najisikia kumchoka mwenzangu bila sbbu yuko sawa kila k2 ila sina ham naye tena kama zamani tulipokuwa wachumba najitahidi nashindwa sina nyumba ndogo ila natamani wakti mwingine ila cjawahi fanya ila mwenzangu wa ndoa nimechoka kabisa hajanikosea haja badilika ila nahisi kumchoka nisaidieni nifanyeje jamani?
Mkuu,
Tatizo lako si la mmoja. Yawezekana wanaoandika hapa wanaandika bila kujua umeathirika vipi kisaikolojia.
Mimi ni mtu mwenye ndoa na ningependa nikushauri kwa ninavyoona inafaa (kama ninavyoiishi ndoa yangu).
Mosi; popote penye tatizo pana chanzo. Hujatufahamisha chanzo cha wewe kumchoka ni kipi, unakijua lakini inaelekea imekuwa ngumu kukiweka bayana, ingekuwa rahisi kwetu kuweza kukushauri kulingana na chanzo cha tatizo.
Pili; kuchokana kwenye ndoa kunatokana na mambo mengi, yawezekana mwenzi wako amebeba ujauzito au kajifungua hivyo yuko kwenye kipindi kigumu kimatamanio, hapa unatakiwa kumvumilia, ni kipindi cha mpito. Yawezekana unamhisi mwenzio kuwa na mahusiano na mtu/watu kitu ambacho ni obvious mapenzi kwako pia yatashuka. Yawezekana pia wewe binafsi umeruhusu mambo ambayo unajua wazi kuwa yatapunguza mapenzi yenu. Ukifanya kazi muda mrefu bila kupumzika ni wazi hata mwili unachoka na unajikuta una muda mdogo sana wa kuwa na mwenzi wako, unaanza kupoteza hamu nae.
Tatu; kama mmefunga ndoa kihalali; kumbuka ahadi zenu za ndoa, ulisema utampenda katika shida na raha, huu ndio wakati wa shida, unatakiwa kuitekeleza ahadi yako sasa! Lakini pia, hata kama hamjafunga ndoa kihalali ila mnaishi kama mme na mke; lazima kuna kitu kiliwafanya mkafikia maamuzi haya, hamkulazimishwa na mtu. Uliona katika viumbe wote huyo ndiye anafaa kuwa mwandani wako; kabla hata ya kutueleza ulitakiwa kuwa umeyaongea na mwenzi wako na kutafuta suluhu ya matatizo yenu.
Mkuu; ndoa ni tamu sana, ina raha mno! Inahitaji kuelewa kuwa mapenzi huchochewa ili yaendelee kukua na kuchanua, wewe ndiye unatakiwa sasa baada ya kubaini kuwa umepungukiwa mapenzi kujifunza ni kipi kizuri kwa mwenzi wako na kuhakikisha unakuwa unakiona kila wakati. Sitaki kuamini ulimpenda sababu ya sura au maumbile tu; kuna mvuto flani ulikupeleka kwake. Pata muda, mwende nje ya maeneo yenu mnapoishi (outing) mkakae na kujaribu kula vilivyopikwa na wengine huku mkifurahia pamoja; jaribu kuilazimisha furaha ikibidi lakini hatma yake utagundua tofauti.
Yawezekana pia chanzo ni kubadilika tabia kwa mwenzi wako na unamfichia siri; hapo ndipo pia unatakiwa kumweleza katika faragha juu ya tatizo lake. Usimweleze kwa kumgombeza au kwa sauti kubwa; kuwa na hekima, mwambie polepole huku ukimweleza unampenda kiasi gani na mabadiliko unayoyaona yanavyokuathiri sana mpaka kupoteza hamu yako kimapenzi kwake.
Mkuu, naweza kuandika mengi lakini bila kujua chanzo inakuwa ni kumpigia mbuzi gitaa, hebu kuwa wazi kidogo tuinusuru ndoa yako, ni ya thamani kwako na thamani kwetu pia kwani mkiparana, wanaoumia ni watoto ambao huenda wakahangaika mitaani na watakaokutana nao ni sisi (Jamii).
Ahsante