Zawadi inaweza kuleta matokeo hasi au chanya. Kama haitaratibiwa vizuri zawadi inaweza kuwa destructive, ndio maana zawadi zote zinawekewa vigezo vya wazi vya kuipata au kuikosa. Huwezi kukurupuka from no where na kumpa binti yako zawadi eti yeye ndiye kaleta kibiriti cha kuwashia moto jikoni na kumuacha yule aliyepika chakula na kutenga mezani. Ukifanya hivyo familia itakusingizia mabaya kwa huyo binti yako uliyempa zawadi kwa sababu za kipumbavu kabisa.
Walioleta furaha ya wazi kwenye mechi ile ya Simba na Singida ni Kichuya aliyejipinda dakika ya 3 tu ya mchezo na kufunga bao safi kabisa, akifuatiwa na Okwi na Kwasi, kila mtu alishangalia kwa raha hata yule asiyekuweko uwanjani. Mfano, kama Ndemla angecheza vizuri kama alivyoona kiongozi wake wa Simba lakini Simba ikafungwa au kutoa sare na Singida bado hiyo zawadi ya gari angepewa Ndemla? Ni ujiinga tu. Mbona Mapinduzi cup hakutoa zawadi, hakuna mchezaji aliyecheza vizuri mechi zote zile?