.
nipo kwenye mahusiano tangu mwezi wa 6 mwishoni baada ya kukaa muda mrefu bila mtu,mungu ni mwema kweli huyu shemeji yenu mpya alinipenda na kunijali ingawa kazi yake ni kuwa busy karibu wiki nzima kasoro j2 tu ndipo anakuwa free na alijitahidi sana kuwa nami na kuspend siku hiyo nzima ya j2 kwenda sehemu mbalimbali na mm ili hata tupumzike na kubadilishana mawazo mbalimbali,haikuishia hapo pia alijitahidi muda wa kazi kunipigia simu muda mwingi kunijuza anapoenda kwaa muda huo hata na mengineyo hope mnajua penzi la kwanzakwanza linavyokuwaga tamu na motomoto ila nasikitika kuwaambia kuwa mwezi wa nane nilipata taarifa za babayangu kupata ajali ikanipasa niende nyumbani mara moja kumcheki baba then baada ya wiki moja nilirudi kuendelea na kazi lakini kwa bahati mbaya tena baada ya kama wiki mbili nilipata tena taarifa baba yangu mkubwa kaanguka ghaflana kufariki hivyo nilienda tena nyumbani na baada ya wiki 2 nilirudi kazini na hapo ndipo nilipoanza kuona tofauti za huyu shemeji yenu kwani inaweza kupita hata siku nzima asinipigie wala kutuma meseji na kila ninapomuuliza anasema anakuwaga busy muda mwingi au huwa anakuwa na bosi wake kama binadamu kuna kummiss mpenzi wako so nimejaribu kumuomba hata tutoke tuongee nijue nn shida anakuwa na visingizio jamani na kwa bahati nzuri tupo wote katika jengo moja,