achengula
JF-Expert Member
- Jul 30, 2009
- 369
- 62
Ndigana Kali ni ugonjwa hatari unaowapata ngombe ukiwa na dalili ya homa kali, kuvimba kwa matezi, upumuaji wa shida na vifo vingi hasa kwa ndama. Ni ugonjwa unaoenezwa na kupe wanaojulikana kitaalamu kwa jina la Rhipicephalus appendiculatus wanao beba vijidudu vya ugonjwa vinavyoitwa Theileria parva kundi la protozoa. Kupe hawa ni wale wanaopatikana kwenye masikio la ngombe wakiwa na rangi ya kahawia (kupe sikio kahawia). Maelezo zaidi juu ya ugonjwa huu soma hapa SEKTA YA MIFUGO TANZANIA