Ndemwai utomvu wenye thamani kubwa ya dawa

SOUND HEALTH

Member
Joined
Jul 8, 2014
Posts
82
Reaction score
25
Mnamo mwaka 2012 nilichomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya chini ya ukucha wa dole gumba mguu wa kushoto.kwa kweli sikuona ni kitu gani kwa kuwa eneo hili lilikuwa na maji kutokana na mvua zilizokuwakuwa zimenyesha.baada ya siku mbili kidole kikavimba sio uvimbe mkubwa nilipojaribu kukamua hakikutoa usaha bali maji tokea hapo ikawa ni mateso maumivu makali pamoja na kutumia madawa mazito(antibiotics) na mengi kuosha sehemu iliyoathirika juhudi haikuzaa matunda.nikapima sukari ikawa normal,nikapima mpaka HIV nikakutwa niko safi.tatizo lile liliniathiri sana kisaikolojia mpaka siku moja nilipokutana na bwana mmoja mtu wa Manyara.
Yule bwana alinipa dawa kidogo kwenye kichupa akaniambia inaitwa NDEMWAI.Akaniambia nipake na na kunywa matone mawili,baada ya kufanya hivyo nikaona mambo ya ajabu kweli ,kidole kilianza kuvuja maji yenye harufu mbaya sana, hali hiyo iliendelea usiku kucha siku iliyofua hali ya kuvuja maji ikakoma baada ya hapo nikapona mpaka leo hii.

dawa iliyobaki nilimpa jamaa mwingine ambaye alisumbuliwa na jeraha nyuma ya goti kwa zaidi ya miaka mitatu bila mafanikio NDEMWAI ikamaliza hilo kabisa.nilimpigia simu jamaa wa manyara ili aniletee japo hata lita 20.jamaa akaniambia haiwezekani kwa sababu ile dawa inapatikana kwa tabu msitu wa NDEMWAI WAMEPEWA WAWEKEZAJI wa nje.wanavuna huo utomvu kupeleka ughaibuni.ombi langu wana jf naomba jina la NDEMWAI Kwa english ili nigoogle zaidi kupata umashuhuri na faida zaidi za mti huu ndemwai.maana niki google ndemwai naambulia patupu.ndugu zangu inaonekana huu mti ndemwai una thamani kubwa sana ya dawa.
 

Kupata lita 20 ni kazi sana
 
Ulitaka lita 20 zote hizo za nini au ulitaka kufanya biashara? Badala ya kuwaelekeza watu kwa mtu aliyekuponya wewe unataka kuifanya iwe dili lako. Hata mimi ningekuambia mti huo haupatikani. Tujifunze kuwapa rizki watu wanaotusaidia tupunguze tamaa
 
Ni kweli kabisa hii ndemwai ni bonge la dawa hata kwa meno ni nzuri mnoo... kupatikana kwake ni shida haswa
 
Wenye maelezo watupe zaid
Unatibu pumu,bawasili,matatizo yote ya meno na fidhi pamoja na kinywa,ini,pararaizi,tezi dume,kuongeza cd4,magonjwa yote ya zinaa sugu na yasio sugu, kunyoosha kizazi kilichopinda,kuvuta kizazi kilicho mbali,mkanda wa jeshi,magonjwa ya masikio, magonjwa ya macho ikiwa na mtoto wa jicho, magonjwa yote ya ngozi, kunenepesha dhakari, walioathirika na punyeto inarudisha dhakari kwenye uimara wake,vidonda vya tumbo,vidonda vya kuumia (pia nzi asogei kwenye kidonda kilichopakwa ndemwai) pamoja na vile vidonda ndugu nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…