Ndoa inanishinda, naomba mnishauri kisheria

Bro pole.
Naomba nipate uhakika wa unachotaka.Ushauri au huruma yetu.Ukitaka ushauri tukupe kwa kuwa unaweza kuwa ni kinyume na utashi wako ukatuongeza ktk mgogoro
 
Mkuu hapa kama unataka kusaidiwa usifiche kitu eleza vzr watu wakusaidie
Kaka nipe muongozo wap nifafanue nipo tayar kuweka waz kila kitu,,mfano kutokana na haya madhila upendo wangu kwake umekwisha lakin nilikuwa navumilia sababu ya watoto hata sasa navumilia sababu ya watoto ni wadogo na mazingira ya kwao si mazur kwa watoto,,pili najua natambua kuwa lengo lao hata tukiachana kwa talaka wao hesabu zao ni fedha itayotolewa kwa ajili ya watoto, kutoa fedha kwa ajili ya matunzo ya watoto sio shida ila najua haitasaidia watoto zaid ya kujinufaisha wao ,,hapo ndio kichwa kinauma
 
Ushauri..
Weka kikao cha familia pande zote mbili muone mnatatuaje migogoro yenu na kama kuna uwezekano wa kusuluhisha..

Pakikosekana suluhu muache mkeo aende kwao, muache aende na watoto maana bado wadogo alafu utakuwa unawahudumia (kutoa matunzo)

Huyo mkeo anapewa kiburi na wazazi wake, ni ngumu sana kumrekebisha mwanamke wa hvyo maana anajua wazazi wake wapo watampokea na maisha yataenda.
 
Bro pole.
Naomba nipate uhakika wa unachotaka.Ushauri au huruma yetu.Ukitaka ushauri tukupe kwa kuwa unaweza kuwa ni kinyume na utashi wako ukatuongeza ktk mgogoro
Sio huruma kaka,,ni unishaur ni sheria gan au utaratibu gan ambao hata kama tutaachana Mahakaman either nibak na watoto kwa ustawi wa afya yao na maisha yao ila kama ikishindikana nipewe utaratibu wa kisheria utaonihakikishia usalama wa wanangu huko waendako! Nataman hata leo tuachane naumia watoto, cjui kama umenielewa
 
Asante kaka,,kama tutakaa kikao tena kitakuwa ni kikao cha tisa,kumuacha aende na watoto niko tayar tatizo ni mazingira ya hapo kwao! Watoto watateseka hawatahudumiwa ipasavyo,,najua hilo!! Hata hizo fedha pia ni kujinufaisha tu lakin hazitasaidia watoto!!
 
Mkuu pole sana ila inawezekana pia una tatizo mahali
 
Ni kweli mkuu wazazi wengi wa kichaga wanapenda kuingilia ndoa za watoto wao, na huwapa kiburi fulani wanawake walioolewa.
Wana hiyo tabia sana!! Kuna ndoa kadhaa nimeona jins walivyoshirikiana wakamfilisi mme kila kitu, hlf baada ya muda wanaleta wazo la kurudiana, ikashindikana. Wanachuma wanapeleka hela kwao!!
Na wanawake wa kichaga , % kubwa ni asili yao! Wanakua na tamaa na mali za mwanaume sana...ikitokea ugomvi kidg tu, kufilisiana kunaaanza.
Hawa wanawake wa kichaga ni kazi, wazazi wao wabadilike na wao binafsi wabadilike waache Utemi usio na maaana!!

Yan wao ndy wamkalie mwanaume kichwani, saa ingine na kwa mganga aende kwaajil ya kumfunga mme asielewe chcht kuhusu mali zake ili tu azishike yeye na awe na maamuz ya mwisho kuhusu kila kitu cha mme na familia ya upande wa mme, awasaidie au lah ila wazazi wake binafs mke watunzwe kila siku!!
 
Haya mambo huwa yananipa moto sana ikiwa mwanaume unashindwa kabisa kuamua mustakabali was ndoa yako.
Kwakifupi hapo haujaoa, bali we we ndie umeolewa.
Unaweza ukawa sahihi ndugu,,tatizo ni wazaz wanapoingilia!! Nnapotoa muongozo wangu wazaz wanaingilia kama hivi hali ambayo tunafikia hatua ya kutishiana maisha!! Lakin asante kwa ushaur wako
 
Ni kutokana na taarifa ambazo amekuwa akipewa na mtoto wao ambapo cjui anachombiwa ni nini!!
Baba mkwe/mama mkwe hana mamlaka ya kuingilia chochote kwenye familia yako. Na hata ikibidi kuja tu kwako lazima upewe taarifa na pia ujue anakuja kufanya nini.
Wewe hauja oa familia ya kwao na mkeo, bali wewe umeoa binti wa wakwe zako. Hivyo basi ukisha oa wewe hakuna yeyote mwenye mamlaka juu ya mkeo zaidi ya wewe.
Na hata baba mkwe wako akimuijia binti yake bila ridhaa yako, basi unaweza ukampa kichapo ama kumshtaki kama mvamizi
 
Mkuu haya mambo ya migogoro ya ndoa Ninayoyashuhudia kwa marafiki hayanipi hamu kabisa ya kuoa...but ikitokea nimeoa mke wangu akaniambia kauli Kama ulivoambiwa..." Mama yako ni mke mwenza wangu" sijui sijui kitakachotokea.............
Inategemea na tabia za huyo mama mkwe... Aeleze mama yake ana shida gani na mkwewe.... Wakwe wa sikuhizi we wasikie tu
 
Hizi ndoa zetu zinakwamishwa na mambo mengi.
Wewe umetufunga kiasi sijajua iwapo bado unamuhitaji mkeo na yeye anakuhitaji au tatizo ni wazazi ninyi bado mnakubaliana.
Lingine uwe mkweli,mpaka watu wazima wanafikia kukuomba kitu maana yake walizoea kupokea.Kama mwanzoni ulikuwa unawapa lkn sasa halo sio nzuri hilo litakuwa jambo LA kuzungumza na halitaleta shida.
Inawezekana pia una mchepuko ambao umestukiwa.Kama hili lipo mabadiliko huwa yapo na huonekana .
Kwa mtazamo wa kawaida ni kama umeshindwa kuhimiri majaribu ya ndoa hivyo inawezekana unatoa maneno yasiyofaa na ndiyo yanayoongeza shida.
Kama kuna jambo baya umefanya ni kuikimbia familia yako.Baba yupo sahihi kumchukua mwanae.Ungehama chumba na siyo nyumba.
 
Mzee Amini Usiamini kilichosababisha ukahatafisha ndoa ni mambo makuu Mawili,
1.Una Mahusiano mabaya na wakwe zako, huko kutowafanyia kitu watakacho pengine wakiamini kuwa unacho ndicho kilichopelekea kuwepo hapo ulipo leo, kwa maana sasa na wao wanakumomoa kupitia binti yao,

2.Akili mbovu za mke wako ambazo ameziacha wazi kutumika na wazazi wake, inavyoonekana wazazi wa binty wanainfluence kubwa kwenye maamuzi ya binty yao, mkeo hawezi kuamua lolote litokanalo na ndoa yake ispokuwa kwa ushauri wa wazazi wake,

Kimsingi Mzee umeoa mwanamke asiyekuwa huru na mwenye Akili tatu, Amini usiamini ndoa yako imeshikwa ukweni, leo binty akiambiwa na wazazi wake rudi kwa mumeo ukatulie basi utapata mke,

Ikiwa unaitaka ndoa yako na kama bado wampenda mke wako, basi rudi kwa wakwezo kawekane nao sawa uwe mtumwa wao, hapo utapata mke,

Kuendelea kujifanya kiburi hiyo NDOA utaiskia tu kwenye clouds TV,

Labda nikuulize wewe ni DINI GANI?
 
Siamini kama mpaka vikao nane vimekaa kutokana na maelezo yako huyo mwanamke bila sababu anakua mkaidi. Nahisi kuna upande wa pili wa stori ambao hujaweka wazi. La sivyo familia ya ulikooa ina shida
 
Duh hapa kweli Kuna shida
 
Unaweza ukawa sahihi ndugu,,tatizo ni wazaz wanapoingilia!! Nnapotoa muongozo wangu wazaz wanaingilia kama hivi hali ambayo tunafikia hatua ya kutishiana maisha!! Lakin asante kwa ushaur wako
Hakuna mzazi anae ruhusiwa kuingilia chochote ndani ya ndoa yako ikiwa hauja fanya jinai.
Na kwakukiri kwamba wazazi wanaingilia, basi ni wewe ndie umewapa nafasi ama mwanya wa wao kuingilia.
Kimsingi wakwe wanapokuja kwako wanapaswa wwe na adabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…