Ndoa imevunjika! Popote ulipo heaven on earth pata hii taarifa!

UNDENIABLE

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2013
Posts
2,326
Reaction score
1,314
Salaam!

Naandika kwa uchungu mkubwa sana, ila lazima niamue kweli yenyewe, decision must be made!

Kwanza natanguliza shukrani zangu zote kwake Heaven on earth kwa kunilea, kunipa hifadhi stahiki, kunijengeka na mengine mengi mazuri aliyoyafanya kwa ajili yangu, namshukuru sana Heaven on earth na nakupenda sana!

Maumivu ya kuachana na mpendwa wangu ni makubwa kiasi kwamba najiona kama ufahamu umenitoka vile! Nipo katika wakati mgumu sana, lakini ni muhimu kufanya maamuzi kwa ajili ya kujenga kesho bora! Naumia sana mwili na roho!

Ni jana tu nilikuwa nahangaika kumsaka mpendwa wangu wa moyoni Heaven on earth,niliweka rehani vitu vya thamani kubwa kwa ajili yake na hv leo ameibuka popote alipokuwa na kukiri kwa kinywa chake kuwa alikuwa amefichwa sehemu kwa ajili ya vunja jungu, na kwa kadhia hii nalazimika kumuweka huru maana nimeshindwa kuhimili mishemishe zake! Naomba pia kutumia nafasi hii kushukuru sana vyombo vyangu vya usalama wangu binafsi na washauri wangu wa masuala ya mahusiano kwa kunisaidia kupata taarifa zingine nyeti ambazo kwa heshima yake Heaven on earth nisingependa kuweka hadharani!

Popote uendako nakutakia kila lililo jema!

Nawashukuruni wote!

Wenu UNDENIABLE

Nakala hii imfikie shemeji yake mkubwa Himidini!
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaaaa majangaaaa majangaaa
....kiko wapiiiiiiiiii hahahaaaaa chezeya zongo weye
 
^^
Usipate tabu UNDENIABLE
Kwa uamuzi ulofanya,
Ikiwa ni kupendana,
Wapo waliopendana,
Kama watoto pacha,
Lakini sio ajabu pia,
Hata pacha hutokea,
Wakashindwa kuelewana,
..
Sina neno mimi
Nimejifunza nami
Penzi upepo Penzi,
Penzi sawa maua,
Huchanua na kunyauka,
Hata kama Heaven
Amekutenda kiasi hiki
Mie sitakutenga,
Nami urafiki nae umeisha,
Tuko pamoja UNDENIABLE
^^
 
Last edited by a moderator:

tanuru la busara! pamoja sana!
 

mwe mwe mweeeeeee!!
yamekua hayo,kulikoni shemeji?

Acha tu shemeji yangu, mm jana nahangaika kumtafuta huku na kule kumbe alikuwa anabinuka na kidume kingine yaani kafungiwa ndani eti! imeniuma sana! hv anataka apendweje sasa! ngoja kwanza nimwache shetani ampende vizuri!
 
Acha tu shemeji yangu, mm jana nahangaika kumtafuta huku na kule kumbe alikuwa anabinuka na kidume kingine yaani kafungiwa ndani eti! imeniuma sana! hv anataka apendweje sasa! ngoja kwanza nimwache shetani ampende vizuri!

jamani halafu kaniambia eti kaachiwa
coz ramadhani imeanza hahahaaa, Heaven on earth weweee!!
 
Last edited by a moderator:
Acha tu shemeji yangu, mm jana nahangaika kumtafuta huku na kule kumbe alikuwa anabinuka na kidume kingine yaani kafungiwa ndani eti! imeniuma sana! hv anataka apendweje sasa! ngoja kwanza nimwache shetani ampende vizuri!

uli niquote vibaya UNDENIABLE mpenzi
 
Last edited by a moderator:

jamani jamani mwambie UNDENIABLE niko hoi bin
taaban juu yake.........,
sa ye anapenda kuinterprate mambo kivingine!!!!
 
Last edited by a moderator:
jamani UNDENIABLE mi mwenzio bado nakuhitaji!!!!

^^
Shemeji roho imeuma
Nilikuonya mapema
Kinywa sawa jumba
Maneno yakitamkwa
Hayarudishwi mama
UNDENIABLE alikupenda,
Lakini si unajua tena
Mtu ukijua unapendwa
Kakangu amelia sana,
Namuombea mola,
Ayashinde mapito pia,
Wakale walisema,
Chozi la mwanaume,
Ni mkosi kwa mke,
Jihadhari usiwe ndege,
Arukae tawi hili na lile,
Yamenigusa sana ee,
^^
 
Last edited by a moderator:

kuachwa huku sijui nani atanitungia tena mashairi
matamu kama yako!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…