JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Pia soma ~ Baada ya Mwenyekiti, Katibu wa Jumuiya wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) naye adaiwa kukamatwa na Jeshi La Polisi usiku huu
=========================
TUJIKUMBUSHE TAARIFA YENYEWE
Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO) umesema Katibu wa NETO Daniel Edger Mkinga amekamatwa Kibaha Miembe Saba nyumbani kwake majira ya usiku wa saa tatu kasoro kwa tuhuma za kuwepo kwenye Jumuiya ya NETO ambapo waliofika nyumbani kwake kumkamata ni Balozi, Mjumbe na Askari watatu kutoka kituo cha Polisi Maili Moja Kibaha, Pwani.
Taarifa iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa NETO, Agnesss Mpundi imesema “Tunaomba Wanasheria wenye mapenzi mema na Shirika la Utetezi wa Haki za Binadamu watusaidie kupata uhuru wake, tunaeendelea kuwakumbusha kuwa NETO sio Chama cha kisiasa, genge la Wahalifu wala halina nia yoyote ovu dhidi ya amani ya Nchi yetu, adhima kuu ya NETO ni kuomba ajira za Walimu wa Serikali na kusisitiza kufanyia kazi makala tuliyoiandikia Serikali”
“Kwa Wakazi wa Dar es salam na Pwani kwa ujumla,(Walimu tusiokuwa na ajira) tukutane leo katika kituo cha polisi Kibaha Mail moja kumwona katibu wetu Daniel, aliyekamatwa hapo jana usiku, sisi sio Wahaini, tunataka ajira, ajira ni haki yetu”
Itakumbuka juzi Mwenyekiti wa NETO Joseph Paulo Kaheza alikamatwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Geita (RCO) kisha akaachiwa kwa dhamana jana ambapo Polisi walisema walimkamata kwa mahojiano kwa kuongoza umoja huo ambao haujasajiliwa.
Chanzo: Millard Ayo