Ndoa ni taasisi muhimu sana katika jamii

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Kuna kisa nimekutana nacho, kisa hiki ni cha mwanaume aliyefanikiwa sana kimaisha. Kwa taaluma ni mhandisi anaefanya kazi na kampuni za kigeni. Mshahara wake kwa mwezi ni kama 12 million hivi bado allowance.

Huyu mwanaume alipokua O level tangu kidato cha pili alipata mpenzi, walipeana mimba na binti yule kuacha shule akiwa kidato cha tatu. Mwanaume aliendelea kidato cha nne, tano na sita. Alikwenda chuo na maisha mengine yaliendelea.

Baada ya binti kujifungua mtoto yule, hakua anatoka kwenye familia inayojiweza. Alizaa watoto wengine na kila mtoto alikua na baba yake. Wakati msomi wetu anakuja likizo nyumbani na kukuta hali ile, aliamua kumchukua mtoto wake na kumpeleka kwa wazazi wake. Anampa mama msaada lakini maisha ya yule binti yameshaharibika. Kuna madeni ya vikoba na pesa ya kula kila siku pamoja na watoto kama wanne hivi.

Yule kaka aligundua mama yake ni mlevi na anakwenda baa na mjukuu wake. Hivyo alipoanza kazi aliamua kumchukua mtoto wake. Aliweka dada wa kazi, alinunua na gari ya kumpeleka mtoto shule kila siku na kuajiri dereva.

Matatizo ni kuwa baba hana muda wa kukaa nyumbani. Pesa ipo, chakula kipo lakini mtoto amekosa malezi. Mwanzo wa kufahamu kisa hiki ni binti yule kufanikiwa kutoa mimba akiwa na miaka 15. Ni baada ya kuapata matatizo ya maumivu na damu kiende kwa kutoka kwa wingi ndipo rafiki zake walimsaidia kupata ushauri.

Unapopata kesi ya binti wa miaka 15 ni lazima upate picha halisi. Baada ya kumhoji sana binti alikiri kuwa mwanaume anaetembea nae ni rafiki wa baba yake ambae ana mke na watoto.

Hiki kisa kimenifakarisha sana. Kaka mhandisi hayuko tayari kuoa, kurudiana na mama wa huyu binti haiwezekani. Nimebaini kuwa taasisi ya ndoa iendelee kuheshimiwa.
 
Hivi kwa nini mtu unaoa au kuolewa?
 
Ndoa ndoano, Hii taasisi ishakufa kibudu tutafute taasisi nyingine badala yahii
 
kwanini asinge mhudumia mtoto na kumuacha akiendelea kukaa na mama yake!?
nimefukua ⚰️
 
nimeshuhudia mademu kibao ambao wanakaa na wazazi wao wawili waliofunga ndoa na wanaenda kanisani wanatoa mimba kila leo...ndoa haina uhusiano wowote na malezi ya mtoto ..mtoto anakua na tabia yake mmwenyewe kama group la damu
 
Hatari sana...

Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Eeeh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…