NDIYO BASI TENA: Yanga itasota kuvunja rekodi hizi za Simba

NDIYO BASI TENA: Yanga itasota kuvunja rekodi hizi za Simba

Ha ha ha hahahahahhahahahhahahah, da umefanya nilogin kucheka kucomment kicheko. Ni kweli sana sana watakwambia tu.

'Yanga imechukua ubingwa wa Tanzania bara mara 24 hivyo ni mabingwa wa kihistoria na wapinzani wetu wa jadi wamechukua mara 18 na imewahi kufika hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika ingawa haikushinda mechi hata moja'

Sasa hapo kuna haja ya kuandika paragraph mbili kweli?
Hata ukurasa mmoja wa note book ndogo haujai, sana sana baada ya kuona ligi imekuwa ngumu kwao sasa wametafuta sababu ya kujitoa kwenye ligi sababu ikiwa ni ya kitoto kabisa. Eti Amis Tambwe amekabwa uwanjani, kwani TFF-YANGA haipo?

1. Mbona Simba mchezaji wao Okwi aliwahi kupasuliwa kichwa na mchezaji wa JKT Oljoro uwanja wa Amri Abeid Arusha Simba haikukimbilia kauli za kujitoa ikaacha sheria ichukue mkondo wake.

2. Wakati Simba ikicheza na Toto Afrika mwaka juzi, Haruna "Boban" aliwahi kufanyiwa makusudi na polisi wa Mwanza- CCM Kirumba. Wakati Boban anamiliki mpira Polisi Yanga wakamwachilia mbwa akaanza kumfukuza Boban. Mbona Simba haikukimbilia kutoa kauli za kujitoa? Hayo ni kwa uchache tu, mengi yapo.

Maonezi ambayo Simba imekuwa ikifanyiwa uwanjani nadhani ingekuwa ni Yanga wangekuwa wameshahama na nchi.
 
Mie member pale msimbazi nilikuwa ninam-challenge member mwenzangu tu ili next time atoe way forward kwa viongozi pindi mkwanja unavyoingia klabuni maana ukiona viongozi wanakimbilia kuwagaia wachezaji ukute nusu inaangukia kwa viongozi
Mkuu tuko pamoja...
 
Dah.. umenikumbusha mbali sana.. hii gemu king kibaden aliondoka na mpira wake baada ya kutupia 3 nyavuni.
hii game ilikuwa kali sana, mpira ulichezwa ktk dimba la Nyamagana ktk jiji la mwanza, sikuwepo kipindi hicho ila mzee wangu (R.I.P) alikuwa na Tape ya hiyo mechi iliyotanganzwa na RTD, Basi siku za jumapili alikuwa akituwekea kuisikiliza na ndipo mapenzi yangu kwa simba yalipoanza kuchipukia! mwaka 1994 ndio kwa mara ya kwanza nilienda uwanjani pale shamba la bibi na mzee wangu tukiwa na jezi zetu za simba kwenda kucheki mechi ya simba na yanga, siku hiyo yanga alipigwa 4 kwa 1 , mfungaji wa goli pekee la Yanga alikuwa ni beki kisiki wa kirundi Costantine Kimanda, siku hiyo hiyo nilimpoteza rafiki yangu kipenzi tuliyekuwa tunasoma naye darasa moja baada ya kugongwa na gari maeneo ya kipawa uwanja wa ndege wakati wakiwa barabarani kushangilia ushindi wa Simba
 
Pole sana mkuu...kwa minajili hiyo lazima uwe simba damu mkuu
 
Umesahau na ile ya mechi 5 point 5 magoli 5 na kufungwa goli 5 na nafasi ya 5
 
Ingekuwa Poa kama tungejadili Maendeleo ya Club badala yakujadili Historia ambazo hazina manufaa katika club zetu. Wenzetu wanashindana kwa club kuwa na vitega uchumi gani,Kuingiza Pato gani,Kuchukua vikombe vingapi sisi tunabakia simba kamfunga yanga mara ngapi,kafika final mara ngapi

Kwa watu wanaojua maendeleo ya mpira hawawezi weka mambo kama hayo hata siku moja..

Tufike wakati tuwe tunajisifia kuwa club imechukua vikombe vya cuf mara ngapi,Kagame mara ngapi,Tusker mara ngapi, Na ligi marangapi?

Au Club inamiliki viwanja vya kisasa vingapi,Majengo ys biashara mangapi,Na inavitumia vipi kujiingizia kipato nakuendeleza club.

Au ni pato gani kwa mwaka inaingiza Club na inalitumia vip hivi huwa tunajiuliza haya tunapoamua kuleta mada kama hizi au tunaandika tu kwa ushabiki? Mwisho wa siku tunaishia hapahapa EAfrica.

Wapi uwanja wa bunju ambao tuliahidiwa ndani ya siku 100ungekuwa umekamilika nasasa mwaka nafikiri kama hauja isha bas unakaribia kuisha na hakuna dalili zozote zaidi ya kuufyeka?

Wapi majengo ya kibiashara yanga ambayo kila siku tunaahidiwa kuwa unaanza na miaka inazidi kusonga?

Nitakushangaa sana endapo utakuwa uki jisifia kuwa mara tumemfunga yanga Goli 6,mara tumefika Final caf wakati ukiangalia maendeleo ya Club ni masikini wa kutupwa na hadi wachezaji inafika wakati mwingine tunashindwa kuwalipa!!

Ni wakati sasa Yanga na simba tukafikiria na kushindania maendeleo ya Clu na sio Kufungwa na kufungana tuige mfano wa nchi za jirani tu mfano Kongo,Hata,Kenya,SA,UG nk. Wote hawa wanashindana kwa maendeleo ya Club na Soka kwa ujumla sisi tumebaki Kushindania kwenye Mapinduz,Ligi,MJ,Zaidi ya Hapo hakuna Jipya.

Ni Hayo tu
 
Makendaa haya pia ni mafanikio lazima tuyajadili
 
Last edited by a moderator:
Makendaa haya pia ni mafanikio lazima tuyajadili
Mafanikio Yapi wakati tuko hapahapa tanzania Hata Africa tu Hatujajulikana, Kuwalipa tu wachezaji ni shida Mafanikio yako wapi ikiwa hata kujenga tu uwanja wa mazoezi tumeshindwa?
 
Kumaliza ubishi twendeni website ya CAF tuangalie viwango vya ubora wa vilabu vya Afrika....tuone Simba na Yanga zipo nafasi zipi.....
Ile Database hawa update. Ni ya mwaka 2011.

Cha kushangaza kuna club fulani ya Morocco inaonyeshwa ipo juu ya Zesco United lakini cha kushangaza hiyo klabu hivi sasa ipo ligi daraja la pili.
 
Simba SC, ndiyo timu pekee hapa nchini Tanzania iliyoweza kuchukua kombe la,
Mtani Jembe, Mara zote hadi hao Nguvu ya Soda ya Pepsi walipoamua kuigomea ligi hiyo na kusababisha Simba SC kukosa mpinzani.
 
Alafu huku kwenye sports,hatupendi stress,kutuwekea makala ndefu ka treni huku hatupendagi
Usitake na wengine wawe na uvivu wako wa kusoma.Na inawezekana unareflect kiwango cha usomi kilichomo Yanga;kimsingi Yanga ina waso kiduchu sana ukilinganisha na Simba.
 
Record nyingine simba haitaweza kuvunja record ya yanga ya kuwa ccm damdam
😁😁😂👏 uko sahihi mkuu.Ongezea nondo nyingine;Simba hawatavunja rekodi ya Yanga ya kucheza pekupeku au tumbo wazi.Na halikadhalika Yanga hawatavunja rekodi ya Simba ya kuwa timu ya kwanza kucheza na viatu au kuvaa jezi.
 
Nahisi hata wakati Simba wanacheza hiyo fainali hukuwepo,nani alikudanganya Simba walipewa fedha kwa kufika fainali?
Usimtishe mwenzako.Unataka kuniambia Simba hawakupewa fedha baada ya kushika nafasi ya pili fainali ya CAF 1993?Nilikuwepo uwanjani na ninaelewa yaliyotokea kabla na baada ya fainali hiyo.
 
Usimtishe mwenzako.Unataka kuniambia Simba hawakupewa fedha baada ya kushika nafasi ya pili fainali ya CAF 1993?Nilikuwepo uwanjani na ninaelewa yaliyotokea kabla na baada ya fainali hiyo.
Ulikuwepo uwanjani Simba wakipewa zawadi ya kufungwa 2-0 na Bolizozo
 
Back
Top Bottom