NDIYO BASI TENA: Yanga itasota kuvunja rekodi hizi za Simba

NDIYO BASI TENA: Yanga itasota kuvunja rekodi hizi za Simba

Kaangalie rekodi za CAF, utaikuta simba kama moja ya timu chache zilizofika fainali ya CAF. Sio la kubeza hili. Kushindana na timu bora zaidi Simba iko juu, haina ubishi! Ni kweli ligi kuu rekodi yenu ni zaidi yetu na itachukua muda kuivunja.
hizo rekodi kama za livapool tu,endeleeni kupigania nafasi yenu ya tano kama kawaida yenu
 
Unamaanisha nn ,"kusema yanga ndio basi tena" kwani mwisho wa dunia kesho kutwa,? Rekodi ya kushinda goli tano inaweza kuvunjwa ka dakika ngapi.Na aliye chukua ubinwa mara 18,atatumia miaka mingapi kufikiarekodi ya aliyechukua ubingwa mara 24..usinipe jibu
Kwa kweli yanga wanawachanganya mashabiki wao...
 
Rekodi za Yanga hazina stress maana hata paragraph moja haijai...

Mkuu grafani11 yanga i hovyo sana

Wamekomaliwa na Ruvu shooting eti wanaanzisha hoja eti wameonewa

Eti wanaanza na magazeti yao kama kawaida..Kujifanya kwamba wamefanyiwa hila...this time hakukuwa na Uchawi

Watu wanakufa uwanjani sembuse hicho kijijeraha cha tambwe.
Makoye Matale acheni kutafuta visingizio...mpira sio kama kazi ya kuuza mayai
 
Malizia na mapendekezo "Recommndations" na kuweka marejeo "References" ya ulikochota hizi habari
 
Ukifika fainali tu, hata kama ukifungwa.. Unapewa heshima kwa kupewa medali, mkwanja mrefu pia utakumbukwa milele na vizazi vijavyo.. tofauti na wale wanaobaki kariokoo wakinywa kahawa na kashata... Na ukifika nusu au robo fainali unapata mkwanja mrefu tu.
Huo mkwanja umesaidia vipi club kuonekana tofauti na club zingine katika nyanja za vitega uchumi
 
Huo mkwanja umesaidia vipi club kuonekana tofauti na club zingine katika nyanja za vitega uchumi

Tangu mwaka 1993 hadi leo ni yapata miaka 22 imepita.. pia zimepita awamu 4 za viongozi, na kila awamu wanakuja na muono wao.. Hivyo ni ngumu kuanalyse kipi kilifanyika kipindi hicho.
 
Huo mkwanja umesaidia vipi club kuonekana tofauti na club zingine katika nyanja za vitega uchumi
Hata tukiamua kuwagawia wachezaji, viongozi au washabiki wote zote kama shukrani yao nyinyi haiwahusu, kinachoongelewa hapa ni uwezo wa timu kuweza kupeperusha bendera ya nchi mpaka fainali.

Swala la fedha ziko wapi hilo sio mada iliyopo mezani, ya ndani nyumba ya pili yaachwe kwa wenyewe, hapa tunaongelea heshima katika soka la Afrika bila kuitaja Simba SC / Mnyama bado haijaandikwa...
 
Vijana wa Simba 1977
Simba ilikuwa inatisha mwaka 1977 ambapo kikosi chake cha kwanza kilikuwa cha kipa Omar Mahadhi, mabeki wa kulia Daud Salum na kushoto Mohammed Kajole. Mabeki wa kati Athumani Juma, Aloo Mwitu na Mohammed “Tall” Bakari. Viungo wa nyuma Aluu Ally na Iddi Kibonye na mbele ni Ezekiel Grayson “Jujuman”, Ismail Mwarabu na Abdallah Mwinyimkuu. Kulia ni Willy Mwaijibe na Abbas Dilunga na kushoto ni Martin Kikwa.
Wafunga mabao walikuwa Abdallah “King” Kibaden, Adam Sabu na Jumanne Hassan Masmenti “Tarzan”. Mbele ya kikosi hiki mtu ukitoka ilikuwa bahati. Ndicho kikosi kilichoifunga Yanga 6-0 mwaka huo.
 
Hata tukiamua kuwagawia wachezaji, viongozi au washabiki wote zote kama shukrani yao nyinyi haiwahusu, kinachoongelewa hapa ni uwezo wa timu kuweza kupeperusha bendera ya nchi mpaka fainali.

Swala la fedha ziko wapi hilo sio mada iliyopo mezani, ya ndani nyumba ya pili yaachwe kwa wenyewe, hapa tunaongelea heshima katika soka la Afrika bila kuitaja Simba SC / Mnyama bado haijaandikwa...
Mie member pale msimbazi nilikuwa ninam-challenge member mwenzangu tu ili next time atoe way forward kwa viongozi pindi mkwanja unavyoingia klabuni maana ukiona viongozi wanakimbilia kuwagaia wachezaji ukute nusu inaangukia kwa viongozi
 
Vijana wa Simba 1977
Simba ilikuwa inatisha mwaka 1977 ambapo kikosi chake cha kwanza kilikuwa cha kipa Omar Mahadhi, mabeki wa kulia Daud Salum na kushoto Mohammed Kajole. Mabeki wa kati Athumani Juma, Aloo Mwitu na Mohammed "Tall" Bakari. Viungo wa nyuma Aluu Ally na Iddi Kibonye na mbele ni Ezekiel Grayson "Jujuman", Ismail Mwarabu na Abdallah Mwinyimkuu. Kulia ni Willy Mwaijibe na Abbas Dilunga na kushoto ni Martin Kikwa.
Wafunga mabao walikuwa Abdallah "King" Kibaden, Adam Sabu na Jumanne Hassan Masmenti "Tarzan". Mbele ya kikosi hiki mtu ukitoka ilikuwa bahati. Ndicho kikosi kilichoifunga Yanga 6-0 mwaka huo.

Dah.. umenikumbusha mbali sana.. hii gemu king kibaden aliondoka na mpira wake baada ya kutupia 3 nyavuni.
 
Rekodi za Yanga hazina stress maana hata paragraph moja haijai...
Ha ha ha hahahahahhahahahhahahah, da umefanya nilogin kucheka kucomment kicheko. Ni kweli sana sana watakwambia tu.


'Yanga imechukua ubingwa wa Tanzania bara mara 24 hivyo ni mabingwa wa kihistoria na wapinzani wetu wa jadi wamechukua mara 18 na imewahi kufika hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika ingawa haikushinda mechi hata moja'

Sasa hapo kuna haja ya kuandika paragraph mbili kweli?
 
Back
Top Bottom