Ndoto gani hutaisahau?

Me niliota naolewa na JK , katika kutoa kiapo nikaganda kdgo ndoto ikaisha.

dah una bahati xana mi nikiota ndoto na hawa jamaa wamo hawa kina Rostam mizizi nawaalibia humo humo,hamna kuremba.
 
mi nkiota nimekutana na rostam namuomba aache wizi..
 
Mimi niliota nakimbizwa na shangazi na yeye alikuwa na uwezo wa kunikamata tu endapo nitapita kwenye kivuli iwe ni chini ya mti au kivuli chochote, basi nilikuwa nakwepa vivuli kama nini, nikiona kivuli tu nakula kona na kurudi juani.

mie ndoto kama hyo huwa inajirudia sana nkamwadisia sista akasema utakuwa mwanga ila she was nt serious
 
Mi niliwah kuota nakula msosi wa maana af kuamka asubuh nikawa na ubao mkali
 
Mi niliota nimekufa ktk kuuaga mwili wangu nikawa kwenye msafara kufika kwenye jeneza nikajiona ndani yake yani nilishtyka!
 
Dah! yaani hii sitaisahau, nimeota namtongoza demu halafu ananiletea mazenguzi nakaa kidogo jamaa anamchukua halafu namwambia niachie namba yako basi akaniambia usiwe na shaka akanipa namba za simu yake, mwishoni akaniambia jina lake na nimtafute kwenye facebook, naamka asubuhi namba ya simu nimeshaisahau ila jina nalikumbuka nikaingia kwenye facebook kumtafuta nikabahatika kumpata dada mmoja matata lakini ni tofauti na niliyemuota na kum-add kama friend, cha kushangaza huyu dada amekuwa ananisumbua sana kunitaka kimapenzi kitu ambacho mi kwangu ni maajabu, hapa nilipo nishaifunga account yangu ya fb
 

unashindwa kukimbia kwa sababu unakuwa umekunja miguu unapokuwa umelala.
 
Sitasahau siku naota niko mbinguni na kupaona plivyo pazuri, nikawa nachekelea kimoyomoyo cha ajabu ndoto ilipokata nikajikuta nipo kitandani nilichukia sana. Lakini nakazana kumpokea Yesu ndani yangu kila siku ili hatimae siku moja nifike huko mbinguni pasipo ndoto.
 

Haya bwana na mawazo yako ya kigalatia!
 
mimi,niliota nimepata remote ya kuforward na kurewind maisha,nikawa naji-rewind nakua mtoto naonekana bright kweli,sasa nikataka nione future ikoje,nikaji-forward,nkajikuta nimeshazikwa na remote iko juu.sitasahau ndoto hiyo.
 
me niliwah kuota nimekutana na wale watoto wa mitaan bas wakanivamia kutaka kunipiga. nikaanza kupambana nao, nliwakatakata kwa mapanga wote mpk wakafa. nilipoamka nlichukia sana hyo ndoto.
 
niliota najamba daah kustuka nikakuta mimavi tele kitandani, nilijiona fedheha sana kwa mdogo angu..
 

kama ulitaka ubaki huko huko, ungeamka ungekunywa sumu afu ulale tena
 
me niliwah kuota nimekutana na wale watoto wa mitaan bas wakanivamia kutaka kunipiga. nikaanza kupambana nao, nliwakatakata kwa mapanga wote mpk wakafa. nilipoamka nlichukia sana hyo ndoto.

Thank you lord that to kill sumone in your dreams is legally accepted.
 

yan mie mpaka leo naota hivo.
 
Kila mara hua naota napigana na watu tofauti tofauti ambao nawaota mara kwa mara ni jakaya na sugu na watu kama kina mesi,ronaldo,neymar na pele yani tunakuwa ulingoni kabisa lakini chakushangaza sijawahi kushinda ata siku moja kama mara ya mwisho mesi alinipa kichapo kizito ila nilikaza lakin raundi ya tano nilisalimu amri yani kuna wakati nilishaota napigana na mdogo wangu akanichapa kwa KO mbaya sana paka saivi akileta jeuri naamua kumuacha tu asije kufanya kweli
 

du pole sana, au ni kibwengo alipita nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…