NDONDO CUP: Mwamuzi atekwa huku mechi ikiendelea

Chumchang Changchum

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2013
Posts
5,988
Reaction score
6,226
MASHABIKI wa timu ya Friends Rangers, jana Jumanne uvumilivu uliwashinda baada ya kuchukua maamuzi magumu ya ‘kumteka’ mwamuzi wa pembeni aliyekuwa akichezesha mchezo wao dhidi ya Misosi FC kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni, Dar.

Mchezo huo wa hatua ya 32 bora ya michuano ya Sports Extra Ndondo Cup, ulimalizika kwa Misosi kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lilofungwa na Idd Selemani dakika ya 31.

Championi lililokuwepo uwanjani hapo, liliwashuhudia mashabiki hao dakika ya 80 wakimbeba mwamuzi huyo ambaye jina lake halikufahamika haraka kwa madai kuwa alikuwa akiionea timu yao.

Hata hivyo, mwamuzi huyo aliachiliwa na kurudi uwanjani kumalizia mchezo huo ambao muda mwingi ulitawaliwa na vurugu zilizokuwa zikifanywa na mashabiki wa Friends.

Chanzo cha habari: Marafiki na Gazeti la Uwazi
 
nakumbuka enzi za Abajalo na sinza stars
 
nakumbuka enzi za Abajalo na sinza stars
Abajalo,Falu Dume na Ashanti..Ilikuwa fainal.Falu Dumentunacheza na Ashanti watoto wa Ilala ule mziki si wa kitoto maana nikiziangalia picha natamani nirudi Ujahilini...Dah
 
Ukitaka kuona watu fyatu, nenda ndondo cup, kuna vitu wanafanya hadi unashindwa kuelewa kama kichwani mwao kuna hata chembe ya ubongo? yani medula oblongata zimekata network kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…