Kuna mume na mke. Walienda shambani na kuukuta uyoga mzuri ila hawakuwa na uhakika km uyoga ule haukuwa na sumu. Walikubaliana kumpa mbwa ilikujiridhisha. Walipofika nyumbani walipika na kisha kumpa mbwa. Siku hiyo mbwa hakupata madhara yoyote. Siku iliyofuata baada ya kuamka cha kwanza ni kumtazama mbwa. Mbwa alikuwa salama salimin! Wakajiridhisha kuwa uyoga hauna sumu. Wakaenda shamba na kuchuma uyoga wa kutosha. Waliporudi mke aliuandaa na familia yote ikala. Ilipofika saa 12 jioni mtoto aliingia kasi na kusema "baba mbwa amekufa,anatoa damu mdomoni" hapo wakajua kuwa kumbe uyoga unaua taratibu hivyo na wao kesho watakufa. No way out. Wakaanza kutubu dhambi zao. Mume akaanza " mke wangu kabla sijafa naomba unisamehe sana kwani nilikuwa natembea na mdogo wako na ile mimba aliyotoa ilikuwa yangu. Nisamehe mke wangu ili m/mungu nae akanisame" huku akiwa amepiga magoti. Mke nae " sawa nimekusamehe. Ila nawe naomba unisamehe kabla sijafa" mume "sema tu mke wangu ntakusamehe mbona we umenisamehe". Mke " Huyu mtoto wa mwisho sio wako, ni wa yule rafiki yako kipenzi(pia ni jirani yao) ni samee mme wangu". Mme akasikitika sn. Mara anaingia mtoto yule yule(wa mwisho) na kusema " baba yule mtu aliye mgonga mbwa kwa baskeli kasema atkuja kesho muonge. Ila mbwa amepona nilikua nacheza mae ss hiv kumbe alizmia tu" jamanh VIPI KUHUSU HII NDOA, ITAENDELEA? Vp km ww ni baba utafanyaje?