ninao mchango kidogo kuhusiana na kibandiko hiki,
1. wosia ni hati ya maandishi ambayo mtu anaandika akiwa na akili timamu, bila kushurutishwa na mtu yeyote kuanisha ni jinsi gani angependa malii zake zigawanywe pindi atakapofariki.
2. wosia ni siri kwa maana kwamba wale ambao watanufaika na mali zao ndani ya huo wosia hawapaswi kujua
3. wosia lazima usainiwe na mashahidi wasiopungua wawili
4. mali zipi zijumuishwe kwenye wosia---hilo linatagemea na muandika wosia ni kitu gani kwake anakidhamini na angependa kigawanywe/apewe mtu mwingine atakapofariki,lakini mara nyingi watu huanisha mali kama, nyumba, viwanja, pesa kwenye account mbalimbali, share kwenye makampuni, magari, vito vya thamani,na vinginevyo. NB: kama unadhani ni vyema ukasema friji na makabati ya nyumbani kwako nani apewe si mbaya ikiwa unahisi hivyo vitu vinaweza kuleta utata katika familia yako pindi utakaofariki..lol
5. kwa mujibu wa sheria ya ndoa (LMA 1971) kifungu cha 56 kinaruhusu mwanamke aliyeolewa kumiliki mali, kuingia kwenye mkataba,kushtaki au kustakiwa kwa jina lake!
6. pia kifungu cha 58 cha sheria tajwa hapo juu kinasema kuwa kama hakuna makubalino yeyote katika ya mume na mke basi mume au mke haruhusiwi kumkataza mwenzie kununua,kumiliki au kuuza/kugawa mali anayomiliki kwa jina lake au kumtaka mwenzie abadilishe umiliki wa mali alizonazo kwa kigezo cha ndoa, lakini mume au mke hawezi kuuza au kijimilikisha nk kwa nyumba wanayoishi pamoja katika kipindi chao cha ndo bila ridhaa ya mwezie
7.pia kifungu cha 60 cha LMA sheria ya ndoa kinasema kuwa katika kipindi cha ndoa mume au mke akimiliki mali kwa jina lake basi mali hiyo itachukuliwa kuwa mwenye jina ndie mmiliki wa mali hiyo unless ushahidi kuthibitisha mali hiyo inamilikwa na mke na mume utakopotolewa kwa mfano mke anamiliki gari kwa jina lake lakini pesa ya kununua hiyo gari ni mume ndio aliyetoa basi mume anatakiwa kuthibitisha kuwa yeye ndio alimpa mke hizo pesa eg, bank statements nk....
8. kwa kifupi sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inaruhusu mke na mume kuwa na mali either jointly or as individual
9.mali ambayo mke na mume hawana haki kudeal nayo bila ya ridhaa ya mwingine ni matrimonial home na mali ambazo wamezipata katika kipindi cha ndoa na zinaonyesha kuwa both mume na mke wanamiliki kwa pamoja!
NAOMBA KUWASILISHA N I STAND TO BE CORRECTED