Ndoa niliyosimamia inanishinda: naomba msaada wa wana JF


Asante sana Mkuu Caroline D,

Kweli Condoms si njema, sipendi hata mimi. Naweza kutmia tu pale ambapo najua ni danger days (maana njia nyingine ya kutoa jamaa nje nayo ni ngumu kidogo).

Kuhusu mume, awali ilikua ni tatizo katika mapenzi maana kwa taarifa za uhakika hakuwa ni mtu wa wasichana sana wakati anasoma.
 
ndo maana inampain!lol
asipopata msaada wa haraka ataanza kutoka nje!by the time anarudi ndani atakuwa ameshaubeba anampa mkewe
 
What about clitoris? Hadn't she engaged in FGM during her childhood? Sorry if it's sounds too personal.

Asante mkuu kwa concern yako. Kuna jambo la ajabu lilitokea kwa huyu mke ambalo siyo la kawaida na liliwafanye waokoke (awali mke alikuwa ni Lutheran na mume ni Aglikan). Ni kwamba kabila la mke huwa hawakeketi kabisa ila kuna wakati clitoris ya mke ilikuwa inapungua size yenyewe na ikabidi waende kwa wazee waulize na mke akawa na hofu sana. Mwishowe wakaamua wakaokoka. Tangu waokoke hali ni ile ile na kwa sababu ya wokovu ule nahisi ndiyo maana ndoa inaendelea japo kwa tabu. Inakuwa tabu kwa kuwa mume kwa imani yake hawezi kugusa hawara kabisa, anategemea tu ndani mwake, na anapenda ajifurahishe angalao kila siku hata kama ni pigo moja. Tatizo pigo moja kwa mke ni basi hadi wiki igonge.
Wachungaji wao wameongea nao na kuhudhuria semina za ndoa hadi za Mwakasege lakini ni tatizo. Sasa labda wataalam mtusaidie, je clitoris inaweza kuanza ku-disapper slowly hadi itoweke ibaki kidogo tu????? Huu ni ushetani au ni mapepo gani?? Ushauri please!!
 
Huyu mke Pombe anatumia?
Mwambie ajaribu Bilauri ya Valuu moja tu pindi Mr. anapotaka.

Mkuu hawa hawatumii pombe kabisa kwa miaka kama 10 hivi. Waliamua kuokoka kutokana na tatizo hilo. Hapo juu nimefafanua tatizo mojawapo.
 


Mkuu NL,

Nashukuru mno kwa ushauri wako wa busara. Binafsi suala la condom ni second hand. Mke wangu ni sehemu yangu hivyo siwezi kumtenga na mwili wangu unless circumstances zinatulazimisha kufanya hivyo (safe vs danger days). Pia wao walitumia sana condom kwa kuwa wana umri wa kuzaa na mke anakuwa na hofu, na waliweza maana interval ya watoto yao ni nzuri sana. Nafikiri pia hawatumii siku zote condom.

Tatizo la kupenda kazi kama paka apendavyo maziwa liko kwa jamaa sana. Nilishamwita tukakaa several times kuwa hata kama ni the best performer kazini (of course he is na amepata promotion akiwa kijana kabisa) ni lazima atafute muda na mke wake hata wakatembee. Wamejaribu ila ninafikiri pengine nahitaji nisafiri nao niwafunze.

Kuhusu hali ya mke kabla ya ndoa sina shaka nayo. Jamaa alikuwa ni wale vijana ambao wanasoma tu hawajishughulishi sana na mademu alikuwa anasisitiza akiwa na wenzake kuwa criteria ya kumwoa mwanamke ni lazima awe virgin maana yeye alikuwa mwaminifu somehow na hawezi kuoa mwanamke ambaye amepitiwa na mwanamume mwingine. Niliwasimamia ndoa nikiwa na umri kiasi katika ndoa yangu (at least nilikuwa na uzoefu mkubwa) na kweli mkewe alikuwa virgin ( ya uhakika na si artificial- wazee hapa wanafanya mila zao). Kwa hali hiyo mke alikuwa mwoga sana na suala zima la tendo la ndoa, wakati ule nawasimamia kesho yake ni lazima unaenda kuwaona na mke alikuwa ni mwekundu analia sana na tulitumia muda wa ziada kumelimisha na alizoea, ila sasa sema uzoefu utakuwa ni kidogo na ni mtu yuko reserved na aibu aibu sana hivyo hata kujifunza kwa wenzake nafikiri ni tabu. Lakini tumewasaidia kikubwa sana, sema kuna tatizo nimeshalieleza hapo juu kuhusu clitoris na liliwafanya wakaokoka kabisa.

Wote tulisimamia ndoa na kuna wakati tulimchukua mke akalala kwetu tukaongea naye, hapishani sana na mume wake katika kuelezea. Yeye anaona hiyo ni udhaifu wake na pia aliamini kuwa pengine alitumiwa mapepo mahaba ili kuharibu critoris yake, unajua tena walokole kwa ,mistari yao na anaamini kabisa siku moja atarejeshewa. Ila inampa shida sana hii.
 
ndo maana inampain!lol
asipopata msaada wa haraka ataanza kutoka nje!by the time anarudi ndani atakuwa ameshaubeba anampa mkewe



Haswa, hilo ndilo balaa ambalo sitaki kabisa kuliwazia kwa wanandoa. Inauma na kuhuzunisha watoto tunaowaacha nyuma wakiteseka na kunyanyaswa na mali za urithi za wazazi wao.
 
Good day all,

Wakuu ninashukuru sana kwa ushauri wenu ambao kwa hakika ni uponyaji kwa ndoa zetu za sasa na zinazotarajiwa, za marafiki, ndugu na majirani zetu. Nitatumia busara zangu kuwafikishia wahusika. Nategemea pia wale ambao watapita hapa ndani ya thread na wana ushauri zaidi wanakaribishwa.
 
[/COLOR]


Haswa, hilo ndilo balaa ambalo sitaki kabisa kuliwazia kwa wanandoa. Inauma na kuhuzunisha watoto tunaowaacha nyuma wakiteseka na kunyanyaswa na mali za urithi za wazazi wao.

naam!
 
Mkuu hawa hawatumii pombe kabisa kwa miaka kama 10 hivi. Waliamua kuokoka kutokana na tatizo hilo. Hapo juu nimefafanua tatizo mojawapo.

Pombe saa nyingine ina busara zake. Ona wameacha na bado tatizo lina exist. Mi napiga ulabu na ndoa yangu iko imara kama jiwe la msingi!
 
hivi tendo la ndoa na ngono vinatofautiana vipi?

...kwa sie tuliooa, tendo la ndoa tumehalalishiwa. Ngono (uzinzi) tunakatazwa hata kukaribia...

Mkuu nimeanza kukupata hasa hapo ulipoanza kufanya comparative analysis ya mahuasiano na mapenzi enzi za zamani na kizazi hiki cha leo.

Lakini itabidi urudi tena Mkuu kama ulivyoahidi for more elaboration

...more elaboration itanibidi niwe muwazi na mkweli...

...sijui nitawakwaza teenegers hapa? anyway,
kwenye 'mazungumzo' baina ya miili ya wawili wapendanao kuna wakati mwenzio anaropokwa '...iiissshhh, enhee, hapo hapo', au anaweweseka na kupagawa 'unanigusa, unanigusa...!' na katika hayo.. Njemba's unaweza kuta jibaba zima linalia kama beberu, au wengine wanaropokwa kila aina ya viapo naahadi nyiiingi, kisa kanogewa!

Hiyo yote inatokana na utundu wa wapendanao hao kutumia miili vilivyo yao kupeana raha wakati wa tendo la ndoa. Panapokosekana 'utundu' huo, hata utamu wa tendo la ndoa hupungua au kutoweka kabisa, na ndio hapo mmoja wa wanandoa hao hujionea sex ni kama wajibu tu wa 'pakua ukimaliza funika' na wala sio starehe.
 
Mkuu Maane,

Baada ya kupitia ufafanuzi/majibu uliotoa hapa jamvini, nimegundua mambo machache ambayo wewe na mama watoto wako mnatakiwa kuyafanyia kazi ili kuinusuru hiyo ndoa.

Kwanza condom inaharibu zaidi kwa kuwa kama mwanamke hapendi tendo halafu ukaongezea na condom, ndiyo unaharibu zaidi. Waachane na condom na kwa kuwa inaonekana wanafanya tendo kwa nadra, basi walenge kwenye siku salama.

Pili, damage ilishafanyika tangu day 1, nahisi kijana wako alitumia nguvu sana na hakumuandaa msichana kwa kiasi kinachotakiwa na hilo lilipelekea mke kuchukia tendo la ndoa na ndio maana wewe unasema mlifanya kazi ya ziada kumshawishi kwamba ni kawaida. Kwa kuwa wote 2 walikuwa bikira, basi kilichofanyika ilikuwa ni "ubakaji" wa hiari na ukaishia kusababisha maumivu makali sana.

Tatu, umesema mume hakuwa mtu wa totoz, hiyo inaweza ikamfanya asiwe na exposure ya kutosha na inawezekana akawa ni mtu ambaye hawezi ku-discuss haya mambo na vijana wenzake. Same applies kwa mke kwa kuwa umesema mke ni mtu ambaye yuko reserved, hilo nalo ni tatizo kubwa sana. Hii combination inaweza kuwafanya wakawa hawawezi ku-discuss mambo ya tendo kwa undani zaidi. Msichana ataishia kusema hafurahii tena na mwanaume hajui kwanini mke hafurahii tendo.

Nne, kuhudhuria semina za ndoa sidhani kama zinasaidia sana inapofika wakati wa discussion ya tendo la ndoa. Organization ya hizo seminars ndio ambayo inazifanya zisiwe productive kwa kuwa zinajumuisha watu wa ages tofauti ili mradi ni wana ndoa, humo ndani utakuta watu wa umri wa miaka 20 mpaka miaka 50. Hao wana ndoa I guess wako around 40 - 45 yrs, so hata kuomba ufafanuzi ama kuuliza maswali inakuwa ngumu kwa sababu ya aibu ama kuogopa.

Nini cha kufanya?

Moja, wanahitaji kupewa semina na stranger ambaye hawafahamu kabisa lakini lazima awe ameokoka. Semina hiyo inatakiwa iwe ya kwao 2 tu, na iende kwa awamu, na ikiwezekana waende kuifanyia nje ya makazi yao ya kudumu. Semina iende kwa awamu kwa ajili ya kujaribu kufanyia kazi kila wanachoambiwa na mtoa semina na wanarudi kutoa feedback kwa ajili ya hatua nyingine. Mtoa semina anatakiwa awe age-mate wao ili wasiogope/wasione aibu kuuliza maswali ama kuomba ufafanuzi.

Mbili, wanunulieni vitabu na wavisome kwa kushirikiana ama kila mtu kwa wakati wake then wa-discuss kama wanaweza kujaribu kufanya yale ambayo wameyasoma kwenye kitabu. Kuna vitabu vingi sana vimeandikwa na watumishi wa Mungu, na tena vitabu vya Kenya viko more explicit mpaka hata styles zimewekwa kwa picha. Wataweza ku-improve hilo tendo na kulishwa neno la Mungu kwa kuwa kuna baadhi ya mambo yamekuwa discussed kwa kushusha mistari kutoka kwenye Biblia.

Swala la clitoris kupungua (ku-disappear) sidhani kama linahusiana na tatizo walilo nalo. Kiini cha tatizo kiko tangu siku ya kwanza kabisa na huyo dada hajaanza kutopenda tendo la ndoa baada ya clitoris kuanza kupotea. Kama nimekusoma vizuri, ndoa ni ya miaka 15, wameokoka like 10 yrs ago, may be 5 yrs baada ya kuoana. Lakini hali ya kutopenda tendo la ndoa ilikuwepo kipindi chote cha ndoa yao. So, damage was done from day 1, hiyo damage ndiyo inatakiwa kurekebishwa.
 

Mie nimefuatilia hii thread bila kuona tatizo liko wapi, lakini kumbe mwisho Maane umesema mwenyewe hiyo first day ndo imeharibu kutokana na mambo haya:
1. wote ni virgin na hivyo mama nadhani alilelewa katika mazingira ya kuiogopa sex, na alipopata taabu siku ya kwanza ndo amejua hiki sio kwa ajili ya kuenjoy tena bali for recreation sana kumridhisha baba basi.
2. hii ni psychological and not physiological wala sio issue ya ku disappear nini, hiyo pia ni muendelezo tu wa sababu za kuepuka hilo tendo ambalo ni adhabu kwake even though unconciously.
3. kutokana na ugeni wao na kuwa too reserved ndio maana 15 years later bado huyu baba sio mjuzi wa njia zipi, sehemu ipi, maneno gani au viungo gani vinamletea hamu mwanamke na akajaribu kuvitumia kwanza bila ya kulazimisha sex muda mrefu hadi mwenzie awe reassured kuwa sex is an enjoyable privilage in a marriage, hivyo huyu baba inabidi ajifunze kuwa mvumilivu na mwenye subira kwa huyo mke wake.
4. suluhisho litapatikana psychologically na kwa vile unasema wameokoka hivyo waambie wawe wazi kwa mtumishi watakaemuamini awape private lesson jinsi gani waanze from scratch, pili mama aombewe hiyo roho ya hofu ya hilo tendo imtoke na kama kweli anamajini mahaba (huwa wanaota wanafanya sex na watu usiowajua nakweli huwa hawapendi kabisa sex na wenzi wao) aombewe na naamini Mungu atawarudishia furaha katika ndoa yao.
5. Ni muhimu wapate semina na maombi jinsi ya kufanya hilo tendo maana madhehebu mengine huwa hayafundishi, matokeo ndo watu wanajifunza kabla ya ndoa. Kwa hiyo wanahitaji sana huyo mama aeleweshwe kuwa sex iliumbwa na Mungu kw ajili ya wanandoa and not a TABOO.
6. mama apunguze kazi na responsibility especially za hapo home, ili awe free na sio ktk tension muda wote, baba nae pia.
nadhani haya machache yatawasaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…