Kimey
JF-Expert Member
- Mar 25, 2009
- 4,117
- 833
VIPIMO vya kimaabara vya wanasayansi nchini Marekani vimebaini kuwa ndizi zina virutubisho maalumu viitwavyo BanLec ambavyo viko sawa na aina mbili za dawa zinazotumika katika kuzuia kuenea kwa virusi vya ukimwi.
Wanasayansi hao wamesema wanaamini virutubisho hivyo vya BanLec ni muhimu na vinaweza kuokoa maisha ya mamilioni ya watu.
Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo ambayo yameripotiwa katika jarida la Biological Chemistry la Michigan, virutubisho hivyo vinatokana na kemikali ambayo inazalishwa kiasili katika mimea ijulikanayo kama âlectinâ ambayo inapambana na magonjwa yanayoikumba mimea.
Watafiti hao wamegundua kuwa lectin iliyo ndani ya ndizi inaweza kukabiliana na madhara ya HIV kwa kuzuia virusi kuingia katika mwili wa binadamu.
BanLec hutumika kama bahasha maalumu ya kuhifadhia protini ambayo hudhibiti kubadilika kwa vinasaba vya vijidudu vya HIV.
Msimamizi mkuu wa jarida la kisayansi kutoka Chuo Kikuu cha Michigan, Michael Swanson alisema: âTatizo la baadhi ya dawa za kudhibiti HIV ni kuwa zinaweza kuzidiwa nguvu, lakini inakuwa vigumu zaidi zinapokuwa na lectin.
âLectin hujiunga na sukari inayopatikana katika nukta tofauti za bahasha za HIV-1, na inadhaniwa kuwa inaweza kuwa na nguvu zaidi ya kuzuia virusi kuikaribia.â
Source: Mwananchi