Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Hali ya Ndoa za utotoni Barani Afrika kwa ujumla
Kulingana na Taasisi ya Takwimu ya UNESCO, kuna watoto milioni 32 ambao hawajaenda shule wa umri wa msingi barani Afrika na vijana milioni 28 wasioenda shule - viwango vya juu zaidi ulimwenguni.
Inaelezwa kuwa katika Bara la Afrika, wasichana wanaoishi katika mazingira yenye vita na migogoro wapo katika hatari za mara 2.5 zaidi kutokwenda shule na kujiweka katika nafasi kubwa kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia na kuingia katika ndoa za utotoni.
Chanzo cha Ramani: Plan International Help End Child Marriage
Maelezo ya Picha: Ramani inaonesha baadhi ya mataifa ya Afrika yenye kiwango cha juu cha ndoa za utotoni
Barani Afrika, nchi 20 zinazoongoza kwa kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni ni pamoja na Chad (67%), CAR (68%), Sudan Kusini (52%), Mali (52%), Niger (76%) na Mauritania (37%).
Hali ilivyo katika nchi za Afrika Magharibi na Afrika ya kati
Shirika la watoto Duniani (UNICEF), linaeleza kuwa katika wasichana 10 wa nchi za Afrika Magharibi na Kati 4 kati yao waliolewa kabla ya kufikisha miaka 18 ambayo ni sawa na 41% ya idadi ya watu milioni 60. Hali hii inafanya eneo hili kuwa na idadi kubwa zaidi ya ndoa za utotoni ulimwenguni. Mnamo mwaka February 24, 2020 Techloy walitoa chati inayoonesha idadi ya ndoa za utotoni katika nchi hizo kama ifuatavyo:
Chanzo cha picha ni UNICEF na Techloy
Picha 1: Chati inaonesha hali ya ndoa za utotoni katika nchi za Afrika Magharibi na Afrika ya kati.
Kwa mujibu wa data na chati iliyotolewa na Unicef na Techloy hapo juu inabainisha kuwa Nchi ya Niger, ina wasichana wapatao milioni 4.1 sawa na 76% walioolewa kabla ya kufikisha miaka 18 ikiwa inaongoza katika ukanda huo huku ikifuatiwa na Jamhuri ya Afrika ya Kati (800,000) sawa na 68% huku nchi ya Chad ina idadi ya (milioni 2.6) sawa na 67%.
Nchi yenye watu wengi zaidi katika ukanda huo, Nigeria, yenye watoto wanaokadiriwa kufikia milioni 22, ina idadi kubwa zaidi ya watoto wa kuolewa, ambayo ni asilimia 40 ya watoto wote wanaoolewa katika eneo hilo. Katika infographic hii ya Techloy, tunaangazia kuenea kwa ndoa za utotoni katika Afrika Magharibi na Kati, ambapo jumla ya wasichana na wanawake walioolewa wakiwa utotoni ni milioni 59, kulingana na data kutoka UNICEF, kufikia Januari 2018).
Hali ilivyo katika nchi za Afrika Mashariki
UNICEF wanaweka bayana kuwa katika nchi za Afrika Mashariki na Kusini, asilimia 31 ya wasichana huolewa kabla ya kufikisha miaka 18, jambo linaloashiria ukiukwaji wa haki za binadamu wa wasichana.
Kwa mujibu ya Girls Not Brides Youth in Action: Leading the movement to end child marriage in East Africa wanaeleza kuwa katika nchi za Afrika Mashariki, mabadiliko na mafanikio ya kukomesha ndoa za utotoni yanakuja taratibu taratibu. Wanaeleza kuwa Kwa miongo kadhaa, harakati za kukomesha ndoa za utotoni zimekuwa zikikua hatua kwa hatua, na zimeleta mafanikio makubwa katika eneo Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kupungua kwa mila hiyo katika nchi kadhaa. Lakini kasi ya maendeleo na mabadiliko bado hairidhishi.
Inaelezwa kuwa katika nchini za Kenya, Tanzania na Uganda, idadi kubwa ya wasichana bado wanaolewa kila mwaka, na 23%, 31% na 34% katika kila nchi hizo wameolewa kabla ya kufikisha miaka 18. UNFPA ilitabiri mwaka 2020 kwamba kwa sababu ya janga la COVID-19, ongezeko la unyanyasaji wa kijinsia, kufungwa kwa shule na mdororo wa kiuchumi kutaweka wasichana wengi zaidi katika hatari ya ndoa za utotoni; milioni 13 zaidi duniani kote kufikia 2030. Mabadiliko ya seismic inahitajika kwa wasichana ambao wako hatarini leo.
Hali ya ndoa za utotoni nchini Tanzania
Katika makala iliyotolewa na Girls Not Brides What we've learnt from the national survey on child marriage in Tanzania wanaeleza kuwa Ili kuelewa vyema kuhusu ndoa za utotoni nchini Tanzania na namna bora ya kukabiliana nazo, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (MOHCDGEC) ilifanya utafiti wa kitaifa kwa kuungwa mkono na wajumbe kadhaa wakiwapo Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF). Aidha mnamo mwaka 2016 katika ripoti ya Child Marriage Survey walimulika maeneo yenye kiwango kikubwa cha ndoa za watoto nchini Tanzania kama ifuatavyo:
Picha: Ramani inaonesha mikoa yenye asilimia kubwa ya ndoa za Utotoni nchini Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2016
Zaidi ya hayo kulingana na utafiti wa (MOHCDGEC) na CDF walieleza kuwa, asilimia 37 ya wasichana nchini Tanzania huolewa kabla ya kutimiza miaka 18. Hii inatokana na asilimia ya wanawake wenye umri wa miaka 20-24 walioolewa kabla ya kufikisha miaka 18. Lakini sio wasichana wote wanakabiliwa na kiwango sawa cha hatari.
Mikoa mingine ina viwango vya juu kuliko mingine, Shinyanga na Tabora zikiwa na viwango vya hadi 59% na 58% wakati Dar es Salaam na Iringa zina viwango vya chini hadi 19% na 8%. Wasichana wanaoishi vijijini na/au wanaotoka katika familia maskini pia wana uwezekano mkubwa wa kuolewa mapema.
pia, takwimu za Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya (TDHS), 2015-2016 zilionyesha kuwa asilimia 36 ya mabinti wenye miaka 20 hadi 24 waliolewa kabla hawajatimiza umri wa miaka 18. Kwa mujibu wa Utafiti wa Demografia ya Afya nchini (TDHS) wa mwaka 2010 mikoa yenye viwango vikubwa vya ueneaji wa ndoa za utotoni hapa nchini ni Shinyanga (59%), Tabora (58%), Mara (55%) na Dodoma (51%).
Hii ni sawa na kusema kuwa kwa wastani, wasichana wawili kati ya watano huolewa kabla hawajatimiza umri wa miaka 18.
Madhara na Athari za ndoa za utotoni kwa ujumla
Relief Web Internation wanaeleza kuwa Ndoa za utotoni huhatarisha afya, elimu na usalama wa wasichana.
- Wanaongeza kuwa ndoa za utotoni mara nyingi huwazuia kufikia uwezo wao kamili wa kiuchumi na kijamii, na huwaweka wasichana katika hatari kubwa ya unyanyasaji wa kijinsia, hatari za kupata mimba za utotoni, fistula ya uzazi na VVU.
- UNICEF wanaeleza kuwa takriban wasichana 95 kati ya 1,000 hujifungua wakiwa na miaka kati ya 15 na 19, kabla ya miili yao kuwa tayari kwa uzazi salama.
Hali hii ya kujifungua mapema husababisha vifo na majeraha kwa akina mama wengi wachanga. UNICEF wanabainisha kuwa Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ni pamoja na kuleta usawa wa kijinsia ili kukomesha ndoa za utotoni ifikapo 2030.
Muelekeo wa ya mapambano ya kukomesha ndoa za utotoni kwa ujumla wake
Mnamo mwaka wa 2018, UNICEF ilikadiria kuwa katika miaka kumi iliyopita, viwango vya ndoa za utotoni vilipungua kwa 15% ulimwenguni. Hata hivyo, maendeleo kuelekea kukomesha ndoa za utotoni hayafanani katika kila sehem ukizingatia jiographia na nchi mbalimbali.
Chanzo cha picha na Data ni Save the Children
Picha 2: Chati inaonesha maendeleo ya mapambano dhidi ya ndoa za utotoni katika maeneo mbalimbali ulimwenguni
Katika uchambuzi huo wa data uliotolewa na UNICEF mwaka 2018 ulieleza kuwa katika muongo mmoja viwango vya ndoa za utotoni vilipungua kwa 15% duniani kote. Katika ngazi ya kikanda, baadhi ya maeneo yameonesha maendeleo makubwa huku mengine yakiwa nyuma.
Maendeleo kuelekea kukomesha ndoa za utotoni yamefanyika kwa kasi tofauti katika maeneo yote: wakati baadhi wamepiga hatua kubwa mbele, wengine wako nyuma. Katika hali nyingi, maendeleo katika muongo mmoja uliopita (2010-2020) hayajalingana na maendeleo yaliyopatikana katika muongo uliopita (2000-2010). Katika nchi za Ulaya ya Mashariki na Asia ya Kati, viwango vinaongezeka.
Hitimisho: Ndoa za utotoni ni miongoni mwa tatizo kubwa linalowakumba wanawake wenye umri chini ya miaka 18 hivyo ni jukumu la kila mwanajamii popote duniani kuanzia ngazi binafsi na familia kuunganisha nguvu kupinga uvunjaji wa haki za wanawake hawa.
Serikali iendelee kuboresha Sheria kuhusu Ndoa za Utotoni na kuongeza ukali wake ili kutokomeza hali hii.
Zaidi ya hayo Wanajamii waendelewe kupewa elimu na kuelezwa madhara yanayoweza kutokea kutokana na Ndoa katika umri mdogo/utotoni