Ndiyo tuheshimu kauli ya Rais, lakini ni ile isiyokinzana na sheria! Vinginevyo tutatembea gizani

Ndiyo tuheshimu kauli ya Rais, lakini ni ile isiyokinzana na sheria! Vinginevyo tutatembea gizani

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Rais tumemchagua sisi wenyewe kwa mujibu wa katiba. Anaongoza serikali na nchi kwa jumla kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi kwa ujumla wake. Kutokumtii Rais ni kuwadharau wananchi na kutokuitii katiba ambayo imemweka madarakani. Huo ni upande mmoja wa shilingi. Upande wa pili ni kwamba Rais kuongoza nchi kinyume na sheria au kutoa maagizo yaliyo tofauti na sheria zilizopo ni kutokuitii katiba na wananchi waliomweka madarakani. Rais ni mtumishi wa watu na ana haki kwa mujibu wa katiba kuongoza nchi kwa manufaa ya wananchi. Kama akafika mahali akaona kwamba anataka kutoa maagizo yatakayokuwa na manufaa kwa wananchi wake, lakini kwa sasa maagizo hayo yanaonekana kukinzana na sheria zilizopo, basi ufanyike utaratibu wa kikatiba wa kufanyia marekebisho sheria hizo ili zitoe uhalali wa maagizo ya Rais kutekelezwa bila kuvunja sheria.

Kwa hiyo kama Rais ameona ni kero na haina tija kwa wananchi kudaiwa malimbikizo ya kodi, tukubali kuwa kupanga ni kuchagua!! Basi yaandikwe mapendekezo ya marekebisho ya sheria ihusuyo ukusanyaji wa kodi unaofanywa na TRA. Hawa TRA wapigwe marufuku kwa mujibu wa sheria KUDAI MALIMBIKIZO YA KODI kwa wafanyabiashara wote, na siyo wa kariakoo tu (sheria ni msumeno), halafu tusikilizie utamu wake!! Vinginevyo itakuwa akidaiwa malimbikizo ya kodi mfanyabiashara aitwaye MUHOGO MCHUNGU halitatoka tamko la kusema TRA wasimdai malimbikizo ya kodi, lakini akidaiwa malimbikizo ya kodi mfanyabiashara aitwaye MUHOGO MTAMU, fasta litatoka tamko la kusema TRA wasimdai malimbikizo ya kodi.

Lingine (AMBALO NDIYO KIINI CHA MAWAZO YANGU), naomba tusiwe tunapotosha au tunatafsiri vibaya kauli na matamko ya Rais wetu mpendwa. Siamini kabisa kuwa Rais ametoa tamko la kuzuia TRA wasidai malimbikizon ya kodi, kama ni hivyo atawezaje kutekeleza mipango ya serikali?. Ila ninaamini kuwa hakubaliani na namna inayotumiwa na TRA kukusanya hayo malimbikizo ya kodi. Hakubaliani na TRA kufunga biashara za watu kwa kisingizio cha malimbikizo ya kodi. Rais anataka TRA na Wafanyabiashara wakae pamoja wazungumze namna rafiki ya kulipa hayo malimbikizo na si kwa kutumia mabavu ya kufunga biashara zao. Biashara zikifungwa serikali itapata wapi mapato yake? Hiyo pesa ya kulipa MISHAHARA MINONO YA TRA ITATOKA WAPI?

Maana haiingii akilini, ninyi TRA mlikuwa wapi hadi mfanyabiashara huyu MUHOGO MTAMU/MUHOGO MCHUNGU akalimbikiza kodi kwa miaka kadhaa? Picha ninayoipata ni kuwa baadhi ya watumishi hawa wa TRA waliridhia mfanyabiashara huyu alimbikize kodi kwa kuwa alikuwa anawapa kitu kidogo (japo inasemekana TRA hupokea kitu kikubwa, ila Polisi ndio hupokea kitu kidogo-sina uhakika na hilo).
 
Kweli kabisa wafanyabiashara wadogo Sheria itaendelea kuwatesa, serikali ya awamu ya 6 haiwajali wanyonge kabisa
 
Duniani kote ELIMU ya kodi hupewa kipaumbele.......

Watanzania hatupendi kulipa Kodi, inawezekana ikawa ni ukosefu wa elimu.....bila ya mkazo wa elimu kwa mlipa kodi basi kazi huwa bure tu.

Ni wafanyakazi tu wanaolipa kodi kupitia MISHAHARA yao, ingekuwa ni hiyari yao basi kwa mwendo tulionao kamwe WASINGELIPA.

Nchi inajengwa na wananchi.

Hakuna wa kutujengea nchi yetu.

Tutoe elimu ya mlipa kodi na inapolipwa itumiwe IPASWAVYO.

Ujanjaujanja hautotufikisha tutakako....tumekuwa watu wa kufanya kazi/biashara kwa kutaka tu TUPATE TUPATE TUPATE bila ya kuifaidisha jamii.

Hebu tujifunze kwa mataifa ya wenzetu waliwezaje/wanawezaje kupata KODI STAHIKI.

#SiempreJMT[emoji120]
 
Hizo ni kauli za kisiasa tu, malimbikizo ya Kodi yanadaiwa na Maafisa wa tra kwa mujibu wa sheria ya Kodi,na mwenye mamlaka ya kusamehe Kodi yoyote ama malimbikizo yake ni Raisi kupitia waziri wa fedha.

Wizara ya ardhi imekuwa kwenye mchakato wa kusamehe wamiliki wa viwanja malimbikizo ya Kodi baada ya kulipa deni la msingi, ambapo mwisho ilikuwa mwezi wa nne na waliofanya malipo hayo nyaraka zilitumwa Dodoma toka Halmashauri zote nchini,kwa utekelezaji.

Hadi leo hayo malimbikizo ya Kodi yanasoma kwenye mfumo kwa wamiliki wote waliokuwa na madeni, wanasema ni mchakato kufuta hayo madeni🤔🤣Nani anataka kupoteza ugali wake?

Wafanyabiashara wa kkoo wajitahid kulipa hayo malimbikizo unless kuwe na mabadiliko kwenye sheria zainazosimamia kodi, simple 🙏
 
Halafu hao wanaodaiwa malimbikizo ya kodi wachunguzwe tuone kama wana vinasaba na viongozi wakuu serikalini. Inakuwaje mtu analimbikiza hadi mamilioni yanayokimbilia kuwa bilioni! Ni dhahiri huyu hakuwa na mpango kabisa wa kulipa kodi akijua atalindwa!
 
Kukwepa kulipa kodi ni sawa na mtu kukwepa kufanya kazi lakini huku akitarajia kuwa ataendelea kula!! Haviendi pamoja!! Hatuwezi kukwepa kulipa kodi halafu tukategemea tuendelee kupata huduma za jamii toka seikalini kama kawaida!! Huwezi ukaamua kuila keki yako halafu iendelee kewepo!! Msingi wa tatizo la kukwepa kodi nchini kwetu ni ukosefu wa elimu ya uraia hususani ukosefu wa elimu ya kodi. Tunafundisha watoza kodi tena katika ngazi ya juu ya elimu lakini hatufundishi kabisa walipa kodi toka ngazi ya chini ya elimu. Tufundishe uzalendo wa kulipa kodi toka shule za chekechea!!
Tuchukie wakwepa kodi kama tulivyokuwa tunachukia makaburu wa afrika ya kusini! Makaburu walikuwa na siasa ya ubaguzi wa rangi. Ukiwa mwafrika ni kwamba polisi wanaruhusiwa kukukamata wakati wowote maana waliamini muda wote mwafrika lazima atakuwa na hatia tu. Sheria yao ilisema "you are guilty in lieu of your black colour unless you prove it otherwise". Ukiwa mweusi una hatia tu mpaka utakapothibitisha vinginevyo. Kwa hiyo tuliwachukia sana makaburu. Nyimbo mashuleni kuanzia shule za msingi zilikuwa zinahusu ubaya wa makaburu. Ukienda JKT kwenye zoezi la range/kulenga shabaha, ile sanamu ya mtu anayengwa tulikuwa tunaambiwa ni kaburu!!
Hali kadhalika mkwepa kodi ni adui mkubwa wa Taifa na ni kikwazo cha maendeleo ya Taifa. Tuwafundishe watoto kuwa ni aibu kubwa kukwepa kodi, ni uovu mkubwa kukwepa kulipa kodi, ni usaliti mkubwa kukwepa kodo. Mkwepa kodi achukiwe kama alivyokuwa anachukiwa kaburu!! Vinginevyo vijana wataendelea kutamani ajira zenye mwanya wa kula rushwa, wizi na ufisadi wa mali ya umma na kukwepa kodi. Pesa ya serikali nim pesa yako kupitia kodin yako. Ukiamini hivyo huwezi kuiba pesa ya serikali kwa sababu utaona ni sawa na kujiibia wewe mwenyewe!.
 
Back
Top Bottom