Ndoa hizi, mtihani!

Ndoa hizi, mtihani!

Mbu

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2007
Posts
12,752
Reaction score
7,861
MFANYABIASHARA Josephat Chengula (27), ameuawa kwa kupigwa risasi bega la kushoto baada ya kumfumania mke wake akiwa na mtu mwingine na kumtoza faini ya Sh 350,000 kitendo ambacho kimetafsiriwa kwamba hakikumfurahisha mtuhumiwa.

Akizungumza na Mwananchi jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda alisema tukio hilo, lilitokea juzi saa 4:00 usiku katika eneo la Madibila Mabada ambako marehemu aliuawa baada ya kupigwa risasi.

Ilidaiwa kuwa awali kabla ya tukio hilo, marehemu Josephat aliwahi kumfumania mmoja wa watumumiwa jina tumelihifadhi, wanaodaiwa kumpiga risasi akifanya mapenzi na mke wake.

Kamanda Kamuhanda alisema siku ya tukio, marehemu akiwa na mke wake, Jeni Mgeni (19) wakila chakula cha usiku jikoni alipigwa risasi kupitia dirisha lenye nyavu za chuma katika bega lake la kushoto na kuharibu moyo wake.

source;
Mfanyabiashara auawa baada ya kumfumania mke wake

...uzoefu unakuashiria jambo gani katika habari hii? Hii ni one sided story, hatujajua bado kilichompelekea mtuhumiwa kutenda kosa hilo, lakini kwa mwelekeo wa habari hii ni kama vile ilikuwa set-up. Au?
 
Back
Top Bottom