Ndo yavunjika baada ya Kuhamia Masaki

Ndo yavunjika baada ya Kuhamia Masaki

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
kuna video moja nimeiona ikipitumwa ya comedy ambayo ningependa kisa chake nami nikigusie kidogo.
bwana mussa alikuwa akifanya kazi kampuni flan na wazungu kwa muda mrefu na kwa kuwa alikuwa ni mtu mchapakazi na mwaminifu wazungu wakampenda na kuamua kumchukulia nyumba maeneo ya masaki kumwamisha alipokuwa akiishi mwanzo tandale kwa tumbo.shida ikaja week tatu baada ya kuwa wamehamia nyumba hiyo.mke akawa anakosa raha na akaanza kukonda ingawa mle ndani palikuwa na kila kitu. siku moja mussa akiwa amerudi jioni akamkuta mke wake amekaa sebuleni na mizigo yake yote amepark.
mussa: kuna nini mama siwema?
mke : nimevumilia humu ndani nimechoka leo naomba tu talaka yangu nirudi kwetu.
mussa:kwan nimefanya nini au nini kimetokea mke wangu?
mke: maisha ya hapa yamenishinda nisije nikafa bure humu ndani..naomba talaka mi nirudi kwetu?
mussa:mbona sikuelewi?kwan nimefanya nini au kimetokea nini nielezee tafadhali.
mke: nimechoka toka tumehamia hapa week ya tatu hii..mtaa gani huu? mtaa utadhani siku zote tunaomboleza msiba. umepoa utadhani kuna matanga. mtaa nimejaribu kuzunguka zunguka hamna hata wa kunambia habari za mjini. hakuna wa kunambia majirani wetu hapa wanaishije n.k kila mtu yupo busy ukienda kila nyumba wanakuja geini tu wanakuchungulia wanakwambia mama yupo kazini. halafu wanafunga mlango ...mimi nimekaa humu ndani kama mwali. kama bubu sina wa kuongea naye... nimekumbuka tulikotoka tandale kwa tumbo. mtaa ulikuwa na amsha amsha nyingi... asubuh watu mnasalimiana na kupeana habari zilizotokea usiku...habari za kushikwa wachawi,wanga.... utasikia mama chande kaibiwa simu dirishani, utasikia baba chiku kafumaniwa..au unakaa unasikia makelele ukienda unakuta watu wamechukuliana bwana. mtaa dakika chache tu utasikia mwizi mwizi..mnakimbiza mnachangamsha damu... mtaa hazipiti siku mbli tatu ngoma mara mwali anatoka..mara mtu anaolewa..mara kuna ndoa ya mkeka... yaan hakuna kulala. nimezunguka natafuta dagaa wa mafungu hamna, nmezunguka natafuta mihogo hamna.. eeeehh.. huku wapi jaman?nimeshindwa nakaa tu ndani utadhani mwali.... hakuna hata wa kupiga naye story. mtaa umelala..kwa nini nife kwa presha miye humu ndani? siwezi, siwezi nipe talaka yangu nirudi mimi kwa wazaz wangu tanadale kwa mtogolwe au kama vipi turudi tukaishi tandale kwa tumbo. maisha haya ya ufungwa siwezi.kila nyumba geti na fensi..sisi kuku wa kisasa? loooh.. maisha gani haya ka tuko segerea. mi nimeshindwa nataka nirudi kwetu.....siwez mimi kufa kwa kijiba cha roho..nina mambo hata sina wa kumsimulia....mi mwnyewe hata sijui yule bibi khadija ambaye ilikuwa aachane na mumewe kaishia wapi..sijui kama fatma ameshachezwa ngoma au bado... sijui mtoto wa baba mashaka kama alifaulu darasa la saba na wakati alipewa mimba na mzee matukutu... haya yote sababu umekuja kunificha huku. nirudishe baba nmeshindwa maisha haya...niache nirudi kwetu... mi sikuua.
 
Kumbe Tandale kuna raha yake sio.. Dada Sky Eclat ya kweli haya??
Huku kwetu kwanza mchana unapigiwa simu, umepika nini? Ukisema mchuzi wa samaki na wali, unaambiwa huku tulipika pilau lakini Khadija hali basi tunamtuma Rama aje amchukulie Khadija wali na samaki. Rama anakuja na bakuli la pilau pia ni full raha.
 
Nitafutie chumba huko madam
 
Huku kwetu kwanza mchana unapigiwa simu, umepika nini? Ukisema mchuzi wa samaki na wali, unaambiwa huku tulipika pilau lakini Khadija hali basi tunamtuma Rama aje amchukulie Khadija wali na samaki. Rama anakuja na bakuli la pilau pia ni full raha.
Hahaha, maisha ya kijamaa kabisa hayo..

Ndio maana huyo binti amejionea taabu kugongagonga mageti!
 
ha ha ha.. kusikia flan kashikwa uchawi ananyolewa nywele.... au kusikia mama flan ni mwnga... mambo ya kawaida sana mtu kupandisha majini.....

huku mkuu uwe na Imani kamili, kusingiziana uchawi ni kama kawa.
 
anakuta watu wamejifungia hamna muda wa kupiga umbea... anatembea kila nyumba anakuta geti na maandishi kuna mbwa mkali au akifika anatokea dada wa kazi anasema mama hayupo ..akiuliza atarudi saa ngapi anamwambia jioni sana saa moja au mwachie biznez kadi yako. mama wa watu hajui biznez kadi ya nini tena.

Hahaha, maisha ya kijamaa kabisa hayo..

Ndio maana huyo binti amejionea taabu kugongagonga mageti!
 
ha ha ha... nimeipenda na kumbe kiuhalisia wamepika ugali na maharagwe au ugali na misumali ya bati.
Huku kwetu kwanza mchana unapigiwa simu, umepika nini? Ukisema mchuzi wa samaki na wali, unaambiwa huku tulipika pilau lakini Khadija hali basi tunamtuma Rama aje amchukulie Khadija wali na samaki. Rama anakuja na bakuli la pilau pia ni full raha.
 
Hahaaa jamani uswahilini kwetu raha sana mara mwizi huyoooo
 
Back
Top Bottom