Ndigana kali (east coast fever)

achengula

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2009
Posts
369
Reaction score
62
Ndigana Kali ni ugonjwa hatari unaowapata ng’ombe ukiwa na dalili ya homa kali, kuvimba kwa matezi, upumuaji wa shida na vifo vingi hasa kwa ndama. Ni ugonjwa unaoenezwa na kupe wanaojulikana kitaalamu kwa jina la ‘Rhipicephalus appendiculatus’ wanao beba vijidudu vya ugonjwa vinavyoitwa Theileria parva kundi la protozoa. Kupe hawa ni wale wanaopatikana kwenye masikio la ng’ombe wakiwa na rangi ya kahawia (kupe sikio kahawia). Maelezo zaidi juu ya ugonjwa huu soma hapa SEKTA YA MIFUGO TANZANIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…