Ndoa za Kulazimishwa Zinawanyima Watu Uhuru na Kuathiri Ushiriki Wao Kamili Katika Jamii

Ndoa za Kulazimishwa Zinawanyima Watu Uhuru na Kuathiri Ushiriki Wao Kamili Katika Jamii

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
NDOA ZA KULAZIMISHWA (4).jpg


Ndoa ya kulazimishwa ni hali ambapo mtu amelazimishwa kuoa au kuolewa bila hiari yake. Ndoa ya kulazimishwa inaweza kutokea kwa shinikizo la kihisia, kifedha, kwa matumizi ya nguvu au vitisho, kwa kurubuniwa na wanafamilia, mwenzi, au wengine.

Ndoa hizi zimepigwa marufuku na mikataba kadhaa ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na ile inayokataza utumwa na vitendo vinavyofanana na utumwa, ikiwa ni pamoja na ndoa za kutumikisha.

Idadi ya wanaume, wanawake na watoto wanaoishi katika ndoa za kulazimishwa imeongezeka duniani kote.

Tatizo la ndoa za kulazimishwa limeendelea kuongezeka kutokana na majanga yanayoendelea kuikumba dunia kama vile COVID-19 na migogoro inayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Changamoto hizi pia zimesababisha ongezeko la umaskini uliokithiri, viwango vya chini vya elimu, ongezeko la uhamiaji wa kutafuta fursa za kuondokana na dhiki, na ongezeko kubwa la unyanyasaji wa kijinsia.

Katika baadhi ya nchi zilizokumbwa na vita, wanawake na wasichana hutekwa nyara na kusafirishwa na makundi yenye silaha na kulazimishwa kuolewa na wapiganaji, wakivumilia kila aina ya dhuluma za kingono, kimwili, na kihisia.

Katika nyakati za migogoro na baada ya migogoro, ndoa za kulazimishwa pia hutumiwa kama njia ya ku-survive. Familia zinazokimbia migogoro ambazo zinakabiliwa na ukosefu wa usalama na hali ngumu ya kiuchumi zinaweza kuona ndoa kama njia ya kupunguza umaskini na “kuwaepusha” wasichana au wanawake na hali ngumu ya maisha.

Vilevile, wasichana na wanawake wanaweza kuangukia kwenye mawindo ya walanguzi wanaodai kuwatafutia mahali salama pa kuishi na nafasi za kazi.

Kichochezi kingine kikubwa cha ndoa za kulazimishwa ni mfumo dume na mifumo ya kijamii inayoendesha (control) maisha wasichana na wanawake. Hii ni pamoja na mitazamo kwamba masuala ya mahusiano na kimapenzi yanaleta picha mbaya kwa msichana/mwanamke na kwa familia yake na kwa hivyo wazazi wake wana jukumu la “kumlinda”, hata kama ana uwezo wa kufanya maamuzi yake mwenyewe.

Ndoa za Lazima (bila JF).jpg

Pia kuna dhana kwamba msichana/mwanamke anapaswa kuzingatia maagizo ya wazazi na ndugu au viongozi wa dini na kijamii juu ya nani wa kuolewa naye. Hata hivyo, msingi wa hili ni dhana potofu kwamba wasichana wote wanataka kuolewa, na kwamba ndoa na uzazi ni chaguo pekee la maisha ya msichana/mwanamke.

Kwa mujibu wa ripoti ya Makadirio ya Utumwa wa Kisasa Duniani mwaka 2022, karibu robo ya wanawake wote waliolazimishwa kuolewa, waliolewa kabla ya umri wa miaka 16.

Ripoti hiyo inaonesha kuwa 24.3% ya wanawake wote milioni 15 waliolazimishwa kuingia kwenye ndoa duniani walikuwa na miaka 15 kurudi chini; 27.3% wakiwa na miaka 16 na 17, huku 35.9% wakiwa na umri wa kati ya miaka 18 na 24; lakini pia 11.2% wakiwa na umri wa miaka 25 hadi 34; na 1.0% wakiwa katika umri wa miaka 35 hadi 44.

Mara baada ya kulazimishwa kuingia kwenye ndoa, hata hivyo, waathiriwa wanakuwa katika hatari ya kukumbana na madhila zaidi, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kingono, utumikishwaji wa nyumbani na kufanyiwa vurugu, na aina nyinginezo kazi za kulazimishwa ndani na nje ya nyumba.

Ndoa hizi ni ukiukaji wa haki za binadamu na ni mila yenye madhara ambayo inawaathiri wanawake na wasichana kwa namna tofauti, na kuwazuia kuishi maisha yao kwa uhuru na amani na kuzuia ushiriki wao kamili katika uchumi, siasa na nyanja za kijamii.
 
Back
Top Bottom