Ndo unaposhangaa mtu kuamua maisha ya familia ya ndani ya mumewe. Nadhani watu wamelipukia matumizi ya mitandao ya kijamii mfano wa mbwa aliyefunguliwa toka kwenye cage. Binafsi sidhani kama ni sahihi kuweka mapicha ya watoto wadogo kwenye mitandao, wakue waamue watakavyo.
Kimsingi ndoa za zamani zilidumu kwa vile mfumo ulikuwa kandamizi na wanawake walikuwa moulded kukubali kukandamizwa, hata kwama walikuwa wakiugua maumivu ya ukandamizwaji, udhalilishwaji kutokana na mfumo wa kijamii lulokuwepo (mfumo dume). Mwanamke anayetoka kwenye ndoa kwa kukataa manyanyaso toka kwa mume au ndugu wa mume alionekana dhaifu, asiyefaa, na anayestahili kutengwa na wanajamii wote (sio ndugu wa mume tu bali hata ndugu wa mwanamke huyo).
Hivyo basi naungana na wote waliosema kuwa uthabiti wa mwanaume katika kuonyesha msimamo wake kwa mkewe dhidi ya mashambulizi toka kwa mume una afasi kubwa sana katika kuokoa ndoa hizi.
Kingine ni kuelewana (understanding each other). Kila binadamu ana mapungufu, hakuna mtimilifu abadan. Hivyo basi pamoja na elimu tulizonazo, teknolojia tuliyonayo, maendeleo na mabadiliko ya kiutamaduni tunayokumbana nayo (hasa kwenye inter tribal na religion marriages) ni muhimu kuwa wawazi na kujadili mapungufu ya wenza wetu. Na katika kujadiliana tukubali kutokubaliana bila kuweka inferiority complex an magrudges juu ya wenza wetu. Flexibility kwenye yale yapasayo iwepo, sio mtu unakuwa na msimamo kama chuma cha pua, yaani hadio uone matokea ndio ukubali kubadilika.