Ndoa zenye Utata..

Ndoa zenye Utata..

...Contadictions kibao...

...jamani naomba nisaidieni, je kuna ndoa kweli hapa iwapo................

...ila sidhani kama kuna sehemu yoyote ambayo nimesema huo ni utaratibu wao waliojiwekea wenyewe..

sijui ila nafikiri ingekuwa ni utaratibu wao sidhani kama angekuwa analalamika na kutaka ushauri kwa watu nje ya familia.

inawezekana ukweli akaujua yeye mwenyewe

...ila mimi nimewakilisha kile nilichokiona kwa macho- face value of the story

Nini mtazamo wako katika ndoa za aina hii?

...ndiyo maana wakasema "siri ya mtungi!", ...kwenye ndoa kuna mengi ...kuwa mwangalifu asije shoga'ko akaja kukusuta na "..pili pili usoila yakuwashia nini?"

Usawa kwa wanawake Afrika bado sana.....
Hiyo mizani kuna wakati italemea sana upande wa mama then itashindwa kuhimili...sasa inategemea ni kwa kiasi gani mwanamke anatambua uwezo wake. Kwamba na yeye ni "mtu sawa kwenye huo muungano". Wanawake huwa tunaachia mambo yanatutesa wee ukija kuamka...una ugonjwa wa moyo au saratani...tusimeze sumu jamani.
..kumpa mume mshahara wote...hapana huo ni uonevu.
...kumwabudu mume hapana yeye ni mwenzi wako...mheshimu na mpende na tegemea vivyo hivyo toka kwake
....wakwe kumnyenyekea mume...no no no yeye ndio anatakiwa awe anawaheshimu
Ila sishangai hii scenario ni very common sema severity zinatofautiana.
 
Usawa kwa wanawake Afrika bado sana.....
Usawa upi bibie mnaolilia??
Kama huamini dini basi nakubaliana na wewe.........kuran tukufu na Biblia vinasema wazi wazi....mwanamke atakuwa chini ya mwanaume....

......hizi gender gender zenu nyie..haya..!!
 
Tunakubaliana na hayo kuwa tena tumetoka kwenye mbavu zenu. Ila sasa hio isiwe ndo chanzo cha kunyanyasika kwa mwanamke! Laa hasha, na ndio kikaletwa kitu usawa kwa wote. upo hapo! Nyongeza kwa hao wanawake wanaotaka kuwa juu na kuwatawala wanaume nadhani ni pungwani kidogo. Maana nadhani binadamu hawezi kutawalia na binadamu mwenzie zaidi ya Mungu tuu.
 
Salamu ndugu zanguni.... jamani naomba nisaidieni, je kuna ndoa kweli hapa iwapo................

1. Pesa za mume hazieleweki zinapokwenda na ukiuliza ni ugomvi ila za mke anataka ajue ametumiaje na anataka mshahara ukitoka tu basi akabidhiwe na yeye ndie awe anayepanga matumizi. Na mke haruhusiwa kununua hata handkerchief ataambiwa yuko extravagant ila mume anauwezo wa kutumia laki tano au sita within a week ikaisha na asiulizwe matumizi.

2. Mke hatakiwi kusaidia ndugu zake na akiomba pesa kwa ajili ya ndugu zake (mke) basi mume hukasirika hadi mke anajuta...

3. Mume siku zote yuko negative about chochote anachokifanya mkewe ingawaje pesa zikipatikana yeye ndie wa kwanza kuzidai

4. Kila siku mume anatafuta makosa kwa mkewe hata kama ni kwenda na kufukua ya nyuma kabla hawajaoana

5. Mume anapenda aabudiwa hata na wakwe zake. kwake yeye wakwe zake si kama wazazi bali watumwa ambao wanastahili kumnyenyekea yeye.

Kwa upande wangu mimi nahisi kama huyu mume anamtumia tu huyu mdada na hana mapenzi ya kweli nae hivyo si ajabu akamwaga huko mbeleni mambo yake yakishakuwa mazuri....

Nini mtazamo wako katika ndoa za aina hii?

Kwa kweli hapa huyu dada anamakosa MAKUBWA sana kama walivyotangulia kusema wenzangu. Ushauri wangu ni huu: akae kitako chini yeye na huyo bwanake amueleze from A-Z bila uonga na kwamsimamo ila kwa upole ofcourse. Then kama bwana akianza kuleta za kuleta awaite wapambe wake wa harusi then ikishindikana afate taratibu zote za sheria waachane mapemaa kabla ya kuja kuumia zaidi hapo mbele. Nawatakia kila la heri this is what is called LOVE IS BLIND AND IN THE DARK.
 
Ndugu Mwanajamii,

Kutokana na maelezo yako hapo, kwangu mimi, hapana ndoa na kama ipo i mashakani.

Mzee Kenneth Kaunda aliuita urafiki/ndoa wa/ya "farasi na mpandaji. Mimi nitaiita ndoa hii ni ya "bwana na mtwana/kitwana wake/chake.

Ule mpango wa kizamani kati ya mume na mke ni wa "kishenzi" na ukiendelezwa katika karne hii, mimi nitauita wa "kihuni" na haufai.

Mke ni "equal partner" wa mume na mume ni vivyo, vinginevyo kila mmoja aambae zake.
 
Tunakubaliana na hayo kuwa tena tumetoka kwenye mbavu zenu. Ila sasa hio isiwe ndo chanzo cha kunyanyasika kwa mwanamke! Laa hasha, na ndio kikaletwa kitu usawa kwa wote. upo hapo! Nyongeza kwa hao wanawake wanaotaka kuwa juu na kuwatawala wanaume nadhani ni pungwani kidogo. Maana nadhani binadamu hawezi kutawalia na binadamu mwenzie zaidi ya Mungu tuu.

talking of the oppressor and the oppressed!
 
1. Pesa za mume hazieleweki zinapokwenda na ukiuliza ni ugomvi ila za mke anataka ajue ametumiaje na anataka mshahara ukitoka tu basi akabidhiwe na yeye ndie awe anayepanga matumizi. Na mke haruhusiwa kununua hata handkerchief ataambiwa yuko extravagant ila mume anauwezo wa kutumia laki tano au sita within a week ikaisha na asiulizwe matumizi.

Inaelekea huyu bwana ni control freak fulani. He gets pleasur from being on top even if it means stepping on his loved one's feet. Pengine kosa kubwa ni kwamba the lady may have not tried to stand for herself. Many women Tanzania do not know how to behave when relationships shift from girlfriend/boyfriend to spouses. In fact even men do not know how to behave as husbands should or are expected to. Ndio unakuta wengi wanaanguka katika matatizo kama haya. wengi mumetoa suggestions ambazo upande mmoja havimjengi mlengwa moja kwa moja bali ni mmoja wetu atafikisha ujumbe kwa mlengwa. Wengi pia humu ndani hawana ndoa so please lets not point fingers. Kila ndoa ina matatizo yake. Y mwenzetu ndio hii. Kumbukeni 'love is blind' she may have seen the signs but chose to ignore them.

2. Mke hatakiwi kusaidia ndugu zake na akiomba pesa kwa ajili ya ndugu zake (mke) basi mume hukasirika hadi mke anajuta...
Hili halinishangazi maana ni kotekote matatizo kama haya yanakuwepo ila kwa mtu kutokutaka kuelezea kutokubaliana kwake katika utoaji wa msaada kwa ndugu naona ni kutomkumtendea haki mwenzi wako.

3. Mume siku zote yuko negative about chochote anachokifanya mkewe ingawaje pesa zikipatikana yeye ndie wa kwanza kuzidai
He just wants to be on top but let me tell you one funny thing about people with such characters. They are never in control! They may think they are ila bibie akisimama kidete this guy will derail and crash ila unfortunately hatujui katika hili la bibie kusimama kidete kunaweza kutomuathiri. Maana guys like him will always want to take the fall with someone else. These are classic signs of psychopaths and sadists

4. Kila siku mume anatafuta makosa kwa mkewe hata kama ni kwenda na kufukua ya nyuma kabla hawajaoana
Refer back to point 3

5. Mume anapenda aabudiwa hata na wakwe zake. kwake yeye wakwe zake si kama wazazi bali watumwa ambao wanastahili kumnyenyekea yeye.
Katika hili huyu kijana, I assume ni kijana, amekosa nidhamu ya hali ya juu. Aidha amelewa madaraka, pesa au wanawake wanaompapatikia. Ila akumbuke lililo na mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Kuna wenzake walikuja kufa vifo vya aibu kutokana na tabia zao. Yaani walijikuta wakiogeshwa na baba mkwe na mama mkwe maana hakuna ndugu aliyetaka kuwahudumia. Wazazi wako sio wazazi wako pekee, wa mkeo pia ni wazazi wako

Kwa upande wangu mimi nahisi kama huyu mume anamtumia tu huyu mdada na hana mapenzi ya kweli nae hivyo si ajabu akamwaga huko mbeleni mambo yake yakishakuwa mazuri.... Ni kweli kabisa hana mapenzi au tuseme hajui kitu mapenzi. Ni limbukeni wa aina fulani

Mwanajamii umetupa story ya upande mmoja sidhani katika haya uliyoyaeleza tunahitaji kufahamu mke aliwahi kumkosea ndio maana kawa hivi kitabia. Hata kama una grudge na mtu yeyote awaye hasa mkeo huwezi ukafikia mahala hapa kama wewe mwenyewe ndiye mwenye tabia chafu.

This poor lady has lost control of her life and her husband is finding satisfaction in this is purely pathetic. Ninampa pole ila pia anapswa kujiuliza maswali mengi. Ni rahisi sana kwa mtu wa nje kusema waachane ila kumbuka sababu za wao kufunga ndoa hatuzijui
 
Ndoa ipo ila imepinda. The man is so selfish and dictator. Ashukuru amempata mke mpole na mvumilivu....na...siku akimpoteza huyo mke wake...atajuta the rest of his life...Lakini tabia aliyo nayo can be traced back ktk jinsi alivyolelewa na mazingira aliyokulia...mazingira yanayepelekea kuwanyima wanawake sauti ndani ya nyumba na kuwanyanyasa.....Inabidi marafiki walio karibu nae wamueleweshe ajirekebishe...aelewe kwamba familia zinazoshamiri ni zile ambako kuna mashauriano na masikilizano kati baba, mama na watoto...nyakati za control and command zimepita...
 
Ktk dunia ya vyama tele vya ktetea wanawake haya bado yapo? This is paradox. Si lazima kuwa ktk ndoa ndio uheshimiwe, mweleze atoke ktk uhusiano huo aone jinsi NYAMAUME nyingine zinavyojua kulea na kubembeleza
 
Jamani aksanteni sana kwa ushauri wenu kwa kweli umenisaidia na kunipa moyo wa kuweza kumshauri dadangu ili ajue kipi cha kufanya. Nilikuwa naogopa kumshauri mwanzo kwa kuhofia kuwa huwenda nitakuwa nakosea kwa kuwa mie sijaolewa mambo ya ndoa siyajui.

Aksanteni sana
 
Ndoa zenye utata.............. laiti kama kusingekuwa na mambo ya kupelekana kwa kasisi sijui, maumivu ndani ya ndoa wala yasingekuwepo nafikiri
 
Ndoa zenye utata.............. laiti kama kusingekuwa na mambo ya kupelekana kwa kasisi sijui, maumivu ndani ya ndoa wala yasingekuwepo nafikiri

Kasisi ni shahidi tu,ndoa ni yao wanaofunga. Tunaishi mara moja tu huku duniani. Ni muhimu pia kujua malezi na aina ya familia ambayo mtu wako/mtarajiwa wako anatoka. Angalia sana nduguyo atakosa vyote.
 
hilo wengi wanalisahau.
 
Jamani aksanteni sana kwa ushauri wenu kwa kweli umenisaidia na kunipa moyo wa kuweza kumshauri dadangu ili ajue kipi cha kufanya. Nilikuwa naogopa kumshauri mwanzo kwa kuhofia kuwa huwenda nitakuwa nakosea kwa kuwa mie sijaolewa mambo ya ndoa siyajui.

Aksanteni sana

Ndugu yangu mbona hapa umejichanganya tena unakumbuka ulivyoniPM uliniambiaje halafu hapa unasema siyo wewe ila yanamsibu dada yako jamani mpaka sina hamu tena ya kuchangia kitu tena.
 
Back
Top Bottom