RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
MHADHARA (92)✍️
Ndoa nyingi za watanzania zimegeuka kuwa makampuni ya biashara. Siku hizi wasomi ni wengi lakini hawana ajira wala mitaji ya kuanzisha biashara, hivyo wamegeukia kutafuta mitaji kupitia ndoa. Hata ambao hawakubahatika kupata elimu pia wameshafahamu kuwa ndoa ni njia nyingine ya kuwatoa kimaisha.
Wengi wameamua kuingia, na wengine wapo mbioni kuingia kwenye ndoa za watu ambao hawana hisia nao na wala hawakuwapenda lakini ni kwasababu kuna pesa na mali. Tena wamekuja na msemo usemao; "bora wali nyama vitani". Wameona si mbaya kuvumilia kuishi miaka 3 - 10 kwenye ndoa kisha kuivunja ndoa.
Kama unafikiria kuoa/kuolewa ni jambo la kheri kwasababu zipo ndoa nyingi zimedumu na zinaendelea kudumu kwa amani, upendo, na maelewano. Muombe Mungu akupe ndoa ya aina hii.
Hata hivyo wakati unaendelea kufikiria kuoa/kuolewa huku ukiendelea kutafuta mpenzi wa maisha yako, tunakukumbusha kuwa kuna watu wapo tayari kujitosa kwenye igizo la ndoa hata kwa miaka 10 ilmradi kutafuta mtaji. Muombe Mungu usikutane na watu wa aina hiyo kwasababu utarudi hatua 10 nyuma za maisha.
RIGHT MARKER
Dar es salaam.