Ndoa ndoano ndoa ni mpango wa mungu

Ndoa ndoano ndoa ni mpango wa mungu

muhandu

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2011
Posts
311
Reaction score
83
Salama wana MMU.Sorry kwa kuwachosha,

MKE AU MUME SIO BIDHAA UNAYO WEZA KUIPATA SUPERMARKET AU SOKO MJINGA,CHUKUA HATUA KAMA UNANIA NA SIMAMIA MISINGI YA MAISHA YAKO BADALA YA KUTANGULIZA MAPENZI KWANI HUWEKA UPOFU AMBAO BAADAE HUGHALIMU SANA.MENGINE NI MAJALIWA YA MWENYEZI MUNGU.
Kuna vitu ambavyo ningependa tushirikishane kwa upana na undani wake kwa faida ya wote,kwani ukifanikiwa wewe infanikiwa familia yako na hatimaye jamii nzima tunafanikiwa,basi fuatilia mtiririko huu ambao siyo rasmi kivile lakini nadhani unaweza kusaidia,panapo wezekana unaweza kurekebisha ili kuleta maana halisi ya kuelimishana.Kuana wengine ambao tayari ndani ya MMU wameshatoa njia na mawazo mbali mbali kwa nia ya kujenga.Fuata herufi hizi na malengo yake katika swala zima la kuoa au kuolewa ila kumbuka siku zote kutotanguliza mapenzi kabla ya misingi ya maisha uliyojiwekea;
A- stands for age-si rahisi kwa kijana wa kiume kumuoa mama wa umri mkubwa let say miaka kumi zaidi yake,na kwa mdada si rahisi kuolewa n kibabu lakini kwa ajili ya lift ya maisha mabinti wanaolewa ingawa huwa kwa kujishikisha tu,acceptance-kwao na kwenu,ability –zaidi ni kwenye thinking capacity yaani uwezo wa mtu kufikiria na kupambanua mambo kulingana na wakati pamoja na mzingira.
B- Stands for body structure,breachless (no mkorogo) inabidi kufahamu kuwa hakuna kitakacho baki kama kilivyo,na ndiyo maana kuna `earth erosion’(mmomonyoko wa udogo),kwa hiyo hata mwili hubadilika katika uhalisia wake.Unae mwona mnene leo ni mwembamba wa kesho,na mwenye afya njema leo ni mgonjwa wa kesho-na kinyume chake pia.Iweke akilini kuwa siku moja kama uliyenae ulimchagua kwa kigezo kikubwa cha umbile lake basi utafika wakati utamwacha uende kutafuta wale ambao unadhani ridhio la moyo wako.Na ndipo hapo utakuta unaenda kununua ile sukari kwa dada poa ili mradi tu yuko vile ambavyo wewe unafikiria kuwa ni presentable machoni mwake.Na kama alimwona sehemu bila kujali ni mali ya mtu basi itakuwa ndo nyumba ndogo. Wanao athirika sana na hili ni upande wa –ke sana kuliko upande wa-me.Hii imetokea sana katika jamii yetu na mifano mnayo,utakuta bosi Fulani kaamua kuwa na mke wa pembeni isivyo rasmi ili awe wa kutoka nae kwenda sehemu mbalimbali za starehe au kwenye -wenyewe hudai lazima awe na mtu presentable.Na Yule ambaye wameanza naye maisha anakuwa scrapper.Ndoa ni kifungo.,ndoa ni mkataba wa maisha.
C- Stands for care-ni ukweli kuwa wanaume ni big babies wanataka care lakini kwa kubalansi mizani ina apply kotekote,courageous,commandless,cactus (can live in either conditions) ni vema Mungu akakujalia ukapata mtu ambaye anaweza kuishi katika hali zote na si Yule wa wakati war aha tu,character,watu tumekulia mazingira tofauti na kukutana ukubwani wote tukiwa na meno 32 na kuamua kuwa pamoja.Si rahisi mkawa na tabia moja lakini inawezekana kabisa mkawa na kitu kinachoitwa `common interet’.Na kuna wakati mmoja anaamua kufuata mwenzake anataka nini hata kama yeye hapendi,mfano –ke wengi ni washabiki wa mpira kwa sababu tu mwenzake ni mpenzi wa mpira wa kutupwa,kuna wakati hufikia wakawa hawaelewani.Sasa Ili mambo yaende sawa amaamua nae kuupenda.Na hali hii imepelekea wengi kunywa pombe kwa kuwa mwenzake amemtaka anywe kwa kisingizio` onja siyo mbaya’mara nyingi huambiwa hivyo.Mbali na hiyo unaweza ukawa mkimya sana na mwenzako ni mwongeaji sana mpaka unaona kuwa ni kero kwako kwani hakupi ule muda ambao umezoea kuwa kimya na kutafakari kivyako.Kitabu kitakatifu (Biblia)kwa kutambua hili kinasema `ni afadhari ukaishi kwenye pembe ya dari kuliko kuishi na mwanamke mgomvi’.Na wengi hapa huwa wanaficha tabia zao za kweli na kujivika uhusika ambao sio wao na baaba ya miezi kadhaa ya ndoa ndo hujionyesha kuwa wao wakoje.Na hii inatokana na mtu kuoa au kuolewa ili apate LIFT YA MAISHA,anatamani kuoa au kuolewa na mtu ambaye tayari kwa juhudi zake amesha toboa kimaisha ili afike katika daraja ambalo anataka watu wamtambue ni nani. Ikitokea kile ambacho kimemfanya akubali kufunga pingu za maisha hakipo ni rahisi sana kuangalia upande mwingine kuna nini na atawezaje ku-maintain hali aliyo kuwa nayo.
D- Stands for disease,kuna magonjwa mbayo hurithiwa na hali fulani za kiafya mfano,kansa ya damu,matiti,kibofu cha mkojo,tb,cycle cell,magonjwa ya akili na hali ya ualibino.Kwa yale ambayo yanaonekana waziwazi huwa ni tatizo kwa wengi wao.Hapa hasa ni wanaume hukimbia wake zao kama atapata mtoto ambae ni mlemavu wa ngozi.Kuna kesi moja mama ana watoto kama watano ambao wote ni walemavu na BABA kaikimbia famila na kutokomea kusiko julikana.Pia kuna mchungaji alioa mpendwa mmoja kwa madai kuwa Mungu amemuotesha,wakapata mtoto wa kwanza akafariki,wa pili,watatu na wane.Wakapiga maombi kwa maelezo kuwa kuwa wanarogwa ndiyo maana watoto hawaishi.lakini ndani ya kanisa kuna mpendwa mmoja (ndiyo uzuri wa kuwa na wanadini walikwenda shule makanisani) akashauri waende wakapime ili kujuaa ni wanini watoto hawaishi.Kweli kwenda kule ikaonekana kila mtu ana cyclecell kali baba anayo na mama anayo-kwa hiyo mtoto mtarajiwa anakuwa `victim’ kiasi kwamba inakuwa ngumu ku-survive.Wataalamu wanajua zaidi.Ilibidi washauriwe waachane,kitu ambacho hakikuwa rahisi kama inavyoweza fikirika.Lakini hatimae walitengana na baba mchungaji akaoa mke mwingine na mama mchungaji nae akaolewa sehemu ingine na,Mungu bariki wote walipata watoto na wenza wao waliokuwa na wakati huo.HAPA TUNAJIFUNZA KITU KIMOJA KUWA USITANGULIZE MAPENZI KWANZA AU TAMAA YA KUWA NA MTU FULANI AMBAYE TU MACHO YAKO YA NYAMA YAMEMWONA KUWA NDO ANAFAA BILA KUTUMIA MACHO YA ROHONI(AMBAYO HUFANYA KAZI KWA KUMSHIRIKISHA MUUMBA WAKO KWA IMANI YAKO).BIBLIA AMBAYO HUWA NAISOMA MWENYEZI MUNGU ANASEMA KUWA`WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA.
E- Stands for endless love,education background,Vijana wengi wa DOT COM mmeenda shule na uwezo wa kufikiria ni mkubwa kulingana na ufahamu ambao umeupata.Na usasa ambao umechukuwa sehemu kubwa ya fikra zetu,katika hali ya kawaida mtu anakuwa ameshajiwekea malengo kuwa akitaka kuoa ni lazima awe na nyumba,gari na kazi nzuri.Aiishii hapo na atakae taka kuwa nae ni lazima awe mweupe,mrefu,ana kitambi,mwili wa mwanamichezo,English figure,nywele ndefu,midomo midogo nk.Mbaya zaidi hayo yoye ni wasifu wa mtu kwa nje.Yaani unampangia Mungu mtu unae mwitaji wakati unae tayari.Ni sawa na kupewa mtihani wewe unaamua kutunga la kwako na kujibu ipasavyo wewe mwenyewe.WEWE NECTA,WEWE BARAZA YAANI KILA KITU.Pamoja na hayo si rahisi kukuta binti wa digrii moja au zaidi kukubali kuolewa na mtu wa kawaida ambaye elimu yake haizidi darasa la saba.Kama itatokea ni kuwa huyu bwana ni mtu ambaye kwa njia zake mwenyewe ameweza kuwa na kipato na ametoboa kimaisha hivyo basi lile `gap’ la elimu hufukiwa na uwezo wa kifedha.Hali kadharika kwa wanaume pia huwezi kuta ameoa mwanamke mwenye elimu kubwa,ila kuna wachache ambao wamethubutu na wameweza kwa uweza wa Mungu kwani YEYE ANA STOO YA WATU NA UKIMWOMBA INVYO STAHILI ANAKUPATIA .
F- Stands for fairness,fascinate,family background,ni muhimu sana na ndiyo maana zamani enzi zile wazee ndiyo walikuwa wana watafutia wachumba vijana wao ndani ya ukoo.Hii iliwapa fursa kujua kwa undani ile familia ambayo inakusudiwa kutoa mtu ambaye anakwenda kushi na kijana wao.Kweli ni vema kufahamu kama ni wachapa kazi,je wachoyo,wanamagonjwa ya kurithi,wanadumu kwenye ndoa.Utakuta mtu bibi yake hakuwahi kuwa kwenye ndoa,mama mdogo,shangazi nk,na mama pia.Mara nyingi huwa hawana ushauri mzuri pale inapotokea KIBINADAMU mmesigana au kuanguka kwa namna moja ama nyingine,akienda kuomba ushauri kwao huambiwa `asikusumbue akili huyo mwanangu kwanza unauwezo wako unaweza hata kuishi mwenyewe mbona sisi tunaishi tu,ACHANA NAE HUYO’na kama binti ana akili za kupewa mara moja huona ni kweli na hapo ndo unakuwa mwisho wenu.Ila baada ya muda anajua kuwa alibugi step. Mwisho foolish in love-siyo mtu unakuwa kama vile uko na kaka au dada yako
G- Stands for GOD,ukimshirikisha wala hana longolongo,mitihani kwa mwanadamu ni ya kawaida.Anaweza kukupatia mtu na ukaona mbona kanipa balaa,hapana wakati mwiingine kubali kushughulikiwa na mambo madogo madogo,na kabla ya kufanya uamuzi kwa lolote linakukwaza kwa mwenza wako mwombe akuhalie maamuzi ya busara.Sikiliza kisa hiki.Kuna bwana mmoja alikuwa ni msomi wa mambo ya madini ndani ya mgodi wa Williamson,jiulize mwenyewe uko wapii,kwa kuwa alikuwa ni mtu mzima bila ya kuwa na mke basi ndugu na jamaa walimshikia kidedea na akaamua kuoa.Japokuwa alikuwa ni mtu mwa dini na maombi yote kwa Mungu,alikuja kupata dada mmoja ambaye alikuwa hajatulia.Kimaisha alikuwa na kila kitu ambacho mtu wa kiwango chake aliihitaji juwa nacho.Basi siku moja aliaga kama kawaida anakwenda dar kwenye semina ya madini na kwa kawaida kama anachukua siku mbili au tatu gari yake mark II ambayo huwa anaipaki palepale uwanjani na kwenda zake akirudi huichukua na maisha yakaenda kama kawaida.Kumbe siku hiyo bwana alichelewa kupata taarifa kuwa semina imesogezwa mbele kwa sababu ambazo ziko nje ya uwezo wa waandaaji,na kwa kuwa walitumia e-mail na yeye hakufungua account yake siko hiyo.Alivyoamka tu akajipanga safari uwanja wa ndege,akiwa njiani akapata simu kuwa semina itakuwa next week.Basi akaamua kwenda ofisini kufanya kazi zingine.Huku nyuma dada wa watu kumbe ana kibuzi chake disco joka mmoja,akawa amemwalika na kumweleza kuwa jamaa hayupo anawezakuja home mida ya jioni na kuvinjari nae.Na ikawa kama walivyo ahidiana masaa yakasonga mbele,mara giza hili.Mtaalamu wangu akaona muda wa kwenda home umefika akajikusanya na kuondoka kwenda home kama mida ya tatu usiku.Ile anakaribia getini hamwoni mlinzi.Kumbe kapewa ofa ya kurudi saa 6 usiku bila hata kuuliza sababu akatokomea anakojua yeye.Mbaya zaidi na geti liko nusu wazi.Jamaa akawa mpole na kkuamua kuacha gari nje akaamua kwenda kwa taadhari manake hajui ni nini kimetukia mpaka pawe vile.Kugusa mlango wa sebuleni uko wazi dining kumechafuka kama vile kulikuwa na sherehe Fulani hivi.Wakati anatafakari nini anakiona akasikia sauti ya mkewe ndani akilalamika kuwa inatosha,akasogea taratibu na kuugusa mlango wa chumbani ambao ulitoa ushirikiano tosha,ukafunguka.KWA MACHO YAKE MAWILI NYUMA YA VIOO VYA MIWANI ALIWAONA MTU NA MPENZI WAKE WAKIWA WAMEPIGWA BUTWAA WASIJUE CHA KUFANYA.Jamaa akachomoa bastola yake alipotaka kuwalenga akili ikamrudia akashusha mkono wenye bastola na kwenda kukaa sebuleni,akawaita na kumruhusu dj aondoke na awe na amani.UNAAMBIWA DJ ALIONDOKA NGUO MKONONI NA KWA KUWA ILI KUWA NI USIKU GIZA LILIMSITIRI.Kwa kitendo hicho dada hakukaahata siku mbili akatoroka na kwenda kwao, na jamaa alimfuata, bi dada alikaa kwa wasiwasi hali ambyo iliwanya wanandugu kutaka kujua kulikoni.Ikabidi aeleaze mkasa mzima,na hazikupita siku jamaa katinga kwao na binti na kumtaka warudi home.Mtaalamu wangu alilaumiwa sana kwa kitendo kile cha kutochukua hatua yoyote.Yeye aliuliza swali moja NI HATUA GANI NZURI KUCHUKUA HILI KUSUDI INIRIDHISHE KUWA HATA KUJA KURUDIA TENA KILE KITENDO?TUMEKUTANA UKUBWANI NA LABDA MUUNGU NDIYE KANIPA HUYU NA ILI AWE KATIKA MSTARI NI LAZIMA HILI LITOKEE NA HAWEZI RUDIA TENA MAANA KAADHIBIWA AKILINI NA SI MWILINI.Ndugu wakawa wapole na bi dada akaomba aandamane na shangazi zake na ndugu yake mmoja ili kuweza kuona kuwa hatakuja kudhurika kwani jamaa hazungumzii kabisa swala lile kitu ambacho kinamtia wonga hata wa kumsogelea.MPAKA SASA NI WATU WAZIMA NA MTAALAMU WANGU KASTAAFU ANAFANYA SHUGHULI ZAKE NA MAMA MSIMAMIZI BAADHI YA OFISI YAOFISI ZAO ZAKIUCHUMI.
Tuwe tayari kujifunza kwani elimu nyingine si rahisi kuipata darasani kwa maana ya shuleni au chuoni,na ndiyo maana utakuta mtu ni msomi mzuri tu wa digrii za heshima lakini kifalia yaani mke na watoto ni kizungumkuti.na mtu mwenye elimu ya kawaida na maisha ya kawaida anaishi kwa raha mustarehe na familia yake.
 
Back
Top Bottom