mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Waziri Kivuli wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, anayeshughulikia masuala ya Bunge, Sera, Vijana, Kazi na Ajira, Mhandisi Ndolezi Petro, amekosoa uchaguzi wa mwaka 2020, akidai kuwa haukuwa huru na haki.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara jimboni Bumbuli, Mkoani Tanga, Mhandisi Ndolezi alieleza kuwa uchaguzi huo "ulikuwa ni uchafuzi" ambao uliwanyima wananchi nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Katika hotuba yake, Mhandisi Ndolezi amelitaka Jeshi la Polisi kutokubali kutumika kisiasa katika michakato ya uchaguzi, akisema kuwa polisi wanapaswa kuwaachia wanasiasa waendelee kunadi sera zao kwa wananchi, na hatimaye wananchi wachague yule anayeonekana kuwafaa zaidi.