anasema hanipendi tena na amenizidi kipato hatuwezi kuishi kwa yeye kuleta mapato makubwa homeye katoa sababu gani za kutaka kuachana na wewe?
anasema hanipendi tena na amenizidi kipato hatuwezi kuishi kwa yeye kuleta mapato makubwa home
naomba nitambae na maeneo niliyoya-bold
1- hanipendi tena...kwanini?..umebadilika nini?
2- amenizidi kipato...wewe ulikuwa wapi akakuzidi kipato?..kipato chake kinatokana na ajira au mapato binafsi?..nini chanzo chake cha mapato binafsi?..nini chanzo cha mapato yake rasmi na ni kiasi gani?
3-kwa yeye kuleta mapato makubwa home...kwanini yeye alete mapato makubwa home?...mapato yako yanaenda wapi?..hujui jukumu la kulea na kulinda familia kwa mila za kiafrika ni la baba?...kwanini unaishi na mkeo kwa kipato kilicho-nje ya uwezo wako?
4- je ni mkeo wa ndoa na muna watoto?..wangapi?..ndoa ina umri gani?
nipe majibu ya maswali haya ili nikupe ushauri sahihi..maana hapa najaribu kusoma maisha yenu ya ndoa na nini hasa ni chanzo cha matatizo.
Kaka, mfano umeenda wamekupa kweli hayo mawasiliano (kitu ambacho sidhani kama wanaweza); halafu nini?
Ingekuwa wewe ndio unataka muachane na unatafuta ushahidi hapo sawa, lakini ni yeye ndio anataka muachane.
Mimi nakushauri, tulia kaa naye mzungumze ukiwa umetulia; washirikishe wazee wamshauri kuhusu watoto n.k. kama ni mke kweli atakusikia na mtasameheana; lakini kama ni kicheche, mwachie aende.
Mpaka idhini ya Police Mjomba.Labda mtu akufanyie kishkaji lkn akigundulika jamaa watafukuza kazi
yeye ameajiriwa na ana kipato cha kila mwezi mimi nimejiajiri na kipato sio kikubwa sana kama unavyojua bishara ndogondogo, naomba kujuzwa kama nikienda tigo watanipa mwenendo wa mawasiliano yao? Naomba nijuze hilo mkuu
tumeshakaa amekomaa kuachana, vipi kama nikienda na barua ya kutoka polisi watanipa?
Mkuu ushaidi muimu kuwa nao ata kama mtaendelea kuishi pamoja itakusaidia for further reference.
note: Naona mkae chini mzungumze labda munaweza kupa solution nzuri
ni kweli mkuu ila sasa namna ya kuupata ndio matatani
Sidhani kama watakupa kwasababu wewe sio mwenye simu, na wale wanawajibika kwa wateja wao tu. Halafu ukishajua itakusaidia nini, yeye keshaweka bayani kuwa hakutaki tena na ameshakupa sababu zake. Binafsi sioni sababu ya kung'ang'ania hiyo ndio ikiwa ameshakupa kinagaubaga.
Wewe bora utambae zako, fanya mikakati na jinsi ya kuwalea hao watoto.