Ndio wasomi wenyewe hawa..

Oooh Miafrika! Mingine imeshaanza kuchinjana kule Nigeria....
 
Kwa Tanzania watu wanaoishi vizuri kwa mishahara na maslahi bora kabisa ni WANASIASA wakifuatiwa kwa karibu kabisa na wasomi wetu hawa. Siwashangai wanapoipuuza TUCTA ambayo imejaa wafanyakazi wa kawaida.Wasomi wetu wana machapisho, safari nyingi tu za nje, miradi mingi tu ya kila namna, ajira zao wenyewe mbali na hizo vyuo, NGOs nyingi kama REDET, ESAURP,....ambazo zinamwagiwa mapesa mengi tu na wafadhili.....Wakichoka kidogo wanaingia kirahisi CCM wanakuwa Wabunge halafu mawaziri akina Prof Kapuya, Prof Maghembe. Mnatarajia wagome kweli?
 
Mwanakijiji kwa taarifaa tuu hapa nchini Tanzania, WASOMI (Walioenda shuleni na vyuoni) ndio kikwazo cha mabadilko ya kweli ya kumkomboa mtanzania halisi kutoka lindi la umaskini unaosababishwa na utawala mbovu.

Wasomi wa Tanzania ukiachilia mbali unafiki wa nafsi zao pia ni mbumbumbuu wa haki yao (zao) za msingi katika nchi yao. Kwao wao ajira, mishahara ya kujenga na kununua gari na nguao, kunywa, kuchanga harusi, kupata vyeo mbali mbali ni kikomo cha furaha yaoo.

Ukosefu wa huduma bora kama maji, umeme, barabara, afya, chaguzi huru na za haki haziwagusii kifikra zaidi ya kuzitumiaa tuu kujijengeaa umaarufuu kijamiii wa kuzijadilii.

Wakoloni walitoa elimu ya ubaguzi kwa kuandaa makundi katika jamii kwa maana ya watawala (wazungu), watumishi (waafrika), wasimamizi (wahindi/waarabu) nasi tumerithi kwa kuwa WASOMI WA KUPENDA KUTAWALA TUUUUUU.
 
Wasomi ndio wanaiharibu hii nchi.Ukiangalia leo jinsi tulivyoiuza uza kimtindo nchi yetu kwa wawekezaji, wasomi wana mchango wao wa hali na mali.Ndio maana siku hizi foleni za kwenda nje kutafuta wawekezaji zimekuwa nyingi. Kumbe wakati jamaa wanajaribu kuwatafuta wawekezaji, ukweli wa mambo ni kwamba kila mtu kwenye msafara ule anajaribu kuangalia atapata kiasi gani kutoka kwa wawekezaji either as a local partner au through assistance kutoka kwenye kampuni zao.
Wizi mtupu huu usomi. As if hatuna vichwa vya kufikiria kisomi. Lol
 

Wilcard, ukweli ni kuwa vyama hakuna...
Ubabaishaji mtupu, hali hii inaendela kuchagiza ukaondoo wa wanachama!!
 
Sasa mnataka kufosi wagome if its not in their interest its not in their interest. This is an issue of interest not all a moral issue.
 
Ah kazi kweli. Hivi wasomi ni watu gani? Tunamaanisha wanataaluma yaani wanaofundisha vyuo vya elimu ya juu au kuna kundi jingine? Hapa JF kila mtu anaonekana kuwa ni msomi maana katika nchi yetu, wengi wenye access ya mtandao ni wasomi. Kwahiyo hizo lawama ni kwa walimu wa vyuo peke yao au kuna kundi jingine! Maana naona umasikini wa miaka yoote hii unaelekezwa kwao.
 
Wasomi wanaozungumzwa hapa ni wanataaluma, wanaofundisha katika vyuo vikuu. Hawa ni kikwazo kikubwa sana cha maendeleo ya kijamii lakini tujiulize tumefikaje hapa tulipo?!

Mimi na wewe tumechangia! Tanzania, tofauti na nchi nyingine nyingi wanataaluma wamejengewa u-Mungu mtu na wasomi wa kati (graduates wa shahada moja au mbili wasio wana taaluma na wanafunzi wa vyuo hivi pamoja na vyombo vya habari).

Utakuta Profesa anaongea vitu ambavyo havipo kabisa katika dunia hii ya sasa ila anapigiwa makofi na humu JF watu wazima na akili zao wanatumia calories nyingi kuwatetea kwa kuwa tu ni walimu wa chuo kikuu.

Ukienda kwenye mihadhara hakuna kitu kipya. Profesa mzima anatokwa na mipofu mdomoni kwa kujaribu kuelezea dhana ya Karl Marx, sijui Nyerere sijui nani bila kuonesha ina relevance gani na hali ya mwanakijiji kule Kyela, Lindi na Ujiji. Akimaliza "ku-rap" anapigiwa makofi na kuja kuabudiwa humu kuwa ooooh is a leading scholar ooh is what and what... Magazeti ndiyo usiseme. Yameingia mkenge wa kufikiri kila kinachosemwa na mwanataaluma wa hadhi ya u Dr au Uprofesa ni alfa na omega. GIVE ME A BREAK PEOPLE!!!!! Tunavuna tulichopanda. Serikali lazima in'gan'gane na hawa watu mpaka wavuruge mipango yote ya TUCTA who else can??

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…