Ndondo Cup, Azam TV acheni huu upuuzi

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Yaani mtu kalipia king'amuzi cha Azam sports HD halafu mnaenda kumuonesha
'ndondo cup'?
seriously?

Hivi Azam wameshindwa hata kuonesha Kagame cup
halafu bila aibu mnaonesha NDONDO CUP?

Michuano ya kimtaani mtaani ambayo haipo hata ratiba ya TFF?

Michuano hiyo ni burudani zaidi kuliko mpira wa kweli..umaarufu wake ni wa vituko vya mashabiki tu.....Azam kama mko serious na mnataka kushindana na DStv
please stop this........

Baada ya Spanish La liga basi tuoneshe Africa club championship au tuonesheni ligi ya EGYPT yenye timu kama AL-ahly na Zamalek
kuna vitu vingi vya kuonesha vya afrika nzima na sio ndondo cup

Mnajiabisha saaana, so mediocre.
 
dahh yaani ww usingekuta sheria mpya ya mrandao sijui ningekuambiaje.... ! so ww umeona ndondo cup ni upuuzi lakini kagame ndio unaisifia ... bado Liwassa ana kazi kubwa saana kuondoa ujinga kwenye vichwa vya watanzania .
 
dahh yaani ww usingekuta sheria mpya ya mrandao sijui ningekuambiaje.... ! so ww umeona ndondo cup ni upuuzi lakini kagame ndio unaisifia ... bado Liwassa ana kazi kubwa saana kuondoa ujinga kwenye vichwa vya watanzania .

Azam ni continental ...wako zaidi ya nchi moja
Ndondo cup ni mashindano ya kimataifa au hata kitaifa?ni ya kimtaa zaidi...hakuna quality football
ndo maana watu wako busy na EPL...investment za aina hii haziendani na quality...
 
Duuuh hizo mechi unazosifia wachezaji wake si wametoka huko? Btw hiyo ndondo cup inaoneshwa 24 hrs hadi ukereke kiasi hiki?
 
azam ni continental ...wako zaidi ya nchi moja
ndondo cup ni mashindano ya kimataifa au hata kitaifa?ni ya kimtaa zaidi...hakuna quality football
ndo maana watu wako busy na epl...investment za aina hii haziendani na quality...

acha ujinga na utumwa wa akili ww , huko ni kukubali kutawaliwa ki akili , mm si shabiki wa mpira ila azam tv imenifanya kama mtanzania kuangalia hii ligi yetu ya nyumbani na timu yangu ni kauzu fc ....... Ww unajisifia na tumu gani ?watanzania tujifunze kupenda vya kwetu jamani.

So upo proud epl ionyeshwe kwe azam hd ,lakini ndondo isionyeshwe kabisa ... Duuuuuh ...nshkamooo
 
Duuuh hizo mechi unazosifia wachezaji wake si wametoka huko? Btw hiyo ndondo cup inaoneshwa 24 hrs hadi ukereke kiasi hiki?

Elewa point please
kama NDONDO cup ingeoneshwa Clouds au tv ingine sina shida
Azam HD wametuambia wanashindana na dstv
michezo ya kimataifa
Je ndondo cup ni michuano ya kimatafa? ya kitaifa?
inasaidia nini?burudani sio?
haipo hata ratiba za TFF....ishu si kukereka ishu nikuwa kuna vitu vingi Azam wanaweza kutuonesha
hawatuoneshi halafu wanaenda kutuonesha kitu ambacho sio interst ya wanamichezo wengi
 


Jaribu kuelewa
ndondo sio ligi daraja lolote TZ
wangeonesha ligi daraja la kwanza au la pili hakuna shida
ndondo cup ni bonanza zaidi......

why wasioneshe michezo ambayo iko kwenye kalenda hata kama ni local?

wameonesha mashindano ya magari local,ligi ya rba na ligi ya vodavom
tunataka hayo zaidi.....sio bonanza
kagame imechezwa tz na ina timu za tz ni muhimu kuliko ndondo cup sababu ya kiwango chake na ni official games
 

Tuwe wakweli, hakuna sehemu wamesema wanashindana na dstv kwenye mechi za kimataifa, wameulizwa kwa nini hawaonyeshi mechi za UEFA au EPL na wamejibu kuwa bado hawajapata haki ya kuonyesha hizo mechi ila wanajaribu na chanzo cha hiyo HD ilikuwa mashariti ya la liga kuonyesha mechi zao ktk ubora wanaoutaka, sasa wewe unaona ni rahisi tu kuonyesha ligi za kimataifa bila kibali maalum? Kagame wakishindwa kuonyesha kwasababu dstv walifika bei zaid yao.
 

Bora umeongea ukweli
walishindwa fika bei ya kagame cup now wanaonesha ndondo cup
nafikiri hiyo statement inajitosheleza.....
 
Wewe jamaa nilikuwa nakuheshimu. Kuanzia leo nmekudharau mno. Kwa taarifa yako hao wachezaji unaowajua wewe unaotaka kuwaona kwenye Kagame 80% wamecheza hizo ndondo. Kama hujui uliza sio kubwabwaja hapa.
 
Hao wa wandondo ndio wanunuzi wakubwa wa bidhaa za Bakhresa kama juice, ice cream, n.k. Ni mpira na biashara rafiki.
 
Wewe jamaa nilikuwa nakuheshimu. Kuanzia leo nmekudharau mno. Kwa taarifa yako hao wachezaji unaowajua wewe unaotaka kuwaona kwenye Kagame 80% wamecheza hizo ndondo. Kama hujui uliza sio kubwabwaja hapa.

Jaribu kuelewa ninachokizungumza
kila kitu kina standards
hata michuano ya umiseta pia wachazaji wake huja kuchezea Kagame cup
but ukiambiwa hii ni UMISETA unajua ni michuano ya kiwango gani

Ndondo cup ni bonanza....tukisema tuanze ku rate mashindano yote ya mpira wa miguu TZ
au tu rate sports events zote kubwa tz... sijui ndondo cup itashika nafasi ya ngapi
but nina uhakika haipo top 5 ya mpira wa miguu peke yake
sio big games...na kumbuka sijasema isioneshwe na TV nimesema azam sports hd
ambayo ni ya kulipia waoeneshe games zenye standars inayoeleweka
Ndondo cup hata TFF haipo kwenye calender yake
 

Ndio maana nikasema kama hujui uliza? ndondo ni bonanza? utachekwa.
Kuna bonanza gani watu wanalipa kiingilio kuiangalia na wanajaa kushinda hata mechi za ligi kuu?
halafu umagharibi usituharibu. Vya nyumbani tuvipende na kuvithamini pia.
 
Azam TV wanachojaribu ni kugusa kila eneo ili waburudishe kila aina ya wateja wake. Kama wewe unatakamani waonyeshe Kriketi wengine hizo ndondo wanatamani pia. Kwani zile mechi za pre season ziko kwenye kalenda ya Fifa au TFF mbona AzamTV wameonyesha.
 
Kwa watu walianza kuangalia ndondo tangu 1990's enzi zile za Lucky Rangers tunakushangaa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…