Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Naam,
Kueleke mechi ya uchaguzi tayari wachezaji wote timu zote wapo uwanjani wanapasha misuli kabla ya kurudi vyumba vya kubadilishia nguo ili watoke rasmi na kuingia uwanjani kusubiri kipenga cha refrii ili kabumbu lianze.
Mpaka sasa kabla ya mechi wachezaji wameanza mazoezi ya kuonesha namna watafanya faulo za makusudi, naam, mechi inaonekana kuwa ya kutumia nguvu na si ufundi
Wachmbuzi wanasema inatarajiwa huenda mchezo ukamshinda refarii maana hali ya mchezo presha iko juu sana ukizingatia msimamo wa ligi ni kama hauleleweki kila mmoja hataki kushuka daraja anataka kuwa kileleni huku kuna mshabiki wa timu wanasema kileleni hawashuki hata kama wakifungwa mechi zote wanajua namna watapata pointi labda ni utani wa kishabiki au ndio ivyo tena.
Kuna wale walioanza kuvujisha mbinu za makocha kuelekea mchezo huku timu pinzani zikijipanga kuwa hawatakubali kuona refa anatoa penati ya nje ya boksi nao wanasema wako tayari kwa lolote ili mradi wahakikishe refa hachezi rafu kwenye sheria zilizowekwa.
Kama vipi tupia mavideo ya kutosha tuwaone wachezaji kabla mechi kuanza ili tujuwe mchezo tuutazame uwanjani au tusubiri matokeo tu kwenye Tv.
Pia soma:Kuelekea 2025 - Kitendo cha Mahakama kwenda kutoa hukumu ya TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni kuzidi kubariki uovu wa CCM