asante DARK CITY,
KWA Thread yenye mshiko kwa jamii nzima,
Kuandika wosia ni jambo jema sana na naamini siyo kwa wanandoa tu,japo huko ndiyo kwenye migogoro mikubwa mingi,
mi naona wosia ni jambo jema kutekelezwa na kila mtu mwenye mali yake ili kuepusha,
migogoro ya mrithi nani pindi atakapokufa,
Pamoja na umuhimu huo ila pia mimi naomba Gharama za kuandaa na kutunza huo wosia,
ZIPUNGUZWE ILI KILA MTU AWEZE KUMUDU GHARAMA ZAKE,
Mfano pale RITA gharama za wosia na utunzaji wake zipo juu sana,
na nadhani zimeongezeka ksb mwaka huu sijajua wanacharge kiasi gani,
mi nina wosia wangu pale RITA ila nina kajideni ka mwaka huu na mwaka jana sijalipia,
Kwa hiyo kwa mfano nikifa leo basi wafuatiliaji wangu watalazimika kulipia kwanza,
kabla ya kukabidhiwa wosia wangu.
SIJUI KAMA NA HUKO KWINGINE KUNA GHARAMA KUBWA ZA KUANDAA WOSIA PAMOJA NA UTUNZAJI WAKE.
KUANDAA WOSIA WALA SIYO UCHURO KAMA BAADHI YA WATU WANAVYODHANI,
NA HAIJALISHI UNA MALI KIASI GANI,
HATA UKIWA NA GAUNI MOJA AU SURUALI MOJA NI BORA KUANDIKA NANI ANAWAJIBIKA ,
KUCHUKUA AU KUTUNZA PINDI UTAKAPOKUFA,AU PIA UNATAKA UZIKWE VIPI NA WAPI ,
ILI KUEPUSHA MATATIZO BAADA YA KIFO CHAKO.