SOUND HEALTH
Member
- Jul 8, 2014
- 82
- 25
Mnamo mwaka 2012 nilichomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya chini ya ukucha wa dole gumba mguu wa kushoto.kwa kweli sikuona ni kitu gani kwa kuwa eneo hili lilikuwa na maji kutokana na mvua zilizokuwakuwa zimenyesha.baada ya siku mbili kidole kikavimba sio uvimbe mkubwa nilipojaribu kukamua hakikutoa usaha bali maji tokea hapo ikawa ni mateso maumivu makali pamoja na kutumia madawa mazito(antibiotics) na mengi kuosha sehemu iliyoathirika juhudi haikuzaa matunda.nikapima sukari ikawa normal,nikapima mpaka HIV nikakutwa niko safi.tatizo lile liliniathiri sana kisaikolojia mpaka siku moja nilipokutana na bwana mmoja mtu wa Manyara.
Yule bwana alinipa dawa kidogo kwenye kichupa akaniambia inaitwa NDEMWAI.Akaniambia nipake na na kunywa matone mawili,baada ya kufanya hivyo nikaona mambo ya ajabu kweli ,kidole kilianza kuvuja maji yenye harufu mbaya sana, hali hiyo iliendelea usiku kucha siku iliyofua hali ya kuvuja maji ikakoma baada ya hapo nikapona mpaka leo hii.
dawa iliyobaki nilimpa jamaa mwingine ambaye alisumbuliwa na jeraha nyuma ya goti kwa zaidi ya miaka mitatu bila mafanikio NDEMWAI ikamaliza hilo kabisa.nilimpigia simu jamaa wa manyara ili aniletee japo hata lita 20.jamaa akaniambia haiwezekani kwa sababu ile dawa inapatikana kwa tabu msitu wa NDEMWAI WAMEPEWA WAWEKEZAJI wa nje.wanavuna huo utomvu kupeleka ughaibuni.ombi langu wana jf naomba jina la NDEMWAI Kwa english ili nigoogle zaidi kupata umashuhuri na faida zaidi za mti huu ndemwai.maana niki google ndemwai naambulia patupu.ndugu zangu inaonekana huu mti ndemwai una thamani kubwa sana ya dawa.