Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
- #41
They say.."Never Underestimate the Power of Stupid People in Large Groups"...
they are wrong.. stupidity just got an army!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
They say.."Never Underestimate the Power of Stupid People in Large Groups"...
Mwanakijiji kwa taarifaa tuu hapa nchini Tanzania, WASOMI (Walioenda shuleni na vyuoni) ndio kikwazo cha mabadilko ya kweli ya kumkomboa mtanzania halisi kutoka lindi la umaskini unaosababishwa na utawala mbovu.wakati mwingine mtu anahitaji kuongeza.. vikao baadaya vikao.. majadiliano baaday a majadiliano.. at the end somebody need to take a stand. Ambao wanasema hawatashiriki kwa sababu "hatukushirikishwa" wanatakiwa waachwe pembeni.
Sisi hapa tunazao UAW na tunaamini uongozi wa UAW kitaifa unahitaji kuonesha maamuzi na kuongoza na vyama vyetu vya sehemu mbalimbali vinakaa na aidha kuunga mkono hoja za UAW au la. Hilo linafanywa kwa kutuita wafanyakazi kama tunakubaliana na mgomo ulioitwa na UAW kwenye tawi letu.. karibu mara zote tunakubali na kuwapa nguvu viongozi wetu kutekeleza maagizo ya UAW.
Sasa huo uongozi wa wafanyakazi wa elimu uliwapa wanaowawakilisha haki ya kuamua kushiriki au la au wao kwa vile ni viongozi wameamua kutoshiriki kwa sababu hawakushrikishwa? As a matter of fact kwenye migomo ya wafanyakazi vile vyama vingine vinajiunga na mgomo kwa sababu vinakubaliana na malengo ya mgomo huo siyo kwa sababu vilishirikishwa kwenye vikao.
Leo hii walimu wa Chuo Kikuu cha Houston wakianza kugoma kwa sababu ya unyanyasaji na serikali kupinga na jumuiya ya wafanyakazi wa elimu kitaifa ikaitisha mgomo, usidhani kiila vyuo vikuu vitataka vishirikishwe kwenye maamuzi. Kitakachofanyika ni kuwa vyuo vingine vitaamua kushiriki (kwa sababu wanakubaliana na mgomo) au la.
Ndio utasikia "Chama cha Wafanyakazi chuo kikuu cha michigan kimetangaza kuunga mkono mgomo wa wafanyakazi huko Houston mpaka matatizo ya wenzao yametatauliwa"..
Ndio maaana kauli ya vyama vya wafanyakazi duniani ni kuwa "Workers of the World Unite!".. sasa hawa wapuuzi (i mean that) wanapoamua kutoshiriki mgomo kwa sababu hawakushirikishwa wanatakiwa watimuliwe na wanachama wao mara moja kwa sababu wameweka ujiko wao mbele kuliko kanuni za msimamo wa pamoja katika kudai maslahi. Ni watu wa hatari katika kuendeleza maslahi ya wafanyakazi..
Don't even get me started kwenye haya ya wafanyakazi...
Kwa Tanzania watu wanaoishi vizuri kwa mishahara na maslahi bora kabisa ni WANASIASA wakifuatiwa kwa karibu kabisa na wasomi wetu hawa. Siwashangai wanapoipuuza TUCTA ambayo imejaa wafanyakazi wa kawaida.Wasomi wetu wana machapisho, safari nyingi tu za nje, miradi mingi tu ya kila namna, ajira zao wenyewe mbali na hizo vyuo, NGOs nyingi kama REDET, ESAURP,....ambazo zinamwagiwa mapesa mengi tu na wafadhili.....Wakichoka kidogo wanaingia kirahisi CCM wanakuwa Wabunge halafu mawaziri akina Prof Kapuya, Prof Maghembe. Mnatarajia wagome kweli?