NDIYO BASI TENA: Yanga itasota kuvunja rekodi hizi za Simba

NDIYO BASI TENA: Yanga itasota kuvunja rekodi hizi za Simba

Mkuu, hayo ndio mambo ya msingi. Hivi timu ikifika fainali au robo fainali ya mashindano fulani, wanapewa kikombe gani?

Simba wanayo kazi ya kuipita Yanga (sijui mwaka upi) kuchukua ubingwa wa nchi toka 18 hadi 24. Angalia hapo kuna tofauti ya miaka sita. Sijui kama Yanga itakuwa imelala ikisubiri Mikia wafike hapo. Na bahati nzuri au mbaya, siku hizi kuna Azam na Mbeya City na wengine wanaweza kuibuka!

Rekodi za Simba ambazo Yanga hajazifikia, ndiyo heading yake! Hayo mengine hayahusu heading ya mtoa uzi
 
Endeleeni kubishana. Hii post ya uzi huu nimeiona mapema sana, nikaangalia knowledge gap nikakosa, nikajiuliza mleta uzi alitaka kufikisha ujumbe upi na kwa nani? Sikuona rationale au justification ya post ndefu kama hii. Kuendelea kubishana hapa ni matumizi mabaya ya muda na bando za intaneti.

Ngoja niwaache wafu wazike wafu wao, Yanga ndiyo kiboko yao! Wengine ni waigizaji tu na wakwapuzi wa vikombe vya mtaani.

Kwa kipi ilichonacho?
 
Ukifika fainali tu, hata kama ukifungwa.. Unapewa heshima kwa kupewa medali, mkwanja mrefu pia utakumbukwa milele na vizazi vijavyo.. tofauti na wale wanaobaki kariokoo wakinywa kahawa na kashata... Na ukifika nusu au robo fainali unapata mkwanja mrefu tu.
Angalia CV's za klabu duniani hakuna wanapoandika mwaka Fulani tuliishia robo fainali au mwaka fulani tulifika fainali.wanaongelea miaka waliochukua makombe tu
 
Angalia CV's za klabu duniani hakuna wanapoandika mwaka Fulani tuliishia robo fainali au mwaka fulani tulifika fainali.wanaongelea miaka waliochukua makombe tu

Mkuu inategemea wewe upo interested na kitu gani katika hiyo CV.. Mfano sisi tunayetaka kujua kila kitu kuhusu Simba Sc, lazma tujue hata zile mechi tulizoishia 1st raundi.
 
Pia Yanga haiwezi kuvunja rekodi ya Simba ya kushika mkia daraja la kwanza(kwasasa ligi kuu)na kuponea chupu chupu kushuka daraja baada ya kubebwa na Yanga.
 
Mtoa p0st ameikuta hii habar kwenye Mwanaspoti akainyanyua kama ilivyo kuileta humu akidhani analeta jambo la maana kumbe!!!!!! rekodi kama hizi zinaandikwa tanzania peke yake.
 
Kumaliza ubishi twendeni website ya CAF tuangalie viwango vya ubora wa vilabu vya Afrika....tuone Simba na Yanga zipo nafasi zipi.....
 
CAF lazima Simba ipo juu ya Yanga. Unabisha kaangalie.
 
Ukweli mchungu, ila ndio hali halisi hiyo! Sioni rekodi hizi zikivunjwa zaidi ya kuimarishwa zaidi.
 
Unamaanisha nn ,"kusema yanga ndio basi tena" kwani mwisho wa dunia kesho kutwa,? Rekodi ya kushinda goli tano inaweza kuvunjwa ka dakika ngapi.Na aliye chukua ubinwa mara 18,atatumia miaka mingapi kufikiarekodi ya aliyechukua ubingwa mara 24..usinipe jibu

Ndio rekodi pekee ya nyie kujivunia, ebu tuongee rekodi za sisi kwa sisi! Hivi ktk kizazi chetu unafikiri 5-0 zitakuja rudi, au tufanye 6 za 1970s.
 
Mkuu, hayo ndio mambo ya msingi. Hivi timu ikifika fainali au robo fainali ya mashindano fulani, wanapewa kikombe gani?

Simba wanayo kazi ya kuipita Yanga (sijui mwaka upi) kuchukua ubingwa wa nchi toka 18 hadi 24. Angalia hapo kuna tofauti ya miaka sita. Sijui kama Yanga itakuwa imelala ikisubiri Mikia wafike hapo. Na bahati nzuri au mbaya, siku hizi kuna Azam na Mbeya City na wengine wanaweza kuibuka!

Kaangalie rekodi za CAF, utaikuta simba kama moja ya timu chache zilizofika fainali ya CAF. Sio la kubeza hili. Kushindana na timu bora zaidi Simba iko juu, haina ubishi! Ni kweli ligi kuu rekodi yenu ni zaidi yetu na itachukua muda kuivunja.
 
Mtoa p0st ameikuta hii habar kwenye Mwanaspoti akainyanyua kama ilivyo kuileta humu akidhani analeta jambo la maana kumbe!!!!!! rekodi kama hizi zinaandikwa tanzania peke yake.
wewe ulitaka tuzitoe wapi mkuu? zile za yanga kulalamika kupigwa ngeta kama kisingizio baada ya kushindwa zinatoka wapi? ukweli no kwamba simba iko bora mara 100 yenu timu ya washirikina
 
Unamaanisha nn ,"kusema yanga ndio basi tena" kwani mwisho wa dunia kesho kutwa,? Rekodi ya kushinda goli tano inaweza kuvunjwa ka dakika ngapi.Na aliye chukua ubinwa mara 18,atatumia miaka mingapi kufikiarekodi ya aliyechukua ubingwa mara 24..usinipe jibu

Kipi bora kati ya hivi, kushinda kikombe kimoja tuu mara nyingi au kushinda vikombe tofauti mara nyingi? Nafikiri hapa, utake usitake Mnyama anatisha! Ndio hali halisi hiyo.
 
Back
Top Bottom