Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
NDOA SIO GEREZA. WANAOSEMA NDOA NI GEREZA NA NDOANO NI WAPOTOSHAJI WAKUBWA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Mapenzi na ndoa msingi wake Mkuu ni UPENDO na MFANANO.
Unapotafuta mwenza wako wa maisha huwezi uruka Wala kuupuuza MSINGI huo.
Mtu ambaye hufanani naye hawezi kuwa Mkeo au Mumeo.
Unaweza ukampenda mtu lakini mkawa hamfanani, na hiyo itawafanya msielewane.
Wanaosema ndoa NDOANO au ni GEREZA ni wale ambao hawakuzingatia Principle hi ya UPENDO na MFANANO.
Unampenda mtu Kisa akuhudumie utaacha kuwa katika GEREZA?
Mtu hamfanani alafu unataka muishi wote kweli?
Kijana, wazee wako wengi wanajuta kuingia ndoani kwa Sababu hiyo ya kuishi na Mke wasiyefanana.
Halikadhalika, Mama zako na shangazi zako wanaipatapata joto la Jiwe kwa kuendekeza kuhudumiwa kama kigezo cha kwanza kwenye Ndoa ilhali hawafanani na wanaume waliowaoa. Kinachotokea ni sio ndoa tena Bali hugeuka GEREZA.
Wewe unajijua ni mwanaume anayetumia pombe itakupasa utafute mwanamke anayefanana na wewe vivyohivyo ili usimtese mtoto wa watu.
Unajijua wewe ni mtu wa mfumo Dume alafu unatafuta wanawake Wasomi na wakisasa ni kama huna Akili sawasawa. Tafuta mwanamke wa JADI ambaye hajaenda shule. Huyo mtaendana.
Sio unakalia kusema Wanawake wa siku hizi au kusema Wanaume wa Siku hizi. Kumbe wewe ndiye mwenye matatizo.
Unaoa au Kuolewa na Sisi Watibeli alafu unataka ulipiwe Mahari, au uhudumiwe au usifanye Kazi. Hivi unaakili Sawasawa.
Unaoa single mother alafu hutaki watoto wake au awasiliane na mzazi Mwenzake hivi upo Akili yako inachaji KWELI!
Wewe kama hutaki watoto wa wanaume wenzako na hautaki mwanamke awasiliane na mzazi Mwenzake si ungeoa Mwanamke asiye na watoto. Lakini kwa vile huna akili na hujitambui unamuona mwenzako ndio anashida wakati mwenye shida ni wewe.
Umempata mwanamke wa watu anamaisha yake ya mitandaoni alafu wewe unaleta kisabengo chako hutaki ati apost hivi ulikosa unayefanana naye?
Kunguru kwa kunguru
Werevu kwa werevu
Washirikina kwa Washirikina
Wenye dini kwa wenye dini
Hivyo yaani.
Ndoa sio GEREZA Wala NDOANO ila watu wenyewe ndio tumeacha kufuata Kanuni za ASILI za mahusiano.
Ati tafuta pesa. Hivi aliyekuambia kuna uhusiano wa pesa na mapenzi au ndoa ni Nani huyo ukampige.

Sabato Njema
Robert Heriel
Taikon master
Kwa sasa Dar es salaam