Ndondo CUP Dodoma 2024 Yazinduliwa kwa Kishindo

Ndondo CUP Dodoma 2024 Yazinduliwa kwa Kishindo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WhatsApp Image 2024-09-08 at 20.41.02(1).jpeg

-Mbunge Mavunde atangaza zawadi nono za washindi

-Anuia kuendeleza na kuvikuza vipaji vya Vijana Dodoma

-GSM Water na Asas Dairies wanogesha mashindano kwa ufadhili

Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde leo amezindua rasmi ya Ndondo Cup Dodoma 2024 ambayo yanaratibiwa na Mbunge Mavunde kwa ushirikiano na Clouds Media Group.

Katika Mashindano hayo yanayoshirikisha Timu 32,m Bingwa wa Mashindano atapata Tsh 15,000,000 na Mshindi wa pili Tsh 7,000,000.

Aidha Mbunge amezishukuru Kampuni za GSM na ASAS kwa kuwa sehemu ya ufadhili wa mashindano hayo ambayo yamelenga kwa kiasi kikubwa katika kuibua na kuviendeleza vipaji vya vijana wanamichezo.

“Ukiacha burudani,katika mashindano haya tumejipanga kuibua vipaji na kuviendeleza kwa kuwa sisi kwetu michezo si burudani tu bali kwetu sisi michezo ni AJIRA”Alisema Mavunde

Akizungumza katika mahojiano leo,Mratibu wa Ndondo Cup Ndg. Yahaya Mohamed “Mkazuzu” amesema mashindano ya mwaka huu ya Ndondo yanabeba ujumbe juu ya elimu ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na pia kwa kushirikiana na Watu wa Marekani elimu inatolewa juu ya masuala ya Afya na hasa kujikinga na maambukizi ya UKIMWI.

WhatsApp Image 2024-09-08 at 20.41.00(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-09-08 at 20.41.03(1).jpeg

WhatsApp Image 2024-09-08 at 20.41.03.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-09-08 at 20.41.00.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-08 at 20.41.00.jpeg
    145.8 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-09-08 at 20.41.01.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-08 at 20.41.01.jpeg
    126.9 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-09-08 at 20.41.02.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-08 at 20.41.02.jpeg
    221.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-09-08 at 20.41.04.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-08 at 20.41.04.jpeg
    157.1 KB · Views: 4
Zawadi kubwa kuliko zawadi kombe la mapinduzi
 
Watu wanatafuta kura 2025,kila mbunge jimboni kwake kuna ndondo cup, wanaamini wanatengeneza mvuto kwa vijana. Yaani wabunge sasa hivi walivyo na presha za 2025 hata mchezo wa marede wanaufadhili.
 
Back
Top Bottom