Ndoa Hii Inaweza Kuvunjwa??

jamani mbona mnashabikia kuvunjwa kwa ndoa hivi mmemuhuliza kama kuna matibabu yoyote alishawahi kuyafanya wangapi wanatibiwa na wanapona? au ripoti ya doctor inasema hana uwezo kabisa? leo kwake kesho kwako kam si wewe basi hata kizazi chako cha baadae, mwaya mwambie binamu yako amuhangaikie mumewe kama si hospital basi hata tiba mbadala.
 
:flypig::flypig::flypig:Man kiukweli haitaweza kuvunjwa.Sababu ni moja tu 'KIAPO',Alichokiunganisha MUNGU Mwanadamu hawezi kukitenganisha! Kifo pekee ndo kitawatenganisha,La Hasha kama alikuwa ana-dramatize ndo anaweza kumtema mshefa wake huyo.Hata hivyo mpe pole nyingi,vijana wa cku hizi wanasema Shake Well before USE.:spy::spy::spy:
 

mbona kama una kauzoe ka sheria au una uzoefu na tatizo hilo kuwa wazi kidogo unaweza maliza tatizo hili jiachie zaidi
 

mkuu sio kila ******* ni punga huwa inatokea kwa baadhi ya wanaume tu. neno punga ni kali mno aisee
 
Kaunga ndoa hiyo imevunjwa rasmi na taratibu zote za kuivunja zimefuatwa na imetangazwa kanisani kuwa ile ndoa ilikuwa batili.

Katavi, kuna mambo mawili ambayo unachanganya: kuvunjwa kwa ndoa (dissolution of marriage) na ndoa kutangazwa batili (declaration of marriage nullity). Kuvunjwa kwa ndoa kunamaanisha kwamba ndoa hiyo ilikuwa ni valid, yaani haikuwa na kizuizi chochote siku ilipofungwa. ni ndoa halali kabisa. Lakini ndoa hii wakati mwingine yaweza kuvunjwa kama kuna sababu kubwa ya kiimani. Kwa mfano kama mwanaume na mwanamke walifungwa ndoa wakiwa wapagani (wafuasi wa dini za kienyeji, yaani hawakubatizwa) ndoa hiyo ya wapagani ni halali kabisa, yaani valid. Lakini inaweza kutokea kwamba mmoja wao baadae akaja kumpokea Yesu na kubatizwa. Mpaka hapo Kanisa halina shida, inaendelea kuitambua ndoa hiyo na inahimiza mbatizwa aendelee kuishi na mpagani. Shida inakuja pale mpagani kwa mfano anapoanza kumkataza mbatizwa asiende kusali, au anamlazimisha kuabudu miungu, kupiga ramli, nk mambo ambayo yanahatarisha imani ya mbatizwa. Hapo mbatizwa baada ya kulishirikisha Kanisa juu ya suala hilo linaweza kumkubalia mbatizwa kuvunja ndoa (dissolve) ndoa hiyo kwa ajili ya kulinda imani ya mbatizwa. Kuvunjwa huku kwa ndoa kunaitwa "Upendeleo wa Paulo" (1 Kor. 7:10-15). Hapo mbatizwa anaweza kuoa au kuolewa na mtu mwingine wa imani ya Kikristo.

Ndoa kutangazwa kuwa ni batili tazama #113. Hiyo inamaanisha kwamba ndoa siku inafungwa kulikuwa na kizuizi kwa hiyo kutokana na kizuizi (impediment) mf. impotency ndoa hiyo haikufungika japo ibada na mashamsham yalikuwepo na baadaye sherehe ya kukata na shoka. ndoa haikutokea, haikuwepo. Kinachofanyika hapo baada ya uchunguzi wa kutosha si kuvunja ndoa (kwani haiukuwepo) bali kutangaza rasmi kwamba ndoa hiyo ni batili, ni batili tangu siku ilipofungwa kwa sababu ya kizuizi.

wewe unasema ndoa hiyo ilivunjwa, hapana! Ilitangazwa kuwa ni batili. kwa macho ya wengi lakini na kwa lugha ya kawaida ya watu wanaweza kudhani ni kuvunja kwa ndoa. Lakini kisheria si kuvunja bali ni kutangaza ubatili wake. Yaani hao wawili licha ya kukaa pamoja kama mume na mke hawajawahi kuwa mume na mke kwa sababu ndoa haijawahi kuwepo kati yao.
 
Asante sana Babuyao kwa kuniongezea elimu katika hili kumbe ilibatilishwa na haikuvunjwa....!!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…