field” amesema Ndejembi


Aidha, amelitaka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na wadau wengine kuhakikisha Watanzania wanaandaliwa mapema ili wanufaike na fursa zinazotokana na miradi inayoendelea kutekelezwa na ile inayotarajiwa kuanza nchini, badala ya kusubiri hadi miradi hiyo ianze ndipo waanze kuweka mikakati ya kuwaandaa.

Amesema ni hatua ya kihistoria kwa TPDC kupewa leseni za kutekeleza moja kwa moja shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi katika vitalu husika, akibainisha kuwa hapo awali leseni hizo zilikuwa zikitolewa zaidi kwa wawekezaji. Ameeleza kuwa kwa sasa TPDC ina uwezo wa kutekeleza shughuli hizo kutokana na uwepo wa wataalamu na uwezo wa kitaasisi.

Hata hivyo, amelitaka TPDC kuhakikisha masharti ya leseni hizo yanazingatiwa, ikiwemo masuala ya usalama, utunzaji wa mazingira na kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa kuzingatia maslahi na manufaa ya wananchi, hususan wale wanaoishi katika maeneo husika.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mussa Makame, ameishukuru Serikali kwa uamuzi wa kulipatia shirika hilo leseni za utafutaji na uendelezaji wa vitalu vya mafuta na gesi. Amesema uamuzi huo utaliwezesha TPDC kuongeza ushiriki wake katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za mafuta na gesi nchini.
IMG_4021.jpeg

Amesema Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini kinaendelea na uzalishaji, huku shirika hilo likitarajia kufanya utafiti wa kina na kuanza uchimbaji wa kisima. Kuhusu Kitalu cha Eyasi–Wembere, amesema TPDC imekamilisha uchambuzi wa taarifa za utafiti wa mitetemo ya ardhini wa pande mbili (2D) na inatarajia kufanya utafiti wa pande tatu (3D).

Kwa upande wa Kitalu cha Songo Songo Magharibi, Makame amesema shirika hilo linakaribia kukamilisha uchambuzi wa taarifa zilizopo ili kubaini uwezekano wa kitalu hicho kuwa na manufaa kibiashara.

Amesisitiza kuwa mafanikio katika sekta ya mafuta na gesi hayatapimwa kwa ugunduzi wa rasilimali pekee, bali pia kwa namna rasilimali hizo zitakavyotumika kuleta tija na kuunda fursa za kiuchumi kwa wananchi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia, Dk. James Mataragio, amesema Serikali imeamua kuipa TPDC leseni hizo kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika sekta ya mafuta na gesi asilia.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nishati, Dkt. Juma Zuberi Homera, amesema utiaji saini wa leseni za utafutaji wa mafuta na gesi unaipa TPDC mamlaka ya kumiliki na kusimamia vitalu vyake, hatua aliyoitaja kuwa mwanzo wa ukurasa mpya katika maendeleo ya shirika hilo.
 
Back
Top Bottom