Ndoa ya 3 ya Dida yavunjika..

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
KIMENUKA !

Siku chache kabla ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuanza, ndoa ya Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Radio Times FM , Khadija Shaibu ' Dida' na mumewe anayepiga mzigo TV1, Ezden Jumanne inadaiwa kuvunjika , ni Ijumaa Wikienda pekee lenye uthubutu wa kuiripoti.

Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Radio Times FM , Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kililinyaka tukio zima nyumbani kwa mtangazaji huyo Mwananyamala - Manjunju , Dar , ishu hiyo ilijiri wiki iliyopita usiku ambapo majirani walimsikia Dida akilia lakini wakashindwa kutoa msaada kutokana na geti kufungwa.

"Tuligonga sana mlango lakini hakuna chochote ila baada ya muda tulimuona mume wa Dida akitoka nje na begi kisha akaingia kwenye Bajaj na kuondoka , tukagundua walikuwa kwenye ugomvi, " kilisema chanzo hicho.

TATIZO NI NINI?

Chanzo kingine makini kimepenyeza madai kuwa ugomvi wa wawili hao uliibuka mara baada ya Ezden kuhoji juu ya mapato ya mkewe.

"Jamaa alikuwa anahoji mshahara na fedha ambazo mkewe anazipata katika shughuli za u-MC , alihoji pia kuhusu mwanaye kusoma Shule ya Saint Kayumba ( hali ya chini ) ndipo mtiti ulipoanzia, " kilisema chanzo hicho. Bw. Ezden Jumanne akipozi .

EZDEN AENDEWA HEWANI

Baada ya kunyetishiwa ishu nzima, mwanahabari wetu, alimtafuta Ezden kwa njia ya simu na kumsomea madai hayo ambapo hakuwa tayari kufafanua zaidi , alijibu kwa kifupi: "Elewa tu kwamba tupo kwenye matatizo na mke wangu ila kwa sasa siko tayari kulizungumzia."

DIDA ANASEMAJE?


Kama ilivyo ada ili kupata uzani wa habari, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Dida, alipopatikana, alifunguka : "Mimi na mume wangu huwa hatuna mipaka katika simu zetu, kila mtu yuko huru kuchezea simu ya mwenziye. Siku ya tukio jamaa ( Ezden ) kabla hajaenda kuoga alitengeneza namba za siri ( pasword ) sasa nilivyotaka kucheza gemu nikamfuata bafuni na kumuuliza mbona simu imefungwa , nikamuomba anifungulie , huwezi amini akaanza kunitukana , nikajiuliza ni simu tu au kuna mengine!" Khadija Shaibu ' Dida' .

KIPIGO KINAENDELEA

Akiendelea kusimulia , Dida alisema ghafla , Ezden alichukua mkanda na kuanza kumpiga . "Nilishangaa sana, nikajiuliza kosa langu ni nini? Alinipiga hadi akanipasua sehemu ya kichwa, sikuamini kama Ezden anaweza kunifanya vile au kama alinichoka angeniambia wakati yeye ndiye mkosaji , " alisema Dida.

EZDEN ATIMKA

Chanzo kilidai kuwa , baada ya Ezden kuona amemuumiza mkewe, alikusanya nguo zake na kukimbia kwa usafiri wa Bajaj kwani Dida alificha funguo zote za magari yake . "Alijua Dida atakwenda polisi hivyo akaona bora atimke zake , " kilisema chanzo. Khadija Shaibu ‘Dida ' na mume wake, Ezden Jumanne wakiwa nyumbani.

DIDA ATAKA TALAKA


Katika kuonyesha kuwa amechukizwa na tukio hilo la kupigwa ambalo amedai limekuwa likitokea mara kwa mara pamoja na kukosa imani naye katika masuala ya kuchepuka , Dida amesema kwa kuwa alishindwa kumuomba msamaha siku ileile ya tukio, anachotaka kutoka kwake ni talaka tu .

TUJIKUMBUSHE


Tukio la kuvunjika kwa ndoa hiyo iliyofungwa mwaka jana ( siku tano kabla ya Mwezi wa Ramadhani kuanza) likikamilika kwa talaka , Dida atakuwa ametimiza idadi ya ndoa tatu kuvunjika. Awali aliolewa na Mohamed Mchopanga ' Mchops' kisha Gervas Mbwiga ' G ' na wote walimmwaga kwa talaka .
 
Sasa zamu yangu ya kumuoa Inshaallah.

duniani hakuna perfect tujiulize ina maana dida ye wakuonewq daily...?mi nahisi ye ndo shida maana ndoa zote hakai ht miaka mitatu!kweli jamani wanaume wote hao ndo tatizo hapana dida anapaswa kujitathmini upya kabla ya kuingia kwenye ndoa tena...!
 
Huyo alipata gundu baada kumsaliti mchops na kutembea na HANDSOME,BABA YA MUZIKI,BABY D ANTA...DULLY SYKES..
 
Jaman, na uzee wote huo anataka kucheza Game kwenye Simu!? Na watoto nao watacheza nn!? Wakati kuna Laptops & Ipad Air!? Au alikuwa na lake Jambo!? Ndio maana Jamaa akaamua ampasue. Mm nnaoga halafu unanambia eti unataka(Nkutolee Lock) ucheze Game kwenye Simu yangu!? Na kama ni mpenzi wa kucheza Game kwenye simu,kwa nn usinunue Simu yako kwa ajili ya shughuli zako hizo za kuchezea Game!?

Wanawake walio wengi wanaulimbukeni wa kukagua simu za waume zao pindi wanapoenda Kuoga. Utadhani wamelogwa,hadi wasubirie hadi MR. Kaenda kuoga ndio waanze mambo yao ya kufokonyoa simu za Waume zao.

Na iwe fundisho kwa Wanawake wengine wenye Miji-tabia kama hii(Inakera Atiiii) Mm nmetoka zangu kazini badala uniulize Honey habari za Kazi/Uchovu, Unataka kunipokea Simu kwa kisingizio cha kutaka kucheza Game. Asishangae kupokea kipigo toka kwa Hubby wake, kwani hakuna mwanaume angeweza kuivumilia hii tabia. Ni mkong'oto tu kwa kwenda Mbele.
 

Mjinga sana yule..
Katoa sababu ya kitoyo,eti acheze game.!!!!
 
Ila Edzen anaendana na Jokate ! Nasema tu kwa Mfano .....Anyway Another Ndoa Ndoano za Bongo acha Nikalime miye ...
 
duniani hakuna perfect tujiulize ina maana dida ye wakuonewq daily...?mi nahisi ye ndo shida maana ndoa zote hakai ht miaka mitatu!kweli jamani wanaume wote hao ndo tatizo hapana dida anapaswa kujitathmini upya kabla ya kuingia kwenye ndoa tena...!

kama unasikilizaga kile kipindi chake cha taarabu basi ndio maneno yake akiwa chumbani haswa kwenye 6 kwa 6 ana mauzi flani hivi ya ndani kwa ndani anapenda kukusema vibaya hata kwa jambo dogo nilitembea nae siku moja but sikuinjoy kabisa nilikereka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…