Ndoa na Mirathi inawaumiza Wanawake

Ndoa na Mirathi inawaumiza Wanawake

Joined
Jul 11, 2020
Posts
66
Reaction score
145
Ipo hivi watu wakifunga ndoa hutangazwa kuwa ni Mwili mmoja, au kitu kimoja, kwa maana maamuzi sasa yanataka concer ya wote wawili.

Lakini mwanamke akifa kwenye ndoa, na mwanaume akiwa hai, hakutakuwa na ugomvi wa mali, kwa kuwa mali hazitakuwa na mpango wa kuganywa.

Lakini akifa mwanaume basi kila kitu kitagawanya hata kama mwanamke yuko hai

Hii inaonyesha kwamba wanandoa sio mwili mmoja ndo maana akifa mwanaume kuna kuwa na shida na sio mwanamke, au mwanamke sio sehemu kuu ya ndoa.

Hili ni kosa kubwa na huwa linawaumiza sana wanawake hasa walioshindwa kupata watoto katika ndoa zao.

Hapa natoa wito kwa ustawi wa jamii kuangalia swala hili ili iwe hata mirathi isiandikwe na mwanaume, bali iandikwe na wanandoa kwa umoja wao. Ili kutoa mamlaka kwa mtu mmoja huku mnasema kuwa wao ni kimoja.

Nawasilisha
 
kwani kwenye 'maandiko' ya Imani zetu ( ukristo +uislam) yanasemaje kuhusiana haya maswala ya mirathi?? na unadhani ni kwanini maandiko yana shauri hivyo??
 
Mother Confessor na mama D naamini muwanawake, lakini nashangaa hamuoni nilichoandika, mnasema ngoja muone

Does this mean kwamba mimi ndio naona shida kwa wanawake kuliko nyie au inawezekana ni fair kila siku wanawake kunyanyisika baada ya waume zao kufariki?
 
Umewasilisha vema Mkuu.
Ila mwanaume ni kichwa cha familia kwa hiyo akifa mwanamke bado mwenye jukumu la kulinda familia anabaki kuwa mwanaume na hii inamfanya kuendelea kubaki msimamizi na mlinzi wa familia.
Sidhani kama nimekuelewa vizuri.
Naomba kuwasilisha
 
Mwanaume akifa, hata kama ameacha watoto mama anakuwa hana mamlaka juu ya mali, na hata watoto hutaka kugawana

Lakini mama akifa, hakuna mtu atamghasi baba kwamba mali tugawane

Hapa ndipo kwenye uonevu, kwa kuwa huwafanya wanawake wawe hawana mamlaka juu ya mali wakati ndoa inatuaminisha wao (wanandoa) ni MWILI MMOJA
 
Mwanaume hutunza mali alizochuma na mkewe.......
mume akifa mwanamke fasta anapoteza mali kwa kugawa hasa akikutana na sticky penis...
 
Hakuna mwili mmoja kwenye ndoa.Kuna watu wawili katika mkataba wa kuwa pamoja ambapo mmoja ni mume na mwingine mke.Desturi jadi na makubalinao ndio yanaamua nani awe mrithi ili mrithi wa kwanza ni mjane.Kisha kama kuna watoto ndio wanafuata .Iwapo hakuna watoto basi mrithi ni mjane na wazazi.

Nafasi ya mwanamke inaelewa ila jukumu la mwanaume pia linaeleweka.Hizo sintofajmu ni kwa sababu ya tabia za mtu silka na uovu tu.
 
Haujawa specific kuwa mwili mmoja kwa mujibu wa dini gani ? Kwa mfano mimi satanist hayo mambo ya mwili mmoja na miradhi hatuyajui
 
Haujawa specific kuwa mwili mmoja kwa mujibu wa dini gani ? Kwa mfano mimi satanist hayo mambo ya mwili mmoja na miradhi hatuyajui
Satanists ni imani changa ambayo bado haijajipambanua kimahusiano

Antony LaVey alijikita zaidi kwenye mambo ya Imani na hakuenda kwenye culture kwa ujumla
 
Kimsingi mume akifariki mwanamke anatakiwa aendelee na maisha pale pale nyumbani kwao akitumia resources zao. Kwa hiyo kwenye hili mke hastahili kuitwa mrithi kwa maana mali ni za familia, mume, mke na watoto. Kama kuna mali ambayo mwanafamilia anahitaji kuimiliki binafsi, hii ndo mwanafamilia anatakiwa aitaje kama mali binafsi na inaweza kuingia kwenye mirathi. Wanasheria chukueni hii muijengee hoja kuwaokoa wanawake...
 
Haujawa specific kuwa mwili mmoja kwa mujibu wa dini gani ? Kwa mfano mimi satanist hayo mambo ya mwili mmoja na miradhi hatuyajui
Hapo sasa, kwa wale wanaume wenye mke zaidi ya mmoja huo mwili mmoja unajitengeneza vipi. Kwa hiyo wale wacha Mungu wa zamani na wafalme walivunja amri ya Mungu kwa makusudi maana kuna huyu Suleimani alikuwa na kijiji kizima cha wanawake.
 
Kimsingi mume akifariki mwanamke anatakiwa aendelee na maisha pale pale nyumbani kwao akitumia resources zao. Kwa hiyo kwenye hili mke hastahili kuitwa mrithi kwa maana mali ni za familia, mume, mke na watoto. Kama kuna mali ambayo mwanafamilia anahitaji kuimiliki binafsi, hii ndo mwanafamilia anatakiwa aitaje kama mali binafsi na inaweza kuingia kwenye mirathi. Wanasheria chukueni hii muijengee hoja kuwaokoa wanawake...
Point ya msingi ni kuwa mirathi igawiwe baada ya wanandoa wote kufa

akifa mwanaume akibaki mwanamke ataendelea kumiliki mali, akifa ndio mali wapewe watoto au warith wengine

Akifa mwanamke mwanaume ataendelea kumiliki hadi pale ambapo atafariki ndio mali wapewe watoto au warith wengine
 
Hapo sasa, kwa wale wanaume wenye mke zaidi ya mmoja huo mwili mmoja unajitengeneza vipi. Kwa hiyo wale wacha Mungu wa zamani na wafalme walivunja amri ya Mungu kwa makusudi maana kuna huyu Suleimani alikuwa na kijiji kizima cha wanawake.
logic
 
Nadhani umeandika mada yako kwa kutazama past experiences na historia ya matukio ya wajane kunyanyaswa.

But kwa hali ilivyosasa hizo situation ni very rare kutokea sababu ya elimu juu ya unyanyasaji wa ndugu za marehemu kwa watoto na mke wa marehemu.

Ila umeongelea upande m'moja, je umeshaona ndoa ya mwanamke mwenye pesa akifariki ndugu wa mke wanavyomjia juu mwanaume?!
 
Back
Top Bottom