Jana nilikuwa nyumbani naangalia fainali ya mpira mashindano amabayo hivi karibuni yamejizolea umaarufu mkubwa hasa kwa vibweka na manjonjo ambayo huambatana na mashindano hayo!, ilikuwa ni fainali ya Ndondo cup, nia nzuri ya mashindano haya ni kusaka vipaji ni jambo jema ambalo hakuna mtu atapinga, lakini kuna kitu kilitokea pale uwanjani ambacho kinastahili kuangaliwa kwa jicho la tatu, kama yalivyo mashindano hayo ni kusaka vipaji, kuliibuliwa vipaji vingi ikiwa ni pamoja na mwamuzi wa Jana ambaye ni kijana mdogo ambaye alionekana ni makini Hadi kupewa jukumu hilo kuchezesha fainali hiyo.
Utata ulikuja mara baada ya goli la Misosi ambalo limeacha maswali mengi ni kitendo cha mchezaji wa Misosi "kumvamia" golikipa wa Gomz na kumpora mpira hatimaye kuweza kuweka mpira kimiani na kuwa bao la kusawazisha kwa timu hiyo,
Kwangu Mimi sikuona uhalai wa bao hilo sijui watu wengine wana mawazo gani juu ya hili namuona refa hakuwa na uzoefu wa kutosha kuruhusu bao lisimame, badala yake mshambuliaji wa Misosi alitakuwa apewe onyo kwa kupewa kadi,
Ukweli kwa hatua ile na ikizingatiwa ilikuwa ni fainali ilistahili iwe imechezeshwa na muamuzi wa hali ya juu, kama ambavyo tuna shuhudia mashindano mengine makubwa huweza kuamuliwa na waamuzi wazoefu, kama lengo ni kuibua vipaji vya marefa nafikiria zoezi Hilo lifanyike kwenye hatua za mwanzo wa mashindano hayo lakini sio katika fainali
Sent using Jamii Forums mobile app