Ndondo Cup na u dondo

Ndondo Cup na u dondo

bulunga

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2010
Posts
303
Reaction score
49
Jana nilikuwa nyumbani naangalia fainali ya mpira mashindano amabayo hivi karibuni yamejizolea umaarufu mkubwa hasa kwa vibweka na manjonjo ambayo huambatana na mashindano hayo!, ilikuwa ni fainali ya Ndondo cup, nia nzuri ya mashindano haya ni kusaka vipaji ni jambo jema ambalo hakuna mtu atapinga, lakini kuna kitu kilitokea pale uwanjani ambacho kinastahili kuangaliwa kwa jicho la tatu, kama yalivyo mashindano hayo ni kusaka vipaji, kuliibuliwa vipaji vingi ikiwa ni pamoja na mwamuzi wa Jana ambaye ni kijana mdogo ambaye alionekana ni makini Hadi kupewa jukumu hilo kuchezesha fainali hiyo.

Utata ulikuja mara baada ya goli la Misosi ambalo limeacha maswali mengi ni kitendo cha mchezaji wa Misosi "kumvamia" golikipa wa Gomz na kumpora mpira hatimaye kuweza kuweka mpira kimiani na kuwa bao la kusawazisha kwa timu hiyo,

Kwangu Mimi sikuona uhalai wa bao hilo sijui watu wengine wana mawazo gani juu ya hili namuona refa hakuwa na uzoefu wa kutosha kuruhusu bao lisimame, badala yake mshambuliaji wa Misosi alitakuwa apewe onyo kwa kupewa kadi,

Ukweli kwa hatua ile na ikizingatiwa ilikuwa ni fainali ilistahili iwe imechezeshwa na muamuzi wa hali ya juu, kama ambavyo tuna shuhudia mashindano mengine makubwa huweza kuamuliwa na waamuzi wazoefu, kama lengo ni kuibua vipaji vya marefa nafikiria zoezi Hilo lifanyike kwenye hatua za mwanzo wa mashindano hayo lakini sio katika fainali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuna mambo mengi ya kujadili

Hilo la ndondo lingepelekwa fb ingefaa sana

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Inaonyesha sio mfatiliaji wa mpira, pole sana pale akumvamia ni uzembe wa kipa tu ule.
Mkuu naomba ufafanue ni uzembe ni upi, maana golipkia alikuwa na mpira mkononi ingelikuwa mpira umerushwa na kipa kwa adui na akafunga bao hilo halina ubishi undelikuwa ni uzembe lakini sio kwa hali ile
 
Tuna mambo mengi ya kujadili

Hilo la ndondo lingepelekwa fb ingefaa sana

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
Sio lazma kila Uzi uchangie alfu usipende kudharau mada za watu na kujifanya upo perfect sana embu yaandke hapa hayo mambo yako ya muhimu unayotaka uyajadili
 
Sio lazma kila Uzi uchangie alfu usipende kudharau mada za watu na kujifanya upo perfect sana embu yaandke hapa hayo mambo yako ya muhimu unayotaka uyajadili
Ok ahsante

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Jana nilikuwa nyumbani naangalia fainali ya mpira mashindano amabayo hivi karibuni yamejizolea umaarufu mkubwa hasa kwa vibweka na manjonjo ambayo huambatana na mashindano hayo!, ilikuwa ni fainali ya Ndondo cup, nia nzuri ya mashindano haya ni kusaka vipaji ni jambo jema ambalo hakuna mtu atapinga, lakini kuna kitu kilitokea pale uwanjani ambacho kinastahili kuangaliwa kwa jicho la tatu, kama yalivyo mashindano hayo ni kusaka vipaji, kuliibuliwa vipaji vingi ikiwa ni pamoja na mwamuzi wa Jana ambaye ni kijana mdogo ambaye alionekana ni makini Hadi kupewa jukumu hilo kuchezesha fainali hiyo.

Utata ulikuja mara baada ya goli la Misosi ambalo limeacha maswali mengi ni kitendo cha mchezaji wa Misosi "kumvamia" golikipa wa Gomz na kumpora mpira hatimaye kuweza kuweka mpira kimiani na kuwa bao la kusawazisha kwa timu hiyo,

Kwangu Mimi sikuona uhalai wa bao hilo sijui watu wengine wana mawazo gani juu ya hili namuona refa hakuwa na uzoefu wa kutosha kuruhusu bao lisimame, badala yake mshambuliaji wa Misosi alitakuwa apewe onyo kwa kupewa kadi,

Ukweli kwa hatua ile na ikizingatiwa ilikuwa ni fainali ilistahili iwe imechezeshwa na muamuzi wa hali ya juu, kama ambavyo tuna shuhudia mashindano mengine makubwa huweza kuamuliwa na waamuzi wazoefu, kama lengo ni kuibua vipaji vya marefa nafikiria zoezi Hilo lifanyike kwenye hatua za mwanzo wa mashindano hayo lakini sio katika fainali

Sent using Jamii Forums mobile app
Umemsikiliza yule kipa wa GOMZ leo kwenye kipind cha leo tena? Mpira ni mchezo wa makosa na kipa alidhan jamaa yupo Mbali na yeye so akawa anapoteza muda ila jamaa akamzuga chap akaugusa mpira ikawa goli na kosa la kipa ni kuuchezea mpira katikati ya goli angetakiwa atoke pembeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naomba ufafanue ni uzembe ni upi, maana golipkia alikuwa na mpira mkononi ingelikuwa mpira umerushwa na kipa kwa adui na akafunga bao hilo halina ubishi undelikuwa ni uzembe lakini sio kwa hali ile

Goli kipa hakuwa na mpira mkononi, ule ni uzembe na sio kipa wa kwanza kufanya hivyo.
 
Umemsikiliza yule kipa wa GOMZ leo kwenye kipind cha leo tena? Mpira ni mchezo wa makosa na kipa alidhan jamaa yupo Mbali na yeye so akawa anapoteza muda ila jamaa akamzuga chap akaugusa mpira ikawa goli na kosa la kipa ni kuuchezea mpira katikati ya goli angetakiwa atoke pembeni

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza kukiri kosa kama hujui sheria ukweli sheria ziko wazi na goal keeper analindwa na sheria hizo
 
While the ball is in the possession of the goalkeeper, it cannot be played by an opponent. Any attempt to do so may be punished by a direct free kick. "In the possession of the goalkeeper" is defined as the goalkeeper having the ball trapped between one hand and a surface (which may include the other hand, the ground, a goalpost, or the keeper's own body). International Board Decision Two of Law 12 emphasizes that the hand includes any part of the hand or arm. However, as stated in the Advice to Referees on the Laws of the Game (Advice 12.16 and 12.17), the goalkeeper is also considered to be in possession of the ball while bouncing it on the ground or while throwing it into the air. Possession is given up if, while throwing the ball into the air, it is allowed to strike the ground. ...

Additionally,

When is Possession Lost? The critical question is when the goalkeeper has released the ball into play and thus has allowed the ball to be played by an opponent. Based on traditional interpretations of this issue and the International Board's Questions and Answers, the referee should consider the ball as having been released into play after leaving the goalkeeper's hands only if the goalkeeper has completed a throw or kick (punt) and the goalkeeper is not able directly to possess the ball again in his or her hands. Thus, the ball is not playable by an opponent during the entire time it is being held by the goalkeeper (including when the ball is being bounced on the ground) or during the entire process of being released into play (including the action of throwing or kicking/punting the ball). In short, opponents may play the ball only if the goalkeeper has clearly distributed the ball by kicking or throwing it.
 
Asante kwa video, neno possession Lina maana kubwa na limeelezwa kwa kirefu katika sheria za mpira, na maana halisi, ukweli goalkeeper alikuwa in possession of the ball na Hilo bao halikustahili
Broo Mimi nlikuwa uwanjan!

Ule mpira kipa hajaudaka ,

Aliuzuia kwa kifua na kuweka kwenye miguu yke akiwa usawa wa goli kitu ambacho ni uzembe wa kipa ...

Alitakiwa autoe ule mpira pemben ndo afanye vile kwa kitendo cha kutuliza mpira kwa kifua inamanisha mpira unaendelea kuchezwa

kipa alipoteza tyming kuudaka mpira pale kwnye miguu yke kwa uzembe mchezaji wa misosi akauwahi na kufunga.

Mi namsifia mchezaji kwa kutokata tamaa " never finish antil finish"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom