Ndoa ya Miaka 30 Kuishia Talaka: Makosa Mapya au Uvumilivu Uliofika Mwisho?

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
22,235
Reaction score
51,111
Familia

Hivi nini hupelekea watu waliokaa kwenye ndoa miaka 20+ au 30+ kuachana?

Huwa ni tabia za zamani ambazo mmoja wao alikuwa akijipa moyo na muda na kuvumilia akidhani tabia itarekebika?

Nina mfano hai wa mama wa familia fulani

Mume amempa talaka mke wake ambaye wameishi pamoja kwa zaidi ya miaka 30

Huyo mzee alikuwa akipelekewa kesi za ndoa za wanafamilia, na alikuwa anakemea sana suala la kuachana

Kuna binti yake aliomba talaka kwa mume wake, huyo mzee akawa mkali kama pilipili

Hakutaka kusikia habari za binti yake kuomba talaka

Binti akalazimishwa kuvumilia, mzee hakutaka kusikia binti anadai talaka
Kwa kulazimisha binti akaondoka kwa mume wake

Mzee akawa mbogo mpaka baadae sana akakubaliana na hali

Sasa leo yeye ndiye ametoa talaka🙌🏼

Nilivyosikia nilishtuka kidogo kwa kuangalia muda ambao ndoa yao imedumu, ila sikuona ajabu sana kwa sababu mimi ni muumini wa amani

Kama hakuna utulivu, amani mchana kweupe naunga mkono anayeamua kukusanya virago

Kilichonifanya niandike ni kwamba nimejiuliza hivi watu wazima wanapokuja kuachana uzeeni, huwa ni makosa mapya au ni makosa ya zamani ambayo mtu alijipa moyo kuvumilia akidhani mwenza atabadilika?

Sioni mantiki ya kuachana uzeeni wakati tayari mmeshaanza kuzeeka na mna wajukuu
Au ndiyo kumaliza uzee salama?

Mie naona watu wakishindwana mapema tu waachane, kila mtu akatafute changamoto mpya

Weekend ya familia na ShesRise_1 ✋️ Upo wapi leo nyumbani na familia au ume chill sehemu 😊
 
Kama mtu anataka kukuua abaki na Mali na unajua kwanini ndoa isivunjike.
 
Peace of mind, dunia imebadilika, zamani kungekuwa na uwazi kama wa sasa, divorce zingekuwa nyingi za kutosha ila walivumilia kuepuka aibu ya jamii itakuonaje umeachika, hiyo haipo tena miaka hii.
 
Familia

Hivi nini hupelekea watu waliokaa kwenye ndoa miaka 20+ au 30+ kuachana?

Huwa ni tabia za zamani ambazo mmoja wao alikuwa akijipa moyo na muda na kuvumilia akidhani tabia itarekebika?

Nina mfano hai wa mama wa familia fulani

Mume amempa talaka mke wake ambaye wameishi pamoja kwa zaidi ya miaka 30

Huyo mzee alikuwa akipelekewa kesi za ndoa za wanafamilia, na alikuwa anakemea sana suala la kuachana

Kuna binti yake aliomba talaka kwa mume wake, huyo mzee akawa mkali kama pilipili

Hakutaka kusikia habari za binti yake kuomba talaka

Binti akalazimishwa kuvumilia, mzee hakutaka kusikia binti anadai talaka
Kwa kulazimisha binti akaondoka kwa mume wake

Mzee akawa mbogo mpaka baadae sana akakubaliana na hali

Sasa leo yeye ndiye ametoa talaka🙌🏼

Nilivyosikia nilishtuka kidogo kwa kuangalia muda ambao ndoa yao imedumu, ila sikuona ajabu sana kwa sababu mimi ni muumini wa amani

Kama hakuna utulivu, amani mchana kweupe naunga mkono anayeamua kukusanya virago

Kilichonifanya niandike ni kwamba nimejiuliza hivi watu wazima wanapokuja kuachana uzeeni, huwa ni makosa mapya au ni makosa ya zamani ambayo mtu alijipa moyo kuvumilia akidhani mwenza atabadilika?

Sioni mantiki ya kuachana uzeeni wakati tayari mmeshaanza kuzeeka na mna wajukuu
Au ndiyo kumaliza uzee salama?

Mie naona watu wakishindwana mapema tu waachane, kila mtu akatafute changamoto mpya

Weekend ya familia na ShesRise_1 ✋️ Upo wapi leo nyumbani na familia au ume chill sehemu 😊
Kuna swali moja mnauliza Sana!
"UKIFA UTATUACHAJE"?
Bora tuachane tuu maana nikiumwa kidogo, unapiga maombi mazito ya kutaka kubadili hati za Mali.
 
Back
Top Bottom