Ndizi mbivu za nazi

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Mahitaji

Ndizi zilozowiva (mkono wa tembo au mzuzu) 4-5

Hiliki nusu kijiko cha chai

Sukari 1 tablespoon (sio lazima)

Tui bubu kiasi

Tui jepesi kiasi


Custard kijiko kimoja cha kulia

Namna ya kutaarisha

Osha vizuri ndizi na zikate sehemu nne

Toa moyo (ule mstari wa kati ya ndizi)

Panga kwenye sufuria

Weka tui jepesi ila lisifunike ndizi

Weka hiliki kwa juu

Subiria ikichemka weka tui bubu

Karibia kuepua changanya custard na maji kidogo mimina katika ndizi

Acha ichemke dakika 5 alafu epua

Note: Upishi huu haukorogwi bali tu kutikisa sufuria taratibu vichanganyike


 
Za kukaanga pia napenda, hizo sasa nikichelewa kuamka nakaanga faster na chai ya tangawizi nimemaliza

Uzipatie na sausage basi na tomato ketchup juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…